Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa taarifa
kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusiana na Kuzama kwa Meli ya
Skagit na hatua Zilizochukuliwa na Serikali huko katika Ukumbi wa Baraza
la wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akifafanua jambo
katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na hatua
Zilizochukuliwa na Serikali baada ya kuzama kwa Meli ya Skagit huko
katika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Gaazeti la Habari leo Khatib Suleiman akiuliza
maswali kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bolozi Seif Ali Idi
hayupo pichani katika Mkutano wake na waandishi hao kuhusiana na Kutoa
taarifa ya Kuzama kwa Meli ya Skagit na hatua zilizochukuliwa na
Serikali huko katika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi la Zamani Kikwajuni
Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliofika katika Mkutano wa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kuhusiana na Kutoa taarifa ya
Kuzama kwa Meli ya Skagit huko katika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi la
Zamani Kikwajuni Zanzibar.Picha na Yussuf Simai,Maelezo-Zanzibar
--
--
Makamo
wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuunda Tume ya uchunguzi wa ajali ya
Mv. Skagit iliyozama July 18 mwaka huu ambapo jumla ya abiria 290 walikuwemo katika meli hiyo.Balozi
Seif ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo
katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni kuhusiana na
kuzama kwa meli hiyo.
Amesema
Tume hiyo itaweza kuishauri Serikali nini cha kufanya katika
kuhakikisha kuwa vyombo ambavyo vinachukuwa abiria vinakuwa vya aina
gani na kuweka utaratibu mzuri utakaoweza kufanikisha usafiri wa
baharini.
Ameongeza kuwa kutokana na hali ya ajali zinazotokea mbali na Tume hiyo,Serikali imeona kuwa ipo haja ya kupitia
sheria zinazohusu usafiri wa baharini na kuweka aina ya viwango vya
meli zitakazoruhusiwa kuingizwa nchini na kuchukua abiria.
Makamu
wa Pili wa Rais amesema kuwa nia ya Serikali juu ya ununuzi wa Meli kwa
ajili ya usafiri ipo pale pale na kwamba juhudi zinaendelea katika
kufanikisha suala hilo.
Akizungumzia
kuhusu ajali hiyo Balozi amefahamisha kuwa jumla ya watu 146 mpaka sasa
wameokolewa wakiwa hai ambapo Maiti 78 zilipatikana wakiwemo
wanaume,wanawake na watoto.
Aidha
amesema kuwa Chombo hicho kilikuwa na Raia wa kigeni 17 na waliookolewa
wakiwa hai ni 15 mmoja amepatikana akiwa amefariki ambaye ni Raia wa
Uholanzi na mmoja mpaka sasa hajapatikana.
Wageni hao kutoka nchi za nje ni wa Ubelgiji,Marekani,Ujerumani, Uholanzi pamoja na Israel na Serikali imetoa huduma kwa wageni hao na tayari wameondoka kurudi makwao kwa salama.
Makamo
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alieleza kuwa kati ya majeruhi 138
waliopelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja iliyopo mjini Zanzibar kwa
uchunguzi hadi kufikia leo wagonjwa wote hao walikwisharuhusiwa baada ya
kupata matibabu.Amewataka
wananchi popote pale ambapo wataiona maiti wapeleke taarifa kwa Jeshi
la Polisi,Wakuu wa Wilaya,Mikoa na Masheha ili taratibu za kuihifadhi
maiti hiyo ziweze kuchukuliwa.
Amesema
kuwa zoezi la uokoji linaendelea na kuwashukuru wananchi Vikosi vya
ulinzi vya Tanzania na vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na
vyombo binafsi na wazamiaji kutoka nchi za nje kwa ushirikiano walioutoa
uliofanikisha kazi ya uokoji wakiwemo pia waandishi wa habari na
wafanyabiashara.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!