StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 19, 2012

HAWA NDIO MAPADRE WA KANISA KATOLIKI WALIOVAMIWA NA KUJERUHIWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Angelo Burgeo (60).
PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto, mapanga na nondo.

Mbali na kupigwa risasi katika ubavu wake wa kushoto na kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea majira ya 4.45 usiku wa kuamkia leo, Padri Burgeo alijeruhiwa vibaya nyuma ya kichwa chake baada ya kupigwa na nondo.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako viongozi wamelazwa kwa ajili ya matibabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.

Herman Myalla (36).
"Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza kupatiwa matibabu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.

Tukio hilo limetokea ikiwa siku moja tu baada ya mlinzi wa Kanisa Katoliki Kihesa Iringa Mjini, Bathelomeo Nzigilwa (64) kujeruhiwa vibaya na majambazi waliovunja kanisa hilo na kufanikiwa kuiba mali mbalimbali zikiwemo fedha taslimu.

Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.

MAGAZETI YA LEO NOV 19

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


.


November 16, 2012

BAADA YA DODOMA, RAIS KIKWETE ATUA ARUSHA, VIONGOZI WA DINI WAMUOMBEA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro jioni leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha (picha: Ikulu)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha (picha: Ikulu)

(picha: Ikulu)

(picha: Ikulu)

WAKILISHA NCHI YAKO, JIUNGE NA GUINESS FOOTBALL CHALLENGE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Wakilisha Nchi Yako Jiunge na Guinness FootBall Challenge Sasa

HUU WIZI WA VIFAA VYA MAGARI DAR ES SALAAM UMEKITHIRI...HEBU SOMA HII

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Ni hoja aliyoianzisha mwanachama mmoja kwenye ukumbi wa Mabadiliko Tanzania:

Jamani imekua tabia sasa ambayo naona serikali hasa kwenye mji wa Dar imeshindwa kabisa kuchukua hatua za kuzuia au angalau kulikemea hili suala, kwa ufupi mamlaka husika ni kama hazipo kutekeleza wajibu wake wa kisheria wa kulinda raia na mali zao!!!

Kuna tatizo kubwa sana la magenge ya majizi kuiba taa, side mirrors, vitasa vya milango au power windows na kila kinachoweza kuchukulika katika magaari ya watu mchana kweupe au hata usiku.

Binafsi nimepatwa na hili tatizo kama mara 3 au 4 hivi, nikaambiwa niende eneo la Gerezani, na kweli nikavipata, ila sasa nikatumia ukamanda kwa kushirikiana na jamaa zangu wa jeshini nikavichukua kwa nguvu bila kuvinunua.

Kununua maana yake ningeliuziwa mali yangu mwenyewe, na hilo lilikua linanikera sana sana kabisa. Ndio maana pamoja na kuvichukua kwa nguvu pia tukatembeza kichapo kwa hawa wezi...

Nimewahi kuripoti suala hili polisi ila kumbe kuna baadhi yao wanashiriki katika hii kazi haramu na inaumiza sana watu kwani sio tu wanaiba hivo pia wanachukua laptops za watu na kusababisha hasara kubwa sana kwa wakazi wa huu mji wa Dar.

Kibaya zaidi ni tabia ya watu hawa kuiba mchana na usiku kwenye foleni au maeneo ya Mlimani City, Vyuoni, Makazini... yaani kwa ufupi kila mahala ukisimamisha gari lako sio salama na unaenda roho inakuuma, je ntalikuta salama?!!

Mamlaka husika zinajua na kama hazijui hazifai kuwepo. Kwa nini ile sentensi intelijensia haitumiki hapa kukomesha wizi huu?

Imefikia hatua nawapa changamoto watu wa Dar ambao unaibiwa mchana na wao wanaona wanakaa kimya kama hawaoni, acheni tabia hizi za ovyo maana leo wewe kesho mwingine. Mimi mara zote nawakabili kwa nguvu, labda nisiwakute, ila nikiwakuta huwa simwachi salama lazima awe kilema, nahakikisha hataiba tena! Watu hawa nimeshuhudia mara 5 wakiwavamia akina mama na kuwanyanganya laptop na hapo usaidizi ukijaribu unashindwa maana na mimi sitaacha gari ili waibe, ila ukikabidhi mwenzio ni rahisi tukawakabili na watajua kwamba sasa sio rahisi kuiba, na sisi kama jamii tutajinusuru bila kutegemea polisi.

Nawasilisha.

Heche Suguta
hechesuguta29@yahoo.com



Nionavyo mimi...
Jeshi la polisi kwa kutokufanya kazi yenu barabara katika kulinda usalama wa raia na mali zao, ndiyo sababu ya kuchangia kuongezeka kwa watu kujichukulia sheria mikononi.

Wananchi kwa kutokusaidiana katika kukomesha tabia ya wizi

1. kwa kutokununua mali za wizi
2. kwa kutokudai risiti halali
3. kwa kutokutoa msaada pale tunaposhuhudia uhalifu unafanyika

tunachangia kukua kwa tatizo hili.


Subi

KUTOKA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI URUSI: WAKOSA CHAKULA NA MALAZI HALI YAO MBAYA, PATA HABARI KAMILI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya. Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.

Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.

Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu kama huna bima ya afya.

Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada kwa wakati.

Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi
ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.

Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao tupo hatarini huku ugenini.

Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3).

URINE-POWERED GENERATOR PRODUCE SIX HOURS OF ELECTRICITY

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
We've all heard the expression "haste makes waste," but how about waste making energy? At the fourth annual Maker Faire Africa in Lagos, Nigeria, a quartet of teenage girls ages 14 through 15 have created a urine-powered generator. This eco-friendly energy source cranks out six hours of electricity for every liter of human bodily fluid by separating the excretion's hydrogen with an electrolytic cell. While this method of human waste disposal seems promising, the device has the potential to be a pee-powered biobomb and will need more than its limited safety measures before you're able to pick one up at your local hardware store. However, if this can help us save a few bucks on our energy bill, then we need to introduce these girls to these guys posthaste.

Huawei Yazindua Mpango Wa Teknohama Katika Sekta Ya Elimu Nchini.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China
Katika Mradi huo wa Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuoni kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo kwamba Mpango huu unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika shule za Primary na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema katika Program hii itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na Teknolojia.

Balozi wa China nchini Tanzania Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika shule na vyuo nchini Tanzania.
Balozi alisema mpango huu ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii.
Aliongeza kwamba Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.

Meza kuu.

Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini Tanzania.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.

Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.

Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.


Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat