StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 8, 2012

VIGOGO WA CHAMA CHA MPIRA MKOANI ARUSHA WADAKWA NA TAKUKURU KWA UTAPELI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Arusha (ARFA), Khalifa Mgonja.


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Arusha (TAKUKURU), imemtia mbaroni na kumfikisha mahakamani mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Arusha (ARFA), Khalifa Mgonja, (70) na Katibu wake, Adam Brown (58) kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia mamilioni ya fedha kinyume cha sheria.
Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha, Hawa Mguruta ,waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Hamidu Simbano na Rehema Mteta, walidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja tarehe tofauti mwaka 2009/10 walitumia madaraka yao vibaya na kujipatia mamilioni ya fedha.
Mteta alisema shitaka la kwanza ni la Mgonja ambapo Desemba 11 /2009 akiwa Mwenyekiti wa ARFA, alighushi barua kuomba Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) shilingi milioni 121,kwa ajili ya kusaidia kuinua timu ya mkoa, kinyume cha sheria.
Shitaka la pili inadaiwa Novemba11 / 2010 Mgonja, akiwa Mwenyekiti alitumia vibaya madaraka yake na kujipatia Sh.milioni 38 na shitaka la tatu kati ya Agosti 28/2010 alitumia madaraka yake vibaya na kujipatia Sh. milioni 6 na shtaka la nne linamhusu Mgonja na Brown kwa pamoja Desemba 2009 na Agosti 26 mwaka 2010, walijipatia Sh. milioni 33 na kuzitumia vibaya.
Baada ya kuwasomea mashtaka hayo, Mteta alisema upande wa serikali hauna pingamizi na dhamana yao na kuongeza kuwa upepelezi dhidi ya kesi hiyo bado haukajamilika.
Pia aliomba Mahakama kuwapatia kibali cha kumkamata mshitakiwa wa tatu, Brown Francis, ambaye hapatikani baada ya kuhojiwa na TAKUKURU na kudhaminiwa.
“Mheshimiwa tunaomba Mahakama itupatie kibari cha kumkamata mshitakiwa huyu, sababu ametoweka na hatujui aliko,”alisema Mteta.
Ombi hilo lilipingwa na Wakili wa washitakiwa hao, Alute Mughway na kusema Mahakama haipaswi kutoa kibali chochote mpaka TAKUKURU ifuate utaratibu wa kimahakama wa kuandika barua ya kuomba kuwakamata, sababu mshitakiwa huyo amekiuka sheria yao na siyo Mahakamani.
Baada ya ombi hilo , Hakimu Hawa Mguruta, aliingilia kati na kumshukuru Wakili huyo kwa kufafanua sheria na kuitaka TAKUKURU kufuata utaratibu wa kumpata mshitakiwa huyo.
Hata hivyo washtakiwa wapo nje kwa dhamana, baada ya wadhamini wao kujitokeza na kusaini bondi za Sh. milioni 75, ambapo mshitakiwa wa kwanza ambaye Mwenyekiti Mgonja, alitakiwa kudhaminiwa na watu wawili ambapo mmoja alisaini bondi ya sh.milioni 60 na mwingine mtumishi serikalini.
Mshitakiwa wa pili Katibu Brown, alidhaminiwa na wadhamini wawli, kwa bondi ya shilingi milioni 15.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 2 mwaka huu, itakapotajwa tena na washitakiwa wanatakiwa kufika mahakaani bila kukosa.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat