Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
VIGOGO 10 waliokuwa wanatuhumiwa kwa ubadhirifu kwenye Ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika Wizara ya
Maliasili na Utalii wamesimamishwa kazi.
Operesheni hiyo safisha
inaendeshwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
ambaye amethibitisha kuwa vigogo hao wamesimaishwa kupisha uchunguzi wa
tuhuma dhidi yao.
Waliosimamishwa wametambuliwa tu kwa vyeo vyao,
ni Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Matumizi ya Wanyamapori, Mkurugenzi wa
Leseni na Uwindaji, Mkurugenzi wa Uwindaji, Mkurugenzi Msaidizi
Maendeleo ya Wanyamapori, Ofisa Mfawidhi Kituo cha Cites na Uwindaji
Arusha.
Wengine ni Ofisa wa Kituo cha Utafiti Arusha, Kaimu
Mfawidhi wa Cites Arusha, Ofisa wa Uwindaji na Utalii Arusha pamoja na
ofisa mmoja wa makao makuu, kitego cha Cites na Uwindaji.
Kabla
ya kusimamisha vigogo hao, tayari Balozi Kagasheki alianza kwa
kuwasimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wanyamapori, Boneventura
Tarimo na Ofisa Wanyamapori Mkuu, Mohamed Madehele.
Balozi
Kagasheki alisema juzi kwamba waliosiamishwa wanachunguzwa na
wakithibitika kufanya ubadhirifu watachukuliwa hatua zaidi za kinidhamu.
“Ni kweli wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Wakibainika watachukuliwa hatua za kinidhamu,” alisema Kagasheki.
Ripoti ya CAG
Kusimamishwa
kwa maofisa na wakurugenzi hao kunatokana na ubadhirifu uliotajwa na
CAG katika ripoti yake ya mwaka uliopita, kitendo kilichosababisha
aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Ezekiel Maige kung’olewa katika nafasi
hiyo kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya
Kikwete Mei 4 mwaka huu.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa hiyo ilipoteza
Sh874,853,564 kutokana na kufanya uamuzi wa upendeleo wa kutoa kiwango
cha chini cha mrahaba kwa mauzo ya misitu.
Maige pia alishutumiwa
kwa kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya
uwindaji, ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na
kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha ni vitalu vipi
walivyopewa.
Pia, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba
na kwamba, vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili.
Mbali na tuhuma hizo, Maige hivi karibuni alidaiwa kununua nyumba kwa
dola 700,000 za Marekani katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua
kwa dola 410,000, sawa na zaidi ya (Sh600 milioni).
SOURCE: MWANANCHI
June 26, 2012
WIZARA MALIASILI: KAGASHEKI ASIMAMISHA VIGOGO 10
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget