Ni aina ya SMG akiwa na risasi kibao
Mahabusu wawili wanaodai kuwa na kesi ya mauaji wametoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi katika Mahakama Kuu jijini Arusha baada ya kumkaba askari aliyekuwa anawalinda kisha wakampokonya bunduki aina ya SMG na kukimbia nayo.
Habari zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabas, baada ya mahabusu hao kufanikiwa kumpora askari huyo silaha, waliruka uzio na kuingia katika mto ulioko karibu na mahakama hiyo na kutokomea kusikojulikana.
Mashududa hao walisema kuwa baada ya tukio hilo, polisi walianza kuwasaka mahabusu hao na kufanikiwa kuipata silaha ikiwa imetelekezwa juu ya jiwe kwenye mto huo ikiwa na risasi zote.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao mahabusu hao walikuwa wanatoka kwenye chumba cha mahabusu kwenda kupanda karandinga kwa ajili ya kurudishwa mahabusu katika gereza la Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Taarifa za awali zilizopatikana ambazo hata hivyo, hazijathibitishwa zimedai kuwa mahabusu hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ambayo yalifanyika wilayani Arumeru.
Tukio hilo lilizua hofu kubwa mahakamani hapo baada ya kuwalazimu baadhi ya watumishi wa mahakama hiyo kujifungia ndani ya vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu huyo kuwafyatulia risasi.
Kamanda Sabas aliahidi kulitolea ufafanuzi tukio hilo leo na kuongeza kuwa polisi inafanya uchunguzi sambamba na msako mkali wa mahabusu hao.
Mashuhuda wengine waliozungumza na NIPASHE walisema kuwa tukio hilo lililotokea saa 7:30 mchana
lilifanyika kwa kasi kubwa baada mahabusu huyo kumvamia askari polisi kisha kumkata mtama na kumnyanganya bunduki hiyo.
“Yule bwana baada tu ya kumnyanganya akawa ameikoki ile bunduki huku askari akiwa chini amelala, wakati huo askari wenzake hawakuwa na silaha hivyo ilikuwa vigumu kumsaidia.”
“Hata hivyo mahabusu huyo alipoona upenyo wa kukimbia alichomoka mbio na bunduki hiyo mkononi akielekea mto uliopo jirani kabisa na mahakama hiyo,” alisema shuhuda mmoja Abdalah Jumanne aliyeshuhudia tukio hilo.
Habari ambazo zimetanda jijini hapa lakini hazikuweza kuthibitishwa na upande wa polisi zilizodai kuwa mahabusu huyo alikuwa ni moja ya watu waliohusika na mauaji ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Usa River aliyeuawa kikatili muda mfupi baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!