StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 5, 2012

HII NDIO MSG ALIYOTUMIWA IGP SAID MWEMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Vurugu za CHADEMA mikoani zimechukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk . Wilbrod Slaa, kumtumia ujumbe wa vitisho Mkuu wa Jeshi la polisi(IGP),Said Mwema.

Ujumbe huo uliotumwa kwa njia ya simu ya mkononi unamtaka IGP Mwema kuhakikisha askari wanakuwa na mabomu ya machozi, bunduki na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa CHADEMA watakaokuwa wakifanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.

Dr Slaa pia amesema iandaliwe karamu ya mauaji, kwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejipanga kukabiliana na polisi wataksokuwa wakiwadhibiti.

Pia amemueleza IGP Mwema na askari wake wajiandae kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.

Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema hayo jana alipozungumza na gazeti fulani maarufu hapa nchini kuhusu vurugu zilizotokea hivi karibuni, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten, Daudi Mwangosi.

Chagonja alinukuu ujumbe uliotumwa kwa IGP mwema uliosema 
“Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague”

Akizungumzia ujumbe huo, Chagonja alisema unaonyesha kiburi,ukaidi na kutotii sheria, hivyo jeshi la polisi litachunguza na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa.


CHANZO: KING JOFA

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat