Chopa
inayotumiwa na CHADEMA ikijiandaa kupaa kutoka viwanja vya NMC Arusha
kuelekea Simanjiro. Ndani yake wakiwemo Mh Godbless Lema, Alphonce
Mawazo na James Ole Millya.
Godbless Lema akiunguruma jukwaani hapo jana.
Ally
Bananga aliewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM akiwakilisha vijana
Arusha kabla ya kuhamia Chadema akiongea na wananchi wa Mirerani kupitia
vipaza sauti vya gari la matangazo wakati msafara ukielekea uwanjani
kuanza mkutano wa mwisho hapo jana.
James Millya akizungumza na wananchi wa Mirerani.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
----
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na operesheni yake ya M4C kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kujua mizizi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania nchini kote, na kukiweka chama karibu zaidi na wananchi.
Safari hii ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara kutembelewa na makamanda wa chama hicho hapo jana wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama, Mh Godbless Lema.
Mh Lema aliambatana na viongozi na makamanda wengine wakiwemo wanachama wapya waliohamia chama hicho hivi karibuni kutokea CCM. Miongoni mwao ni pamoja na James Ole Millya, Ally Bananga na Alphonce Mawazo.
Jumla ya mikutano saba ilifanyika kwa siku ya jana, sita ikifanyika kwa kuzuru maeneo tofauti ya Simanjiro kwa kutumia helcopta na baadae kumalizia na mkutano mkubwa wa jioni katika uwanja wa shule ya msingi Mirerani iliyopo eneo la Mirerani. Lema, Mawazo na Millya ndio waliotumia chopa na wengine walitumia gari mpya za chama hicho kwa njia za barabara kutokea Arusha Mjini.

0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!