Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
SIMBA
SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa
penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kufuatia
sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Penalti
za Simba zilikwamishwa nyavuni na Mwinyi Kazomoto, Amir Maftah na Kiggi
Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande wa Azam FC,
aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati Samir Hajji Nuhu
ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao
‘iliota mbawa’.
Kabla
ya matuta, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu alitangulia
kuifungia Simba dakika ya 29 kabla ya Hamisi Mcha ‘Vialli’ kusawazisha
dakika ya 45 na ushei.
Kipindi cha pili mchezo ulichangamka zaidi na dakika ya 81, John Bocco
‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili, kabla ya
Kazimoto kuisawazishia Simba kwa penalti dakika ya 87, baada ya Danny
Mrwanda kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa ushindi huo, Simba SC wamezawadiwa Sh. Milioni 10 na Azam FC Milioni 5.
|
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Sunzu (10) baada ya kufunga.
|
|
Aggre Morris wa kwanza kushoto, John Bocco wakimpongeza Viallli (wa pili kushoto) kufunga la kusawazisha |
|
Kikosi kilichoanza Azam |
|
Kikosi kilichoanza Simba |
|
Wachezaji
wa Timu ya Simba na viongozi wao wakishangilia baada ya Kutwaa
Ubingwabaada ya kuifunga Azam FC katika fainali za kuwania Kombe la
Urafiki mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. |
|
Milovan anaangalia saa dakika chache kabla ya mechi kwisha |
|
Uhuru Sulkeiman akiwa na Kombe la ubingwa: PICHA zaidi http://bongostaz.blogspot.com/ |
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!