Jaji mmoja nchini pakistan
ametoa kibali cha kukamatwa kwa Makhdoom Shahabuddin, ambaye ametajwa na
serikali ya nchi hiyo kama mgombea anayeungwa mkono na wengi kuwa
waziri mkuu mpya.
Kibali hicho kimehusiana na uagizaji wa dawa za hospitalini wakati Shahabudin akiwa waziri wa afya.Bwana Shahabuddin ni mmoja wa maafisa wakuu wa chama cha Pakistan People's Party ambacho kinaongoza serikali ya sasa ya mseto.
Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kumuidhinisha rasmi hapo kesho kuwa waziri mkuu.
Uamuzi huo wa mahakama ni tukio la hivi karibuni, linalothibitisha uhasama kati ya idara ya mahama na serikali ya nchi hiyo.