StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 5, 2012

SIKU YA MTANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mahali: Tanzania House, 1232 22Nd Street, N.W. Washington D.C.; 20037
Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012 Kiingilio: BURE
Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo Watanzania watashiriki
kwenye kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (Wamarekani na wa Mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.

Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania. Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania. Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na huduma
zitolewazo na Watanzania waishio hapa Marekani.

Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni),vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na Watanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo. 

Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:

Dkt. Suitbert Mkama 202 884 1087 au barua pepe smkama@tanzaniaembassy-us.org
Asia Dachi 202 884 1096 barua pepe adachi@tanzaniaembassy-us.org
Rosemary Mziray 202 884 1081 
au barua pepe rmziray@tanzaniaembassy-us.org
Ubalozi unapenda kuwahamasisha 
Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.

Karibuni Wote

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat