Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Kundi la ng’ombe
INAKADIRIWA kuwa askari polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika shambulizi lililofanywa dhidi yao walipokuwa wanajaribu kuokoa mifugo waliokuwa wameibwa.
Taarifa zaidi zinasema maofisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, Kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi. Msemaji wa polisi amesema kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliaji watatu, lakini viongozi wa kijiji wanatofautiana kwa kusema kuwa huenda maiti zaidi wa tukio hilo wakapatikana.
Hata hivyo jana miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi waliouawa kuwa 40. Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho ya mifugo wao Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.
Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake. Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili, inaarifiwa kuwa wakaguzi wawili wakuu wa polisi hawajulikani waliko.
Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini. Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki mbili zilizopita hadi 43.
Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa mishahara.
November 13, 2012
Askari Polisi 40 Wauawa na Wezi wa Mifugo Kenya
Millionfortune.com
JAMII
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!