StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

June 26, 2012

TPBC: MIKATABA YA FRANCIS CHEKA NA PROMOTA KAIKE SIYAJI INATAMBULIKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba) kati ya Francis Cheka na Kaike Siyaji aliyosaini kupigana na Japhet Kaseba siku ya July 7, mwaka huu.

 Aidha Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia Francsi Cheka awe na mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili hali ya kutoelewana iliyokwisha kujitokeza imalizwe kwa manufaa ya tasnia ya ngumi nchini.

TPBC inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya wote yalindwe.

Tunapenda pia kuwashauri mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba zaidi ya mmoja hususan wakati bado wakiwa na pambano mkononi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat