WAZIRI WA ELIMU DK SHUKURU KAWAMBWA
Mmoja
wa wamiliki wa shule ya mtakatifu Benedict, Renatus Michael amesema
suala la mwalimu aliyehusika na suala la kuwavua nguo wanafunzi darasani
na kuwaacha uchi ni uhalifu wa kawaida usiokuwa na madhara yoyote kwa
mtoto.
Aidha amesema uhalifu mkubwa ni ule wa kuwapiga wanafunzi viboko.
Mmiliki huyo alisema hayo jana Dar es salaam na kuongeza kuwa uongozi wa shule una mpango wa kumchukulia hatua mwalimu aliyehusika na tukio hilo ambaye ni wa jinsi ya kike.
"Mimi nawashangaa sana habari hiyo, hayo ni mambo ya shule na huo ni uhalifu wa mdogo na hauna madhara yoyote kwa mtoto…ndio maana hata polisi waliliweka pembeni kwani limekaa muda wote huo…mmeandika kwa ukali kama vile lilikuwa suala la kupiga viboko?," alihoji mmiliki huyo ambaye alikuwa akilalama kuandikwa kwa taarifa hizo.
Alisema tukio hilo ambalo liliwakumba wanafunzi wanne wa kiume lilitokea Julai na kwamba mara kwa mara amekuwa na mazungumzo na mzazi aliyetoa taarifa hizo polisi na kwamba hawakufikia maafikiano.
"Kiukweli tuliwahi kukaa naye sehemu mbalimbali na mara ya mwisho tulikutana usiku katika hotel moja iliyoko eneo la Buza ambapo mzazi huyo alikuwa akilalamika kwa nini mtoto wake afanyiwe kitendo kama hicho ambacho kingeweza kumuathiri kisaikolojia," alisema Renatus.
Alisema akiwa kama mmiliki alijitahidi sana kumuomba samahani mzazi huyo akimhakikishia kuchukuliwa hatua kwa mwalimu huyo lakini hakutaka yaishe na ndipo alipokwenda kutoa taarifa polisi.
Kuhusu kuchukuliwa kwa hatua kwa mwalimu huyo alisema uongozi wa shule una mpango wa kufanya hivyo ambapo ulikuwa ukisubiri kuanza kwa likizo ya Septemba mwezi ujao.
Kuhusu ni kwa nini maamuzi juu ya mwalimu huyo yachukue muda mrefu kiasi hicho ikilinganishwa na athari iliyowakuta wanafunzi hao, alisema kuna adhabu ya kumpa mwalimu na kuna adhabu ya wanafunzi nzima hivyo ni lazima uchunguzi wa suala hilo ukamilike.
Hata hivyo Renatus alihofia kusambaratika kwa shule hiyo ambayo alidai ni changa ikiwa na wanafunzi wasiofikia 120 kwa idadi yao peke yake akisisitiza kuwa walishaongea na mzazi huyo mara kadhaa kuhusiana na tukio hilo, kwani hata wao halikuwafurahisha.

0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!