Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Majambazi wanne wameuwawa mkoani Tabora wakati wa mapambano makali ya kurushiana risasi baina yao na Askari Polisi baada ya jaribio lao la kutaka kuvamia eneo la Congres centre kuzuiwa na jeshi hilo huku wakiwa wamejifunika usoni kwa vitambaa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Antony Rutta, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 25 mwaka huu majira ya saa tisa mchana katika kijiji cha Kaliua Magharibi, wilayani Kaliua Mkoani Tabora.
Kamanda Rutta alisema eneo la Congres Centre ambalo majambazi walipanga kuvamia ni eneo ambalo hutumiwa na wafanyabiashara wengi kufanya biashara zao.
Alisema majambazi hao walikuwa wakitumia bunduki aina ya Shot gun na baada ya tukio hilo bunduki hiyo ilipatikana ikiwa na risasi 12 na maganda sita ya risasi za silaha hiyo yaliokotwa eneo la tukio.
Aidha baada ya kutolewa vitambaa usoni jambazi mmoja aliyeuwawa ametambulika kwa jina la Masud Haruna mkazi wa Kijiji cha Imalamihayo, wilayani Kaliua na wengine watatu bado hawajatambulika.
CHANZO: NIPASHE
August 29, 2012
NEWS!!!!!! MAJAMBAZI 4 WAUWAWA MKOANI TABORA WAKATIWAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!