Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Na: Mussa Juma, Arusha,Mwananchi.
Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwahutubia wafuasi wake baada ya
Jaji MKuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman kuahirisha kesi ya rufaa ya
aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.Picha Zote na Jackson
Odoyo Mussa Juma, Arusha MAWAKILI wanaomtetea aliyekuwa Mbunge wa
Arusha, Godbless Lema wamedai mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa
mteja wao yuko huru kwa kuwa mahakama haikutengua ubunge wake.Katika
kesi hiyo, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande anawaongoza wenzake wa
Mahakama ya Rufani, Salum Massati na Natalia Kimaro kusikiliza maombi ya
rufani hiyo, inayopinga Lema kuvuliwa ubunge.
Mawakili
hao wa Lema jana walitoa hoja ya kupinga hukumu hiyo kufuatia mabishano
baina yao na upande wa utetezi kwa maelezo kuwa taratibu za ufunguaji
wa rufaa hiyo zimekosewa. Awali wakili Alute Mughwai aliiomba mahakama
hiyo kutupilia mbali rufani hiyo kwa kile alichoeleza kuwa ina upungufu
mwingi wa kisheria na kikanuni. Wakili huyo alitaja baadhi ya kasoro za
rufani hiyo kuwa ni hati ya kukaza hukumu (tuzo) ambayo imewasilishwa
mahakamani hapo kutokuwa na mhuri wa Jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa
hukumu ya kesi hiyo.
Alidai kuwa katika rufani hiyo
pia kuna upungufu kuhusu tarehe za kuwasilishwa kwa rufani, pia baadhi
ya vifungu vimekosewa.Wakili Mughwai alitoa kumbukumbu ya kesi kadhaa
ambazo mahakama ya rufani ilizitupa baada ya kukosa hadhi ya kisheria
kusikilizwa.
“Mawakili wa Lema walipaswa kabla ya
kuwasilisha mahakamani rufani yao, kujiridhisha kama kuna upungufu
katika nyaraka ambazo wanawasilisha mahakamani.” Alisema kubwa katika
makosa ambayo amebaini katika rufani hiyo ni kuwasilishwa bila kuwekwa
mhuri hati ya kukaza hukumu (tuzo) iliyotolewa na Jaji aliyetoa hukumu
katika kesi ya awali. “Hapa nani ambaye anajua sahihi ya Jaji? Alihoji.
Hawa mawakili walipaswa kushinikiza kuwekwa mhuri wa mahakama katika
hukumu hiyo ili kuthibitisha uhalali wake,” alisema Alute. Hata hiyo,
wakili huyo alisema badala yake, mawakili hao waliwasilisha mahakamani
rufani hiyo ndani ya siku 29 tu baada ya hukumu, badala ya siku 60
ambazo walipewa.
“Kwa kuwasilisha mahakama ya rufani,
hukumu ambayo bado haina mhuri wa Jaji ni ukiukwaji wa kanuni na
taratibu za mahakama.” Mughwai alidai kuwa katika mazingira ya sasa
hakuna cha kurekebishwa katika rufani hiyo, badala yake itupwe na
kuwataka wakata rufani kulipa gharama zote za kesi. Hata hivyo, hoja
hizo zilipingwa na mawakili wa Lema ambao ni Tundu Lissu na Method
Kimomogoro, ambao walidai kuwa hawakuwa na mamlaka ya kumlazimisha Jaji
Rwakibarila kuweka mhuri.
Lissu alidai "Kama
inaonekana sasa kuwa ni batili, basi hata uamuzi wa kumvua ubunge Lema
ni batili," alisema. Wakili Kimomogoro Kwa upande wake, Wakili
Kimomogoro alisema kisheria kasoro hizo ya mhuri wa mahakama na tarehe,
haziwezi kusababisha rufani hiyo kutupwa kwani haziathiri madai ya
msingi katika rufani.
Alidai kesi hiyo ya Lema ilikuwa
ya kipekee kwani mara tu baada ya hukumu kutolewa faili lilipelekwa
jijini Dar es Salaam na maombi ya nyaraka kadhaa za kesi hiyo yalitumwa
kutoka Dar es Salaam. “Katika mazingira kama haya hatuwezi kuepuka
makosa ya kibinadamu ambayo yanatambulika kisheria,” alidai Kimomogoro.
Aliongeza kuwa katika hoja hiyo, waliandika kifugu namba 114 badala ya
113 kimakosa ya kiuchapaji, lakini hakipotoshi kitu chochote kwani
kifungu hicho hakipo. Wakili Kimomogoro alisema wakili mwenzake, Mughwai
ameshindwa kuzungumzia uamuzi ya kesi ambazo, hazikufutwa kutokana na
kuwa na upungufu mdogo wa aina hiyo ambao kimsingi hauathiri rufani.
Hata
hivyo, alisema kama wakili huyo alibaini makosa hayo, katika
uwasilishaji wa hoja zake, alipaswa pia kurekebisha kwa mujibu wa sheria
ya mwaka 2009 ya mahakama. Kimomogoro pia aliwasilisha mahakamani hoja
kadhaa za kisheria na uamuzi ya Mahakama ya Rufani za ndani na nje ya
nchi, ambazo hazikutupilia mbali rufani ambazo zilikuwa na upungufu
mdogo, kwani lengo la mahakama hizo ni kutafuta haki.
“Siyo
kila kasoro au usumbufu kwenye hukumu unaweza kusababisha kutupwa
rufani kwani kasoro zote zilizotajwa ni za makosa na uchapaji na
nyingine ni za kiutaratibu tu,” alisema. Alifafanua kuwa makosa ambayo
yanaweza kusababisha rufani kutupwa ni kama aina namba ya kesi, majina
na wadhifa wa wadau katika shauri husika, mambo yanayolalamikiwa na
mahakama imeamua nini.
Wakili huyo alifafanua kuwa
jambo la kukosekana mhuri wa mahakama wa Jaji siyo kubwa na kusababisha
kutupwa rufani kwani hakuna ambaye anapinga hukumu iliyowasilishwa
mahakamani. Kwa upande wake, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Vitalis
Timoth alisema anaunga mkono hoja za mawakili wa Lema, kuwa pingamizi ya
wakili Mughwai haina msingi wa kisheria.
Alisema hati
ya kukaza hukumu (Tuzo) inatolewa chini ya sheria ya mwenendo wa makosa
ya jinai na siyo chini ya sheria ya masijala za mahakama. Alisema siyo
kazi ya jaji aliyetoa hukumu, kuweka mhuri hukumu yake bali hiyo ni kazi
ya msajili wa mahakama na masijala za mahakama.
“Kama
hati ya kukaza hukumu ina matatizo anayepaswa kulaumiwa siyo mawakili
bali ni mahakama ambayo ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuweka mhuri,”
alisema. Alidai kuwa pingamizi ya awali ya rufani inapaswa kuwa na sifa
mbili, kwanza iwe na suala la kisheria na pili iendane na kesi ya
msingi. “Katika hoja za wakili Mughwai ni wazi inathibitika pingamizi
hili halina matakwa ya kisheria kwani hata kama ikipitwa siyo kuwa
itazuia kurejeshwa tena na kusikilizwa kwa rufani ya msingi.” Alidai ni
busara kuacha kuwa na pingamizi ambazo zinaongeza gharama za kesi na
muda wa kusikiliza.
“Ushauri wangu kila shauri
liamuliwe kwa mazingira yake na uamuzi wa sasa uzingatie mahakama katika
kutenda haki,” aliongeza. Alidai kwamba kutupwa kwa hoja ya kutaka
waomba rufani wachapwe mijeledi kwani kazi ya mahakama siyo kuchapa watu
bali ni kutoa haki. “Tunashauri kusikilizwa rufani kwa kuzingatia
sheria na ushahidi,” alisema. Jopo la Majaji Baada ya kutolewa kwa hoja
za pande zote za mawakili, Jaji Chande na Jaji Massati waliwauliza
maswali kadhaa mawakili hao na kujieleza na baadaye Jaji Chande
alitangaza kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi hapo itakapotangazwa. Jaji
Chande alisema vikao vya Mahakama ya Rufani Kanda ya Arusha vimemalizika
jana, hivyo uamuzi wa kutupwa kwa pingamizi la rufani hiyo au la
utatolewa siku itakayopangwa na mahakama.
Baada ya
uamuzi huo umati wa wafuasi wa Chadema, uliokuwa ndani na nje ya
mahakama ulianza kuimba nyimbo mbalimbali kama vile Lema Jembe na bila
Lema patachimbika. Katika hatua ya kuepuka vurugu, Lema alizungumza na
wafuasi hao nje ya mahakama na kuwataka kuondoka kwa amani kwenda katika
ofisi ya Chadema iliyopo Ngarenaro kwa amani bila vurugu.
Warufaniwa
katika kesi hiyo ni makada wa CCM, Happy Kivuyo, Mussa Mkanga na Agnes
Mollel ambao walishinda kesi ambayo hukumu yake ilimvua ubunge Lema
Aprili 4, mwaka huu.
October 3, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!