StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 16, 2012

AJALI YAUA MMOJA NZOVWE MBEYA, SABA WAJERRUHIWA, GEITA 11 WAFA PAPOHAPO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Lori lakubeba kifusi cha mawe aina ya Skania Namba T 525ACP Mali ya Bhanji , lililo katika breki na kushindwa kusimama katika Mteremko wa Nzovwe na kuenda kugonga Gari aina ya Prado ambapo Dereva wa Gari hilo dogo alifariki hapo hapo.

Gari aina ya Prado lenye namba za usajili T720BUV iliyo kuwa inaendeshwa na mama Edna Sanga ambaye alifariki hapo hapo baada ya ajali hiyo.

Muuguzi katika Hospitali ya Rufaa Usebia Ulalo akiwasomea majina waandishi wa habari, ya majeruhi





Dereva wa Lori hilo Daudi akiwa amelazwa katika hospitali hiyo ya Rufaa Mbeya.



MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya Gari jana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.

WATU 11 wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea jana Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.

Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha Upasuaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.

Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo (36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa Kalangalala mjini Geita.

Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji hospitalini hapo.

Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la ‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land Cruiser.

Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla likakutana na gari linguine mbele.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat