Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Julius Malema akizungumza na wafuasi wake wanaomuunga mkono
JULIAS
Malema amewaambia wafuasi wake kuwa hatishiki na uamuzi wa Mahakama
kusema kuwa ana kesi ya kujibu. Mahakama nchini Afrika ya Kusini
ilimwachilia kwa dhamana Malema anayekabiliwa na shtaka la kuhaulisha
pesa.
Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa Malema ambaye
aliwahutubia wafuasi wake nje ya Mahakama, pia anatuhumiwa kwa kutumia
nafasi yake ya zamani kama kiongozi wa tawi la vijana la ANC
kujitajirisha yeye na washirika wake wa biashara.
Washirika wake
wengine wanne nao walikabiliwa na mashtaka sawa na hiyo katika kesi yao
iliyosikilizwa hapo jana. Katika hotuba yake kwa mamia ya wafuasi wake
nje ya mahakama mjini Polokwane, bwana Malema alisema ataendelea na
juhudi zake za kutetea maelefu wanaoishi katika umaskini nchini humo.
Seng’enge
zilizungushwa katika eneo la mahakama hiyo iliyopo Polokwane, mji
mkubwa wa jimbo analotokea mwanasiasa huyo, Limpopo. Wafuasi wake
wanasema mashtaka hayo yameshinikizwa kisiasa.
Wakiimba na
kucheza nje ya mahakama hiyo wafuasi wengi wa chama hicho cha ANC tawi
la vijana walishikilia mabango yaliosema ‘Muacheni kiongozi wetu’.
Maofisa wa usalaman walidhibiti ulinzi na kulikuwa na utulivu mkubwa.
Julius
Malema na washirika wake wa kibiashara wanashutumiwa kwa kufaidi
kutokanana na mikataba ya serikali katika jimbo la Limpopo, tuhuma
ambazo anazikana. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 31 pia
anachunguzwa katika kesi tofauti ya ukwepaji kulipa ushuru.
Malema
ni maarufu sana Afrika Kusini kwa ukakamavu wake wa kutetea maslahi ya
wananchi na maisha yake ya kifahari, huku akijitambulisha kama
mpiganiaji uhuru wa uchumi. Alitimuliwa kwenye chama hicho tawala mnamo
mwezi Aprili akishutumiwa kwa kuzusha migawanyiko katika chama hicho.
Ni
mkosoaji mkali wa a Jacob Zuma, hivi karibuni akimshutumu rais huyo kwa
alivyoushughulikia mgomo wa wachimba migodi wa Marikana. Kwa mujibu wa
mwandishi wa masuala ya Afrika, Andrew Harding, baadhi ya watu Afrika
kusini wanaamini anafikishwa haraka mahakamani, ikiwa ni chini ya wiki
moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake, ili kuimarisha nafasi
ya kisiasa ya Zuma.
Mwandishi wetu anaeleza kwamba huenda ikawa
ni kesi ya muda mrefu, ambayo huenda ikatoa nafasi ya kujulikana ukweli
kuhusu suala hilo la rushwa, ambalo watu wengi wanaamini inaitia nchi
hiyo doa.
-BBC
September 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!