MADAKTARI nchini wameanza mgomo katika baadhi ya hospitali nchini
baada ya Serikali kushindwa kutekeleza madai yao waliyowasilisha katika
Kamati ya Majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Mgomo
huo umetangazwa na Jumuiya ya Madaktari nchini huku ikifafanua kwamba
kati ya madai kumi waliyotaka yatekelezwe na Serikali, hakuna hata moja
lililofanyiwa kazi. Hata hivyo, jana madaktari hao ambao walikaa vikao
vya majadiliano na Serikali kwa siku 90 baada ya kusitisha mgomo wao wa
pili, wamesema katika madai yao kumi, hakuna hata moja lililotekelezwa
na Serikali. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka jana
aliwaeleza waandishi wa habari kwamba ili warejee kazini, Serikali
inatakiwa kutekeleza madai yao yote na kusisitiza kwamba dai lao la
kwanza ni kuitaka Serikali kuboresha huduma za msingi kwa wagonjwa.
“Mgomo
umeanza jana na hauna kikomo, lengo ni kuishinikiza Serikali kutekeleza
madai yetu, hata zile huduma za dharura nazo kuanzia kesho (leo)
zinaweza kusitishwa,” alisema Dk Ulimboka. Wakati Ulimboka akieleza
hayo, huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya
Mifupa (Moi) ilikuwa ikitolewa kwa kusuasua huku baadhi ya wafanyakazi
wakisisitiza kuwa mgomo huo upo.
Licha ya wafanyakazi hao kukiri
kuwa siku za mwisho wa wiki idadi ya wagonjwa katika hospitali hizo
huwa ndogo, lakini walisisitiza kuwapo kwa mgomo huo na kufafanua kuwa
kwa mtu mgeni katika eneo hilo si rahisi kutambua hali hiyo. Mwananchi
Jumapili lilifika katika hospitali hiyo na kukuta huduma zikitolewa
‘kiaina’ huku baadhi ya wagonjwa wakieleza kwamba zimezorota, sio kama
siku zilizopita.
Tamko la Jumuiya Akieleza kwa kina sababu
za mgomo huo, Dk Ulimboka alisema katika madai waliyoyawasilisha, hakuna
hata moja lililotekelezwa na kufafanua kwamba Serikali imeongeza dai
ambalo wao hawakuliwasilisha. Madai hayo ni pamoja na kupandishwa kwa
ongezeko la mishahara, posho ya kuitwa kazini, posho za kufanya kazi
katika mazingira magumu, bima ya afya, nyumba za kuishi, kukopeshwa
magari kwa ajili ya usafiri, kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi
kwa kupeleka vifaa vya kazi, dawa na kuboresha miundombinu.
“Serikali
imesema imerekebisha viwango vinavyotumika kulipa posho ya uchunguzi wa
maiti kwa Sh 100,000 kwa uchunguzi wa madaktari na Sh50,000 kwa
watumishi wengine, lakini hili halikuwa dai letu!” alisema Dk
Ulimboka. Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi
aliwatahadharisha madaktari hao kuacha mgomo, akieleza kuwa ni batili na
ni kinyume cha viapo vyao vya kazi. Dk Mwinyi aliainisha mambo 10
ambayo madaktari walikuwa wamepanga kutekelezewa na kusema kuwa kwa
sehemu, yametekelezwa na baadhi ya mambo yaliyobakia wanaweza
kuyazungumza.
Mwanza
Madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hosptali ya Rufaa ya Bugando jana walianza mgomo rasmi baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali yaliyosababisha madaktari hao kugoma mapema mwaka huu. Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mwakilishi wa Kamati ndogo ya kufuatilia madai madaktari hao, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.
“Kwa kuwa leo sio siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu (kesho) ndo utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi, lakini hakutakuwa na huduma,”alisema
Moshi
Hali ya utendaji wa madaktari mkoani Kilimanjaro imeonekana ya kusuasua huku baadhi ya madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wakisema hawaingii kazini na wengine wakisema bado wanasikilizia.
Katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi, madaktari waliokuwa zamu walisema kwa leo huwezi kujua aliyeko kwenye mgomo na ambaye hayupo, kwani wengi hawako kazini leo hadi kesho. B
aadhi ya wagonjwa waliolazwa
Hospitali ya KCMC katika wodi ya wanawake, walisema kuwa walitangaziwa
kuwa kutakuwa na mgomo wa madaktari na kila mmoja aangalie cha kufanya
na kuwa walifika wodini hapo asubuhi na hawakuzungumza na mgonjwa na
kutoka. Wagonjwa hao wamesema Ijumaa jioni wagonjwa wengi waliruhusiwa
kuondoka hata kama hali zao hazijatengemaa ambapo walisema wanahofia
afya zao kama madaktari watatekeleza msimamo wao. Mbeya Katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya madaktari 10 kati ya 80 ndiyo waliokubali
jana kuendelea na huduma ya kutibu wagonjwa ambapo wengine wameanza
mgomo rasmi.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu,
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Eliuter Samky amethibitisha
kuwapo na hali ya mgomo na kwamba ana uhakika wa madaktari 10 waliopo
zamu kuendelea kazi.
Awali Mwandishi wa gazeti hili
alipofika katika hospitali hiyo hakukuta daktari yeyote na ofisi za
utawala zikiwa zimefungwa huku katika eneo la mapokezi likiwa na
wagonjwa ambao wamekaa wakisubiria kupata huduma. Katika kitengo cha
wazazi Meta wanawake wanaokwenda kupata huduma wamesema wameingiwa na
hofu kubwa kwa kukosa huduma hiyo baada ya kuona matangazo yanayosema
hakuna mgojwa atakayepatiwa matibabu.
Wakizungumza hospitalini
hapo wanawake hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao, walisema kuwa
mbali na kuona tangazo hilo lakini pia waliambiwa na baadhi ya madaktari
kuwa ni bora wakaenda sehemu nyingine kwa ajili ya matibabu kwa kile
kilichoelezwa kuwa kuwa na wao wapo katika mgomo huo hivyo hakuta kuwa
na huduma yeyote kwa mgonjwa.
Arusha
Hali ya mgomo wa madaktari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, haikuonekana jana asubuhi ingawa katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya madaktari na manesi hawakufika wodimi kuwaona wagonjwa kama wananvyofanya siku nyingine.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dk Mlay alipoulizwa
na gazeti hili alisema hali hiyo isihusishwe na mgomo uliotangazwa na
chama cha madaktari kwa kuwa kimetona na sababu kwamba leo na kesho ni
siku za mapumziko .
Baadhi ya wagonjwa na ndugu wanaowauguza walihojiwa na gazeti hili walionyeshwa kushangazwa na hali ya madaktari na manesi kushindwa kuwatembelea leo katika wodi zao kinyume na siku zote.
Mganga Mkuu wa hospitali alisema kwamba hospitalini kwake hakuna mgomo wowote wa madaktari kwa kuwa wanafanya kazi kama kawaida na wala hawatambui suala la mgomo wa madaktari uliotangazwa na Chama cha Madaktari nchini(MAT).
Baadhi ya wagonjwa na ndugu wanaowauguza walihojiwa na gazeti hili walionyeshwa kushangazwa na hali ya madaktari na manesi kushindwa kuwatembelea leo katika wodi zao kinyume na siku zote.
Mganga Mkuu wa hospitali alisema kwamba hospitalini kwake hakuna mgomo wowote wa madaktari kwa kuwa wanafanya kazi kama kawaida na wala hawatambui suala la mgomo wa madaktari uliotangazwa na Chama cha Madaktari nchini(MAT).
Tanga Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo
pamoja hospitali nyingine za wilayani jana ziliendelea na huduma ya
kutoa matibabu kwa wagonjwa kama kawaida. Katika Hospitali ya Bombo
ambayo ni ya Mkoa wa Tanga, Mwandishi wa habari hizi jana alikuta
madaktari pamoja na wauguzi waliokuwa zamu wakiendelea na kutoa matibabu
kwa wagonjwa waliolazwa pamoja na wale wa kutoka nje.
Wakizungumza
na Mwananchi Jumapili madaktari wa Hospitali ya Bombo walisema
wameshindwa kufanya mgomo kwa kuwa hawana taarifa za kuwataka kufanya
hivyo bali wamekuwa wakisikia na kusoma kupitia vyombo vya habari.
Haruna
Juma ambaye ni mkazi wa Barabara ya 10 Jijini Tanga, aliwashukuru
madaktari wa Hospitali ya Bombo kwa kutogoma kwa kuwa mdogo wake
anayesumbuliwa na Apendex alipangiwa kufanyiwa upasuaji jana ambapo
waganga walimfanyia kama kawaida.
Waziri
Serikali imesema kuwa itaendelea na msimamo wake ilioutoa bungeni mjini Dodoma wa kuwataka madaktari nchini kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wakati ambapo madai yao ya msingi yakiwa yanashughulikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro jana baada ya kufanya ziara yake katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alisema kuwa kimsingi yako mambo ambayo katika mazungumzo na madaktari hao walikubaliana lakini pia yako mambo ambayo hawakukubalina.
Serikali imesema kuwa itaendelea na msimamo wake ilioutoa bungeni mjini Dodoma wa kuwataka madaktari nchini kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wakati ambapo madai yao ya msingi yakiwa yanashughulikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro jana baada ya kufanya ziara yake katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alisema kuwa kimsingi yako mambo ambayo katika mazungumzo na madaktari hao walikubaliana lakini pia yako mambo ambayo hawakukubalina.
Dk Rashid alisema kuwa mambo ambayo walikubalina
na madaktari hao yanaendelea kushughulikiwa lakini mambo ambayo
walishindwa kukubalina katika baraza la usuluhishi madaktari hao
walikimbilia mahakamani ili kutafuta suluhu.
“Na sisi tunasubiri
maamuzi ya mahakama kwa hivyo kitendo cha wao kugoma kinakwenda kinyume
na sheria kwa kuwa jambo hilo bado halijapatiwa ufumbuzi na mahakama,”
alisisitiza.
Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro hakukuwa na
dalili zozote za madaktari na wauguzi kugoma, huduma za matibabu kwa
wagonjwa zilikuwa zikiendelea kama kawaida huku baadhi ya wauguzi na
madaktari wa hospitali hiyo wakidai kutokuwa tayari kuingia katika mgomo
huo.
Amana, Temeke Katika hospitali ya Amana na Temeke za jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa huduma kama kawaida, isipokuwa Hospitali ya Mwananyamala ambayo kulikuwa na madaktari na waguzi wachache. Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Meshack Shemwela aliiambia Mwananchi Jumapili jana kwamba huduma ya afya zinaendelea kutolewa kama kawaida na kwamba wanafanya tathmini ilikutambua kama kuna madaktari waliogoma.
Amana, Temeke Katika hospitali ya Amana na Temeke za jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa huduma kama kawaida, isipokuwa Hospitali ya Mwananyamala ambayo kulikuwa na madaktari na waguzi wachache. Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Meshack Shemwela aliiambia Mwananchi Jumapili jana kwamba huduma ya afya zinaendelea kutolewa kama kawaida na kwamba wanafanya tathmini ilikutambua kama kuna madaktari waliogoma.
Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Said Meck Sadick alisema kuanzia jana saa 6 usiku walifanya uchunguzi na
kubaini kwamba kuna watu waliokuwa wanapita katika kila hosptali
kuhamasisha kufanyika lakini madaktari hawajagoma.
Imeandaliwa
na Rehema Matowo,Moshi, Venance George, Morogoro, Burhani Yakub,Tanga,
Brandy Nelson, Godfrey Kahango,Mbeya, Moses Mashalla,Arusha,Sheilla
Sezzy,Mwanza Aidan Mhando, Ibrahim Yamola, Geofrey Nyang'oro na Fidelis
Butahe,Fidelis Butahe na Geofrey Nyang’oro