Mtu mmoja ameuwaa na wengine kujeruhiwa na mabomu mjini Mombasa siku moja baada ya onyo kutolewa na ofisi za ubalozi wa Marekani.
Polisi mjini Mombasa imesema " mashambulizi hayo yalitokea saa nne usiku
kwa muda wa masaa ya Kenya wakati wakazi wa mji huo wanaangalia
mshindano ya kombe la Ulaya kwenye bar moja iliyopo Mombasa mjini."
Onyo la mashambulizi katika mji wa Mombasa, lilitiliwa maanani na
kuzifanya serikali za nchi za Magharibi kuwaonya wananchi wao kuwa
waangalifu watakapo kuwa katika matembezi ya kitalii katika mji wa
Mombasa.