StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 1, 2012

FIESTA ILIVYONOGA MUSOMA, JIONEE MWENYEWE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 

Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.

kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.Tamasha hilo litafanyika leo jioni mjini Shinyanga ndani ya uwanja wa Kambarage.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat