Na king Jofa: Kilimanjaro Blog
Gari la kikosi cha zimamoto likiwa eneo la tukio
Moto mkubwa
Umeibuka katika nyumba iliyoko Eneo la Majengo mjini Moshi na
kusababisha Hasara kubwa.Tukio hilo limetokea Leo Mnamo wa Saa nane na
robo Mchana Baada ya Kutokea Hitilafu ya Umeme iliyosababisha Mlipuko
mkubwa wa Moto.
Wakati tukio
hilo linatokea Wapangaji wanaoishi katika nyummba hiyo walikua Kazini
nyumba haikua na Mtu Hapo ndipo jitihada za kudhibiti Moto huo zilipanza
kuchukuliwa na Wananchi kwa kutoa tarifa kwa kikosi cha Zimamoto na
kuja kushirikiana na Wananchi lakini haikuwezekana kuuzima Moto huo mara
Moja.
Majirani wakijaribu kuokoa baadhi ya vitu vilivyosalia
Mwenyekiti wa
Mtaa wa eneo hilo anayefahamika kwa jina moja tu la Mama Sabitina
alisema Kikosi cha zmamoto kilifika kwa muda ila tatizo ni kuwa Moto
ulikua ni mkubwa sana na umeme ulikua bado haujazimwa kwa hiyo bado
kulikua na shoti katika nguzo ya umeme iliyokua karibu na nyumba hiyo.
Nyumba hiyo Mali ya Mzee koshuma yenye jumla ya Wapangaji wanne moto
uliwea kuzimwa baada ya dakika 45 lakini hakuna kitu kilichoweza okolewa
kwani kvitu vyote viliteketea kwa Moto.
Nyumba inavyoonekana baada ya Moto kuzimwa.
Mpaka
tunaondoka eneo hilo hakukua na idadi rasmi ya gharama za Mali
zilizoteketea kwa kuwa wapangaji wengine walikua hawajafika bado eneo la
tukio kwa kuwa walikua bado Makazini.
Source: Kilimanjaro blog (Na Joshua Fanuel)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!