StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 16, 2012

Simba wachapwa 2-0 na URA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Kipigo alichokipata Yanga katika mchezo wake wa awali dhidi ya Atletico ya Burundi kimejirudia leo kwa watani wao wa jadi Simba ambao nao kama Yanga wamechapwa goli 2-0 na URA ya Uganda.

Simba ilishuka katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo katika mchezo wake wa awali wa makundi kuwania kombe la Kagame.

Magoli la kwanza la URA lilipachikwa wavuni katika dakika ya 11 na mfungaji Feni Ali aliyevalia jezi namba 1O.

Wakati Yanga jana ikifungwa goli la pili katika dakika za nyongeza ndivyo ilivyokuta Simba leo baada ya kufungwa goli la pili katika dakika ya 90+2  kwa njia ya kichwa huku mfungaji akiwa yule Yule Feni Ali.

Magoli ya leo yote yamepachikwa kwa njia ya kichwa.

Wakati huo huo Simba inaweza kujutia kumuacha mchezaji wake wa zamani Derick Waluya ambaye leo alikuwa mlinzi mzuri na kizingiti kwa timu ya URA.






Mabingwa wa Soka Tanzania bara na Urafiki, Simba ya Dar es Salaam hadi sasa ipo nyuma kwa goli moja dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wa Makundi Kombe la Kagame.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat