<
Baadhi
ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakiongozwa na
baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group wakiwa katika picha ya
pamoja jioni ya leo na watoto wanaolelewa na kituo cha watoto
Yatima/waishio katika mazingira sambamba na walezi wao kiitwacho Jipe
Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni
ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni
ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa
msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho
chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.
Msanii
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akishiriki kukabidhi sehemu
ya msaada kwa niaba ya wasanii wenzake kwa baadhi ya watoto wanaolelewa
na kituo hicho,kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group
akikabidhi pia sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa walezi
wa kituo hicho,kilichopo Musoma Mjini.
Mratibu
Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo akitoa
mkono wa shukurani kwa ujio wao kwa baadhi ya Wasanii mahiri wa hip
hop hapa Bongo Prof. Jay na Fid Q .
Afisa
Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza
machache kwa niaba ya Kampuni na pia kwa wasanii aliombatana nao,katika
suala zima la kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo
vyakula kwa kituo hicho mapema leo jioni,kulia kwake ni Mratibu
Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo na kushoto
ni Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa
Kuyenga.
Mratibu
wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga
akiwakaribisha vyema baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Clouds Media
Group na Wasanii walioambana nao jioni ya leo,akiwemo Prof Jay,Fid
Q,Chege,Mwasiti,Bibi Cheke,Omy Dimpo,Bob Junior,Roma,Barnaba na
wengineo.
Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya,wakiongozwa na mkongwe wa muziki wa
Bongofleva,Prof Jay wakitia saini kitabu cha wakati,mara walipowasili
kwenye kituo cha Jipe Moyo Center jioni ya leo,wasanii hao watatumbuiza
jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo kesho pia
watakamua kwenye uwanja wa Kambarage,mjini Sinyanga.
Mmoja
wa wasanii anaekuja kwa kasi katika anga ya bongofleva,Ommy Dimpo a.k.a
Pozi kwa Pozi akijitambulisha mbele ya wenyeji,ambapo wageni wote
wakiwamo wasanii walijtambulisha.
Mkongwe kwa umri lakini anakamua vilivyo kwenye anga ya bongofleva,Bibi Cheka nae akijitambulisha mbele ya wenyeji.
Sehemu ya misaada kama inavyoonekana mara baada ya kukabidhiwa kwenye kituo hicho.
Baadhi
ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwasili kwenye kituo cha
kulelea watoto Yatima/waishio katika mazingira magumu kiitwacho Jipe
Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni
ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni
ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa
msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho
chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!