StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 13, 2012

HUYU NDIYE MKURUGENZI MKUU WA BBC ALIYEJIUZULU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa BBC, George Entwistle

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Habari, BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo. George Entwistle amejiuzulu kama Mkurugenzi BBC kwa kile kufanyika makosa katika moja ya vipindi vya shirika hilo la habari Ulimwenguni. Taarifa zaidi zinasema Entwistle amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.

Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative, Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto. Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.

Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchunguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile. Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi, usiku Entwistle alisema; “ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya”.

Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema; “huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma”. “Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika”

“Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amediriki kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika – uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi”.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat