StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 22, 2012

MIKATABA YA MADINI SASA KUGAWANYWA FIFTY FIFTY WAWEKEZAJI KWA WAZAWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi.
Serikali ipo mbioni kubadili mikataba ya madini kati ya wazawa na wawekezaji kutoka nje na kuifanya kuwa nusu kwa nusu yaani asilimia 50%kwa50% ili kuchangia pato la taifa na kuifanya rasilimali ya madini kusaidia kukuza uchumi na kuwanufaisha watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Eliakim Maswi wakati akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wadogo wa vito jijini Arusha na kusema kuwa kama tumeshindwa kuiendesha sekta hiyo ni bora tukaichia kizazi kijacho ili vizazi vijavyo visije kutulaumu .

Maswi alitanabaisha kuwa kwa kuanzia na mkataba wa kampuni ya Tanzanite one ya wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambao upo mwishoni mwa mkataba wake.

“Kampuni ya TANZANITE ONE mkataba wake umefika kikomo hivyo wakishailipa serikali mrahaba na kama watahitaji kuendelea basi mkataba wetu ni nusu kwa nusu”alisema Maswi.

Aliongeza katibu mkuu huyo kuwa kuanzia sasa watajitahidi ili sekta hiyo ichangie pato la taifa kama nchi nyingine zenye rasilimali hiyo zinavyo nufaika na sekta ya madini.

Nae Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa madini hapa nchini Sammy Mollel alisema kuwa wanataka kuifanya Tanzania kuwa kituo cha uuzaji,ukataji na ununuzi wa madini na vito katika bara la Afrika na kutaka serekali kuwapa ushirikiano kwenye hilo.

Mollel alisema kuwa wao watatoa ushirikiano kwa serekali kuweza kuwadhibiti wale wote wanaokwepa kuilipa serekali mapato na kuwafichua wafanyabiashara wakubwa wanaokwenda moja kwa moja migodini.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat