Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Waziri wa fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na maongezi ya uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard. (Standard Bank) hapa jijini Tokyo- Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha na maendeleo ya uchumi, Mhe. Xavier – Luc Duval walipokuwa wakibadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya nchi zao hizo mbili Jijini – Japan – Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na wajumbe kutoka nchi Mauritius kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Maendeleo ya uchumi, Bw. Ali Mansoor akifuatiwa na Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha na Maendeleo ya uchumi , Mhe. Xavier – Luc Duval walipokuwa wakielezana juu ya maendeleo kati ya nchi hizi mbili Jijini – Japan – Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa na Mwenyekiti wa Bodi ya uwekezaji Bw. Maurice Lam wa Mauritius wakibadilishana hati za mawasiliano Jijini Tokyo-Japan.
Wakatikati ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha Mhe. Xavier – Luc Duval akiwa na ujumbe wake walipokuwa na Mazungumzo na wa Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa hayupo kwenye picha hapa jijini Tokyo- Japan.
Gavana wa Benki Kuu Tanzania,Prof. Benno Ndullu akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Servacius Likwilile wakifuatilia kikao cha Mawaziri wa Afrika Mashariki kilichoitishwa na katibu Mkuu wa Afrika Mashariki Jijini Japan – Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Waziri wa Fedha wa Rwanda.
Gavana wa Benki ya Tanzania akiwa na Gavana wa Benki kuu ya Rwanda wakisikiliza kwa makini mkutano na wajumbe wa Afrika Mashariki hapa Jijini Tokyo – Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akimpokea Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Robinson Githae tayari kwa kikao chao kinachohusu mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni waziri wa Fedha wa Rwanda.(Picha na Ingiahedi Mduma na Scola Malinga Jijini Tokyo – Japan).
October 16, 2012
MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI WA FEDHA KATIKA MIKUTANO YA IMF NA WB JAPAN.
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!