WAKAZI wa Kibamba, Kinondoni, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo,
wamezikimbia nyumba zao baada ya kutokea kishindo kikubwa cha milipuko
katika Kambi ya Jeshi la Vifaru ilyoko Mloganzila,Kisarawe, Pwani.
Tukio hilo limetokea kati ya saa tano na 7:04 usiku ambapo
milipuko hiyo ilikuwa mitano, ikiambatana na kukatika kwa umeme,
mawasiliano ya simu pia kukiwa na mvua kubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Fullshangweblog, wakazi hao
walisema tukio hilo limewashtua kwasababu halijawahi kutokea katika
miaka zaidi ya saba walioshi kwenye neo hilo.
Walisema waliamua kukimbia na kuelekea kusikojulikana kwa ajili ya kuokoa maisha yao.
Mmoja wa wakazi hao Mhando Yahaya alisema Wakazi wote wa Kibamba
walikimbilia kwenye kijiji kidogo cha Kibwegele ambapo waliamua kuacha
nyumba pamoja na mali zao bila kujali.
“Ujuwe serikali inabidi itowe angalizo kabla na siyo kufanya siri
kwa kuwa matokeo ya siri ndiyo kama haya wananchi tunatishika na
kukimbia hovyo usiku huu, mvua na giza vikituandama ”alisema Yahaya.
Naye Egnes Habiyu, alisema milipuko kama hiyo, imesababisha baadhi
ya wagonjwa wa moyo kushtuka hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu na
kuanguka kwenye maji ya mvua ilyokuwa ikinyesha.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo, Msemaji wa Jeshi
hilo, Kanali, Kapambala Mgawe alisema hayo yalikuwa mazoezi ya kawaida
na hayana uhusiano wowote wa kivita.
Vilevile aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa milipuko hiyo haina madhara bali ni moja ya mazoezi ya kawaida hivyo wawewatulivu.
Kanali, Mgawe alisema taarifa zilitolewa kwa wakazi wanaoishi
jirani na kambi hiyo, bali kwakuwa yalifanyika usiku kukiwa kumetulia
kumesababisha sauti ya milipuko hiyo kusikika mbali
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!