StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 20, 2012

KIKOSI CHA USALAMA WAKIENDELEA NA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO KATIKA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Koplo Isack na Afande Tunu wakizikagua pikipiki zilizokuwa zikipita katika eneo la Ipogolo mjini Iringa katika barabara ya Dar es salaam Tunduma wakati wa ukaguzi wamagari leo


(Staff Sergeant) Yohana Mjema na Afande Tunu wa kikosi cha Trafiki wakikagua moja ya magari yaliyokaguliwa na kupatiwa Stika maalum za ukaguzi leo mjini Iringa, wakati wa zoezi la ukaguzi katika kuadhimisha wiki ya Nenda wa usalama Barabarani, ukaguzi huo umefanyika katika eneo la Ipogolo katika barabara kuu ya Dar es salaam- Tunduma
Kikosi cha Trafiki kinaendesha zoezi la ukaguzi wa magari yote na kuyapa stika maalum zinazonyesha kuwa yamekaguliwa katika kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Ukaguzi huo umefanyika katika eneo la Ipogolo mjini Iringa kwenye barabara kuu ya Dar es salaam -Tunduma ambako maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa

(Vehicle Inspector)Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika jeshi la polisi Trafiki mkoani Iringa akimhoji mmoja wa madereva wa magari makubwa wakati alipokuwa akikagua gari hilo lililokuwa likitokea nchini Congo DRC ambako lilipeleka mafuta, kulia ni Afande Tunu akishiriki katika zoezi la ukaguzi wa magari,

Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika jeshi la polisi Trafiki akumuandikia Stika mmoja wa madereva wa Daladala mkoani Iringa mara baada ya kukagua gari hilo.

Stafu Sajenti Yohana Mjema akilikagua Roli lenye namba T 456 ADQ lililokuwa limebeba matofali katika zoezi la ukaguzi wa magari kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama Barabarani, kulia ni Afande Tunu akishiriki katika zoezi hilo.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat