Waziri
Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake
kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi
jana Bungeni.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu
swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe,
aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo
huo.
Alisema
kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari
wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi
maeneo ambayo madaktari waliogoma.
Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.
Kuhusu
Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea
taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika
sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo
wa madakatari.
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.