Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
NA Millionfortune.com News
|
Sisi
ni watu wa kujali jamii bwana... Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey
Nyange 'Kaburu' (katikati) akiwa pamoja na nahodha wa timu hiyo, Juma
Kaseja (kulia) na beki Juma Nyosso (kushoto) wakibeba vyandarua na
zawadi nyingine kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa wakati walipotembelea
hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sanula
Athanas |
|
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akiwa katika eneo la hospitali ya Mwananyamala. Picha: Sanula Athanas |
|
Chu chu chuuuuu.... tototoooooooo |
|
Mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha usajili, Salim Kinje pia alikuwepo Mwananyamala Hospital. |
|
Lengo
letu ni kusaidia jamii hivi kila mara... Kaburu (kulia) akitoa mawili
matatu wakati Simba ilipotembelea wagonjwa na kutoa zawadi leo. |
|
Mnaonaje hali ya hapa hospitali? |
|
Juma K. Juma akitoa chandarua kwa mgonjwa |
|
Kaburu akiongoza msafara |
|
Hii ndio Coaster yetu lakini basi kubwa la kisasa linakuja Agosti 15 |
|
Ezekiel Kamwaga akijiandaa kumwaga vyandarua hospitalini Mwananyamala leo |
|
Leo sio mwisho, tutakuja tena na tena... Kaburu akizungumza na akina mama hospitalini Mwananyamala |
VIONGOZI,
wachezaji na wazee mbalimbali wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,
Simba wamefanya tukio la kihistoria leo baada ya kutembelea wagonjwa
kwenye Hospitali ya Mwanaymala jijini Dar es Salaam na kugawa misaada
mbalimbali.
Tukio
hilo nadra kuonekana likifanywa na klabu za soka nchini limeelezewa na
uongozi wa Simba kuwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku maalum
ya kila mwaka ya klabu hiyo ya 'Simba Day'.
Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' ndiye aliyeongoza
msafara huo huku kwa upande wa wachezaji, kipa na nahodha Juma Kaseja
ni miongoni mwa nyota walioshiriki kukabidhi misaada hiyo, akiambatana
na nyota wenzake kadhaa wakiwamo Juma Said Nyosso, Kigi Makassy na
kiungo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Kenya, Salim Kinje.
Akizungumza
hospitalini hapo, Kaburu alisema kuwa wamewatembelea wagonjwa na
kuwapa misaada kwa vile klabu yao ni sehemu ya jamii na hivyo wanapaswa
kurejesha kidogo wanachokipata kwa kuwajali watu wenye mahitaji
maalum.
Akaongeza
kuwa mbali na kutembelea wagonjwa, pia watatembelea baadhi ya vituo
vya watoto yatima na kuwapelekea misaada mbalimbali.
Baadaye,
msafara huo wa Simba uliowatembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya
akina mama wajawazito na pia ya watoto waligawa vitu mbalimbali kama
vyandarua, maji na sabuni.
Mganga
Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Sophinias Ngonyani, aliwashukuru
viongozi na wachezaji wa Simba kwa hatua yao ya kuwatembelea na kugawa
misaada kwa wagonjwa; huku pia akiziasa klabu za soka na wanamichezo
wengine kuiga moyo huo.
MTOTO APEWA JINA 'JUMA KASEJA'
Katika
tukio mojawapo la kusisimua hospitalini hapo, mama mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Rose Joseph alisema kuwa amefurahi sana
kuwaona 'live' wachezaji wa timu anayoishabikia ya Simba an kwamba,
ameamua kumpa jina la 'Juma Kaseja' mtoto wake aliyemzaa leo asubuhi
kwa vile alipata bahati ya kubebwa na kipa huyo nyota wa 'Wekundu wa
Msimbazi' na timu ya taifa, Taifa Stars.
“Nimefurahi sana kumuona Kaseja akimbeba mwanangu,” alisema Rose.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!