Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7%
akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo
la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.
Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan,
amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa
matokeo ya uchaguzi hayatobalika.
Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na
vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi
wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.
Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio
kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa
zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai
zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa
majeshi.
Wafuasi wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi
yao katika eneo la kaskazini mwa mji ambako kuna makao makuu ya Tume ya
uchaguzi huko Nasser City.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi Jaji
Sultan alianza kwa kunena kua tangazo la matokeo ya uchaguzi yalikua
yamezongwa na shinikizo pamoja na hali ya wasiwasi.
Tume ya uchaguzi ilizingatia sheria
ilipochunguza visanduku vya kupigia kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna
kilicho juu ya sheria.
Jaji huyo akaongezea kukanusha madai
mawili nyeti kuhusu njama za kuibia uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi
za kupigia kura ziliwekwa ndani ya visanduku tayari zikiwa na majina ya
mgombea wanayemtaka ashinde.
Hatimaye Jaji Sultan akamtangaza mshindi
kua ni Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Muslim Brotherhood
cha Freedom and Justice, Bw.Mursi.
Baada ya dakika kadhaa akitangaza
marekebisho kuhusu matokeo madomadogo ya kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi
kua mshindi kwa kuzoa kura 13,230,131, na Bw.Shafiq akiweza kuzoa
12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.
Chanzo: bbc swahili. http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
June 25, 2012
Mohammed Mursi Aibuka Kidedea Uchaguzi Wa Misri
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget