Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imemwagiza Meneja wa Mamlaka ya
Mapato (TRA), mkoani Arusha kutekeleza amri ya mahakama kwa kukabidhi
haraka magari saba ya kifahari ya wakili maarufu nchini Median Mwale
inayoyashikilia.
Akitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Charles Magesa alisema kitendo cha mawakili wa
Serikali, Fredrick Manyanda na Neema Ringo kuendelea kuzuia magari hayo
ambayo mahakama ilishayatolea uamuzi ni kuidharau mahakama na ni
kinyume cha sheria .
Alisema tangu kufunguliwa kwa shauri hilo la
jinai lililofunguliwa Agosti 9, mwaka jana linalomkabili mshtakiwa
Mwale, shauri hilo limeshindwa kuendelea kutokana na mawakili wa
Serikali kuendelea kuweka mapingamizi yasiyo ya msingi ya kuzuia magari
ya mshtakiwa Mwale na kusababisha kutoendelea kwa kesi ya msingi
inayomkabili.
Hakimu Magesa alisisitiza kuwa kitendo cha mawakili
wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kuandika barua TRA ya
kuzuia uamuzi ya mahakama na kuitaka TRA mkoani hapa isikabidhi magari
hayo ni utovu wa nidhamu na ni kinyume cha sheria.
Alisema hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia amri halali ya mahakama ispokuwa mahakama za juu pekee.
Hakimu
huyo alisema awali mahakama hiyo ilitoa hukumu Machi 7, mwaka huu ya
kutaka wakili Mwale arudishiwe magari hayo hata hivyo upande wa Serikali
haukuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa mahakama kuu chini ya Jaji
Kakusulo Sambu.
Alisema mahakama hiyo iliridhika na uamuzi ya
hakimu Magesa na kutaka faili la kesi hiyo lirudishwe katika mahakama
hiyo ya hakimu mkazi kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa shauri la msingi
linalomkabili.
Hata hivyo mawakili hao wa Serikali waliendelea
kupiga danadana na mara nyingi wamekuwa hawafiki mahakamani na wakifika
wanatoa sababu zisizo za msingi na kufanya kuahirishwa kwa shauri hilo.
Wakati
huohuo, hakimu Magesa ametupitia mbali maombi ya mawakili wa Serikali
waliyowasilisha mahakamani hapo ya kutaka ajitoe kwenye shauri hilo ili
haki iweze kutendeka wakidai kuwa ,hakimu Magesa amekuwa na ukaribu na
ndugu wa mshtakiwa.
July 3, 2012
Mahakama Arusha yaijia juu TRA, wanasheria wa Serikali
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget