RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa
kuwa refa wa mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya
Yanga.
Mechi
ya wabunge hao mashabiki wa Simba na Yanga, inatarajiwa kufanyika Julai
7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya matukio
yatakayopamba Tamasha la Usiku wa Tumaini.
Meneja
Mkuu wa Global Publishers, wanaoandaa tamasha hilo, Abdallah Mrisho,
alisema kuwa wameshamuandikia barua JK ya kumuomba awe mgeni rasmi,
vilevile awe refa wa mechi hiyo ya wabunge na kwamba matarajio ni
mazuri.
“Tuna
matarajio ambayo ni chanya kuhusu Mheshimiwa Rais kuingia uwanjani na
kuchezesha mechi ya wabunge na kwa kweli hili litakuwa tukio la
kihistoria kuwahi kutokea,” alisema Mrisho na kuongeza:
“Tunaamini
kwamba kitendo Mheshimiwa Rais kuchezesha mechi hiyo ya wabunge, siyo
tu kwamba kitawafurahisha wananchi watakaohudhuria tamasha hilo la Usiku
wa Tumaini, bali pia kitakuwa faraja kubwa kwa kila mhudhuriaji na
Watanzania kwa jumla.”
Katika
tamasha hilo, mbali na mechi ya wabunge, kutakuwa na mchezo wa soka
kati ya wasanii wa filamu Tanzania (Bongo Movie) dhidi ya wenzao wa
muziki (Bongo Fleva). Vilevile wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo,
watachuana na wenzao wa Shule ya Sekondari Jitegemee.
Upande
wa masumbwi, bondia Francis Cheka atamaliza ubishi na Japhet Kaseba,
ikikumbukwa kwamba mara ya mwisho walipopigana, pambano lao halikufika
mwisho.
Kuhusu
burudani, wanamuziki wakali jukwaani, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ na
Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ watapambana kuoneshani ni nani anatisha kwa
kumiliki ‘steji’ ukanda wa Afrika Mashariki.
Wakali wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma’, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’, Kundi la Pah One na wengine wengi watakuwepo.
Source; Global Publishers Info