Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya Uwekezaji 2012 yenye kauli mbiu 'Sera
Kuelekea Kizazi Kipya katika Uwekezaji' ambapo
amewasisitiza watunga sera wa Tanzania kutumia rasimu ya Sera ya
Uwekezaji ya Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2012 kama kipaumbele katika
kuunda sera za Kitaifa za Uwekezaji. Kushoto ni Afisa Habari wa Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC) Bi. Stella Vuzo.
Baadhi ya Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini waliohudhuria uzinduzi wa World Investment Report 2012.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi akiwasilisha Ripoti hiyo
ya Mwaka 2012 ambapo amezungumzia zaidi mazingira ya uwekezaji Tanzania
huku akigusia mwelekeo, changamoto na fursa zinazopatikana.
Bw. Raymond Mbilinyi ameweka wazi kuwa
mujibu wa Ripoti hiyo Tanzania kwa sasa imepiga hatua katika kuboresha
miundo mbinu haswa ya Barabara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Dkt. Alberic Kacou (kushoto) na wadau wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya Fursa za Uwekezaji 2012.
Pichani ni Minongoni mwa Mabalozi,
wawakilishi wa Serikali, wakuu wa mashirika ya Maendeleo, wawakilishi wa
mashirika ya kijamii katika uzinduzi huo.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akimkaribisha Dkt. Kacou na Bw.
Mbilinyi (hawapo pichani) kuzindua rasmi 'World Investment Report 2012'.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akikata utepe
kuzindua kitabu chenye Ripoti ya Uwekezaji ya Kimataifa 2012 sambamba
na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mkurugenzi wa Zamani wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania Bw. Emmanuel Ole Naiko akitoa maoni yake kuhusiana na
Ripoti ya Kimataifa ya Uwekezaji 2012.
Pichani Juu na Chini Wadau wa Sekta ya
Uwekezaji, Maafisa wa Umoja wa Mataifa, Mabalozi pamoja Wawakilishi wa
Idara mbalimbali za Serikali waliohudhuria Uzinduzi huo.
Pichani
ni Minongoni mwa Mabalozi, wawakilishi wa Serikali, wakuu wa mashirika
ya Maendeleo, wawakilishi wa mashirika ya kijamii katika uzinduzi huo.
Dkt. Alberic Kacou na Mkurugenzi wa
Zamani wa kituo cha Taifa cha Uwekezaji chini Bw. Emmanuel Ole Naiko
wakipeana mkono wa Pongezi baada ya kuzindua Ripoti ya Kimataifa ya
Uwekezaji 2012.
Dkt. Kacou akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya uzinduzi huo.
Bw. Emmanuel Ole Naiko (kulia) na Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa
hapa nchini (UNDP) Bi. Louise Chamberlain wakijadili kuhusu umuhimu wa
matumizi ya Ripoti za Uwekezaji katika kukuza uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!