Umoja
wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rhumba, Dance, muziki wa Injili na aina
zingine leo umetoa agizo kwa makampuni yanayouza miito ya simu nchini
pamoja na makampuni ya simu kuiondoa miitio hiyo ndani ya siku saba
kuanzia leo mpaka pale watakapokubaliana mikataba mipya.
Katika
barua hiyo iliyoandikwa kwenda kwa waandishi wa habari na iliyosainiwa
na wasanii zaidi ya 150 nchini, wasanii hao wameyataka makampuni ya simu
kuondoa matangazo ya ringtone hizo kwenye radio, magazeti, tv, website
na kwenye ujumbe mfupi wa simu.
Hatua
hiyo imechukuliwa na wasanii hao baada ya kubaini kuwa makampuni ya
simu yanawanyonya kwa kiasi kikubwa kwa kuwalipa chini ya asilimia 10 ya
mauzo ya ringtone hizo huku yenyewe yakibaki na zaidi ya asilimia 80.
Wiki
iliyopita mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe aliliibua suala hilo bungeni na
kudai kuwa imeundwa kamati itakayoangalia upya utaratibu wa mauzo ya
ringtone.
Press Release ndio hii.
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa
ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel,
Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la
kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na
Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na
kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka
hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki
wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na
nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu
ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya
biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka
wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika
kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu
ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni
asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili
linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya
pato toka kwenye shoo.
Hivyo
tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa
maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi
zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa
pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu
kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe
Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho
tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili
kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!