Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amezungumzia afya yake na kueleza kwamba madaktari waliomfanyia uchunguzi wa vipimo wamethibitisha kwamba ni njema.
Taarifa ya Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli (CCM), kwa vyombo vya habari jana ilieleza kwamba kutokana na afya yake kuwa nzuri atarejea nchini kutoka Munich, Ujerumani hivi karibuni.
“Namshukuru Mungu siha yangu ni imara na kwamba madaktari walionifanyia uchunguzi wamejiridhisha pasi na shaka kwamba afya yangu ni njema…nimeendelea kupata maendeleo na matibabu mazuri katika jicho langu moja ambalo nilifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita hapa hapa, Ujerumani,” alisema katika taarifa hiyo.
Alisema “natarajia kurejea nyumbani wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuungana na Watanzania wenzangu katika kulijenga taifa letu.”
Alisema amekuwa jijini Munich kwa wiki nzima sasa na kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi na katika taifa kwa ujumla.
“Nikiwa mwana CCM na Mtanzania nasononeshwa sana na taarifa za kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chama chetu, serikalini na katika taasisi mbalimbali,” alisema.
Alisema rushwa ni tatizo na kansa ambayo inapaswa kutafutiwa ufumbuzi wa kimfumo badala ya kuendelea kufikiri kwamba linaweza kumalizwa kwa njia ya kulalamika, kulaumiana na kupakana matope.
November 7, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!