Bahati Bukuku.
STAA wa nyimbo za Injili Bongo anayetamba na albamu ya Dunia Haina Huruma, Bahati Bukuku amenusurika kulimwa talaka baa kutoka kwa mumewe waliyetengana naye miaka 7 iliyopita, Daniel Basila.
Kwa mujibu wa chanzo, ishu hiyo ilitokea mwishoni mwa mwezi Julai, mwaka huu ndani ya Baa ya Land Mark Hotel iliyopo Ubungo, jijini Dar.
Ilidaiwa kuwa, Basila alimwita ‘mtalaka’ wake huyo hotelini hapo ampe talaka yake baada ya kuishi ‘singo’ kwa miaka saba huku ndoa yao ikiwa haijulikani hatima yake.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!