Watu wawili Wahindi waliokimbia nyumbani kwasababu ya hofu ya kisasi kwa unyanyasaji dhidi ya Waislamu katika mji la Assam walikufa na wengine tisa kujeruhiwa baada ya kusukumwa kutoka katika treni lilokuwa katika mwendo kasi Jumapili hii iliyokuwa sikukuu ya iddi, alisema afisa wa Reli.
Tukio hilo lilitokea karibu na kituo cha reli Jalpaiguri katika sehemu ya kaskazini ya jimbo la West Bengal, karibu na Assam, alisema afisa huyo."Watu 2 walikufa, wanne walijeruhiwa vibaya na wengine watano walipata majeraha madogo," Wahindi wengi kaskazini wamekimbia miji kama vile Bangalore na Mumbai baada ya uvumi na ujumbe wa maandishi na kwenye mitandao iliyoonya na kutoa taarifa ya kuwapo mashambulizi, mvutano kukiwa ni mapambano kati ya Waislamu na wazawa kabila la Bodo juu ya masuala ya kiimani.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!