Meli
ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama
majira ya saa nane mchana wa leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada
ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli
hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande
mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada
mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya
Bandari na vyombo vyengine.
Mpaka
tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na kiasi cha
abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya
Mnazimmoja.
Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.
Wazamiaji
kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali
kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!