Polisi wameviambia vyanzo vya New York Daily News kwamba kijana huyo alikuwa akikabiliwa na baadhi ya masuala ya kifedha ikiwamo deni la $ 5,000,000 alilokuwa kaidaiwa katika kodi.
Kulingana na New York Post ukurasa wa Sita, akaunti ya benki Lighty haikuwa na hela kufuatia talaka wake kutoka kwa mke wake wa miaka saba, Veronica, mwaka jana.
Mara baada ya habari za kifo chake wengi wameandika katika kurasa zao za Twitter kutoa heshima zao. "Pumzika kwa amani Chris Lighty, tunawaombea familia na wapendwa!" Aliandika Rihanna, na kuongeza, "Mungu tafadhali umpe rehema."
Mwanzilishi wa Def Jam Russell Simmons nae aliandika katika ukurasa wake wa twitter, "Leo hii, tumempoteza shujaa wa hip-hop na mmoja wa wabunifu katika sanaa hii."
Baaadhi wengine waliondika kuhusu kifo hicho na kutoa pole ni Kim Kardashian na wengineo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!