Mohamed
Bonzo (63yrs) akitoa nasaa baada ya kumpiga bondia chipukizi James
Martin(22 )ambae ni sawa na mwanae wa tatu. Kulia ni Ibrahim kamwe na
kushoto ni Yasin Abdallah-Ustadh
Mohamed Bonzo(63) inasemekana ndio bondia mzee nchini atacheza siku ya Iddi Mosi.
Kampuni
ya Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya Mkurugenzi wake Ally Ommar
inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa jiji la
Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa Afrika
mashariki yatakayopigwa siku ya iddi mosi na iddi pili.
Ally
omar’Mwazoa’ amemhakikishia Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa nchini
Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika
na mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya
iddi Mosi katika ukumbi wa CCM HALL, Said mundi wa Tanga atazipiga na
Habibu pengo wa Dar es salaam katika kugombania ubingwa wa Taifa wa TPBC
uzito wa super feather raundi kumi.
Ameongeza
kuwa bondia Jumanne Mohamed wa Tanga atazipiga na Ali Bugingo wa Dar es
salaam katika uzito wa light weight raundi kumi katika uzito wa super
fly, Haji juma (Tanga) na Mwaite Juma (Dsm) watacheza raundi nane na
mapambano mengineyo mengi ya utangulizi wa mabondia wa watakaotoka
katika vitongoji mbalimbali vya jiji la Tanga.
Na
siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la
ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na
bondia toka Uganda pambano la raundi kumi, pia Zuberi Kitandula wa Tanga
atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi, Jay jay
Ngotiko wa Tanga atapigana na bondia Juma Afande kutoka Morogoro pia
kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia wakongwe wa
Tanga na wale chipukizi.
Takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi.
Mwazoa
amesema hizi ni mbio za kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika
Mashariki kwanda mkoani Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa
Tanzania na mmoja wa Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!