StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 31, 2012

MKUTANO MKUU WA WANAHISA TBL JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria, Steve Kilindo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche.

KWA PICHA NA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WILL.I.AM AND CHERYL COLE WAPATA AJALI WAKITOKA STUDIO JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




WILLIAM NA CHERLY JANA BAADA YA AJALI HIYO AMBAYO HAWAKUPATA MAJERAHA MAKUBWA

Rapa maarufu wa kundi la Black eyed peas William alikuwa akiendesha gari kando ya barabara katika mji wa Los Angeles na mwimbaji wa uingereza Cheryl Cole mapema jana asubuhi wakati gari lake lilipogonga gari ambalo lililokuwa limeegeshwa. 

Msemaji wa nyota huyo awali alijaribu kuficha tukio kwa kueleza kuwa kama "tukio lisilo la umuhimu" na kusisitiza hakuna aliyeumia, lakini picha halisi polisi waliyoikuta baadae ilikinzana na msemaji huyo kwani walikuta damu eneo la tukio

Katika tukio hilo, william aliweza kuonekana kuwa na matone ya damu yakitiririka uso wake baada ya airbag ya gari kuzuia kichwa chake kutoka katika usukani.

CHANZO CHA KIFO CHA MTOTO WA RAMBO (SYLIVESTER STALLONE) HIKI HAPA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

KUSHOTO NI RAMBO (SYLIVESTER STALLONE) NA KULIA NI SAGE STALLONE MAREHEMU MTOTO WA SYLIVESTER STALLONE
 
Sage stallone enzi za uhai wake.
 
Mwana wa Sylvester Stallone, Sage Stallone, alifariki dunia kifo cha asili, millionfortune hot news imetanabaishwa.

Alikutwa amekufa katika nyumba yake na mfanyakazi mwenzake Julai 13. Hakuna mchezo mchafu alikuwa watuhumiwa, na Matokeo ya toxicology test yalionyesha tu kiasi kidogo cha hydrocodone katika mwili wake.Ingawa madawa ya kulevya hayajahusishwa na kifo cha kijana huyo aliyekufa kiwa na umri wa miaka 36, kiasi kidogo cha hydrocodone Painkiller kilikutwa katika mfumo wake.
Mapema mwezi huu, Sylvester akieleza kuhusu kifo cha mwanawe, akieleza "Good Morning Amerika" ya kwamba kukabiliana na hasara imekuwa "mgumu sana." Aidha vifo vimekuwa vikikabili familia yake kwani hivi juzi amefiwa na dada yake.

MUST SEE THIS: WEMA SEPETU "YOU ROCK GIRL"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Wema hails from a Diplomat Family ; the last child in a family of four girls of Ambassador Isaack Abraham Sepetu. This beautiful soft spoken and light skinned girl, started performing since her childhood in school Drama’s in Dar es Salaam. She was born in 1988 at Dr Andrew’s Hospital, Dar es Salaam. 

KUJUA MENGINE ZAIDI KUHUSU WEMA, ELIMU, MAFANIKIO KIMAISHA, AND SO MUCH MORE..

DIAMOND KUSHUSHA VITU MAREKANI KESHO KUANZIA SAA NNE USIKU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


VIP TABLES ZIMEBAKI CHACHE PIGA SIMU HIZI ;-
      DMK  301-661-6207  &  J&P  240-605-1870

MAKAMU WA RAIS DR. BILAL AKIHUTUBIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZISIZOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya Watanzania walioongozana na Makamu Rais katika Mkutano huo wakiwa kwenye picha ya Pamoja.


Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilali akihutubia Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Siasa ya Upande wowote unaomalizika leo mjini Teheran, Iran. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine alisisitiza msimamo wa Tanzania kuendelea kupigania haki, kutetea wanyonge, kupinga ubeberu na ukandamizaji kote duniani, pia aliiasa Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro yote kwa njia ya amani.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


MAHAKAMA YAMPATA WAZIRI NA HATIA YA MAUAJI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Maya Kodnani.
MAHAKAMA moja nchini India imempata na hatia waziri wa serikali kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya waisilamu tisini na tano wakati wa ghasia za kidini katika jimbo la Gujarat miaka kumi iliyopita.

Maya Kodnani aliyekuwa waziri wa mambo ya wanawake, alituhumiwa kwa kuchochea ghasia dhidi ya jamii za waisilamu katika wilaya ya Naroda Patiya mjini Ahmedabad.

Alipatikana na hatia akiwa na mshtakiwa mwenzake ambaye ni kiongozi wa wapiganaji wa kihindu Babu Bajrangi pamoja na washukiwa wengine thelathini.

Ghasia za Gujarat zilizuka baada ya mahujaji sitini wa kihindu kufariki katika ajali ya Treni.

Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa waisilamu waliuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA KINONDONI AFARIKI DUNIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni na Mbarali Hawa Ngulume amefariki duniahospitali ya Jeshi ya Lugalo, jijini Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana amesema taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa baadaye.Pichani juu alipokua akizungumza na waadishi wa habari nyumbani kwake Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Juu ya Maradhi yanayomsumbua hivi karibuni

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MAZISHI YA ASKOFU WILLIAM KIKOTI, HAPA AKITIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, Mhashamu Pascal William Kikoti kwenye nyumba ya Askofu ilioyoko makao makuu ya jimbo la Mpanda Agust 30, 2012. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

TISHIO TANZANIA, WATOTO WA MTAANI, WANAONGEZEKA KWA KASI! SOMA HII

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Watoto wa mtaani wanaojishughulisha na shughuli za kujipatia kipato katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, wakiwa wameuchapa usingizi huku mmoja wao wakijiuliza na kujishauri kuamka wakati baadhi yao tayari wakiwa wameamka na kuanza kazi za kusafisha Vioo vya magari eneo hilo latika foleni ili kujipatia chochote kwa ajili ya kununua chakula.


Hawa ni baadhi yao wakiwa tayari wameamka wakipeana vifaa vya kufanyia kazi ili kuanza kazi yao ya kuosha vioo vya magari.
Kwa uchunguzi ulifanywa na blog yako ya jamii millionfortune hot news, tumegundua wimbi la kuongezeka kwa watoto hawa wa mitaani  linatokana na kupungua kwa malezi sahihi katika jamii na baadhi ya wazazi kutohudumia vema familia zao au kukwepa majukumu hivyo watoto wengi kuachwa wakiishi na bibi au babu zao ambao wengi wamekuwa hawawezi kuwalea wajukuu zao vema. Aidha kwa kutumia mwanya huo watoto hao wamekuwa wakitoroka na kuja mijini kutafuta maisha na huishia kuwa watoto wa mitaani na wengi wao huishia kutumia madawa ya kulevya, bangi na miraa na kazi zao kubwa kupora na kuiba vitu huku wakijishikilia chini ya miamvuli ya kazi kama kuosha vioo vya magari katika mataa na kubeba mizigo.

ANGALIZO: 
TAIFA LA KESHO LINAELEKEA WAPI ? WATOTO HAWA WENGINE WANAKUA NA KUWA WATU WAZIMA WAKIWA KATIKA HALI HII NA MAZINGIRA HAYA MWISHO WAKE NI NINI?

WALIOIGOMEA SENSA WAKIONA CHA MTEMAKUNI, HEBU FUATANA NAMI HAPA!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Pichani ni wananchi waliokataa kuhesabiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bwana Guram Hussein Kifu. katikati ni Kiongozi wa Mgomo Bwana Ally Mwangoto, kutoka dini ya Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali wakiwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,wakisubiri kupelekwa Polisi wilayani humo.



Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu nchini kushiriki zoezi la Sensa ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa kwa madai kuwa serikali imepuuza madai yao.


Imeelezwa kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa kuhesabiwa.


Akizungumza na BLOG YETU jana kuhusiana na madai hayo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.


“Wao wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.

WOW! MJENGO MPYA WA MHE. MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE ULIOPO MBEZI BEACH DAR ES SALAAM UNATISHA, BOFYA UJIONEE MWENYEWE!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
Watu wakijiachia
Kabati la vyombo
Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi la kifahari mjengoni humo
Wakati wa msosi
Mambo ya dressing table
Kitanda chake cha kulalia
---

Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.

Picha kwa hisani ya Mdau Kapingaz blog

August 30, 2012

UDAKU POINT: AMANDA AFUNGUKA;-SIJAPENDA KUITWA MGUMBA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’.

Na Gladness Mallya
BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ kutukanwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa ni mgumba, mwenyewe amefunguka na kusema madai hayo si ya kweli.
Akichezesha taya na Motomoto Newz, Amanda alikiri kutukanwa katika mtandao kuwa yeye ni mgumba kwa vile alikaa kwenye ndoa kwa miaka minne bila kuzaa.
“Mimi si mgumba, niliwahi kubeba mimba miaka ya nyuma ikatoka. Pia umri wangu bado mdogo kuitwa jina hilo, sikutaka kuzaa kwenye ile ndoa kwa sababu zangu,” alisema Amanda.


MWENYEKITI BMT AZINDUA ROCK CITY MARATHON 2012

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Wadhamini wa tamasha la Rock City Marathon 2012, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jana katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Mauaji Ya Morogoro

Tweeted this Like this, be the first of your Friends





Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga kauli za Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye kulipotosha taifa kuhusu mashambulizi na mauji yanayoelezwa kufanywa na askari Mkoani Morogoro na badala yake kinataka uchunguzi huru ufanyike haraka kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act).


Kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani zina mwelekeo wa kulilinda Jeshi la Polisi ambalo askari na maofisa wake ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji, badala ya kuwezesha ukweli kuthibitika na hatua kuchukuliwa kwa wahusika.
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, FAHAMU JINSI WANAWAKE WANAVYOCHANGIA TATIZO HILI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.

Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:

BOFYA HAPA ILI UISOME HABARI KAMILI

August 29, 2012

POLISI MKOA WA MANYARA WAKUMBWA NA KASHFA; WA MPIGA KIJANA MPAKA KUPOTEZA FAHAMU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

KIJANA HUYO AKIWA HOSPITALI

MAMA MZAZI WA KIJANA KADOGOO KALANGA AMBAYE ALIPIGWA NA MAASKARI WA KITUO CHA OLKESIMETI IKISEMEKANA AMEIBA MBUZI AKIWA ANAONYESHA SEHEMU AMBAZO MTOTO WAKE ANAMAUMIVU MAKALI MARA BAADA YA UPIGWA.

WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SELIANI WAKIWA WANAMTOA KIJNA HUYO KWA AJILI YAKUMUAMISHA HOSPITALI MARA BAADA YAKUKOSA KIFAAA CHA KUMPIMIA KTIKA HOSPITALI HIYO AMBAPO ALIPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA AGAKHAN.

KASHFA nzito imelikumba jeshi la polisi mkoani Manyara baada ya askari wake watatu kutuhumiwa kumpiga kijana ,Kadogoo Kalanga(16) mkazi wa Orkesmet wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu kitendo kilichopeleka kijana huyo kulazwa wodi ya wagonjwa mahututi(ICU) katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.

Tukio hilo lilijitokeza juzi majira ya saa 5;30 katika eneo la Orkesmet ambapo askari hao mmoja wao akitambulika kwa jina moja la John walimkamata mara baada ya kumtuhumu kuiba mbuzi wa jirani yake ambaye ametambuliwa kwa jina la Mama Shedi mkazi wa eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian mama mzazi wa kijana huyo,Paulina Kalanga alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi hao kabla ya kuanza kumshushia kipigo kikali.

Alisema kwamba mara baada ya kumkamata walianza kumpiga kwa kutumia rungu na mateke katika maeneo yake mbalimbali ya mwili kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na mkojo mfululizo na kisha kupoteza fahamu.

Huku akitokwa na machozi mama huyo alisema kwamba askari hao wakati wakiendelea kumpiga kijana wake walimshika katika sehemu zake za siri na kisha kuzivuta huku wakizigongagonga kwa kitako cha silaha ya moto.

“Walimkamata na kisha kuanza kumpiga kwa marungu na mateke na kama hawakuridhika wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kuzigongagonga na kitako cha silaha ndipo akaanza kukojoa na kisha kupoteza fahamu”alisema huku akitokwa na machozi

Mama huyo alienda mbali zaidi na kusisitiza ya kwamba polisi hao baada ya kuona hali ya kijana wake imekuwa mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa ajili ya matibabu.

Hatahivyo,alisema kwamba alipokea taarifa kutoka kwa rafiki yake kuhusu tukio hilo na ndipo alipochukua jukumu la kukimbia kituoni hapo na kukuta hali ya kijana wake ikizidi kuwa mbaya ambapo alikuwa haongei huku akirusharusha miguu na kichwa chake.

Alisema kwamba baada ya kuona hali hiyo ndipo yeye pamoja na ndugu zake walichukua jukumu la kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance) walilopewa na kisha kumkimbiza katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.

Hatahivyo,alisisitiza kwamba pamoja na askari hao kumtuhumu kuiba mbuzi hao lakini cha ajabu hawajamfungulia mashtaka yoyote na hata wao walipotaka kufungua mashtaka dhidi ya askari waliompiga walinyimwa .

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara,Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo alikiri kupata taarifa zake huku akisema kwa kifupi kwamba tayari ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.

“Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo”alisema na kukata simu ghafla

Hatahivyo,aliongeza kwa kusema kwamba endapo kuna askari atabainika kuhusika na tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

KINYWAJI CHA MALTIZA CHAZINDILIWA JIJINI MWANZA LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Moja kati ya mabalozi wa kinywaji cha Maltiza,Balidina Constatin (kulia) akiwaonyesha wateja kinywaji hicho kipya ambacho kinatengenezwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) ambacho hakina kilevi kwenye uzinduzi uliofanyika jana katika kiwanja cha Furahifisha jijini Mwanza.

Kundi Wasafi Classic Hatupendi dharau likikonga nyoyo za watu wakati wa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Maltiza,katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Kundi la sanaa la Africa Bamus wakiwa wamebeba mfano wa kopo za kinywaji kipya cha Maltiza wakionyesha kwa wadau waliohudhulia uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Sehemu ya wananchi waliohudhulia uzinduzi huo wakionja kwa furaha kubwa ladha ya kinywaji cha Maltiza mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ASKOFU KIKOTI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Baba Askofu William Pascal Kikoti.

Kifo cha Askofu Kikoti kilitokea jana Jumanne tarehe 28 Agosti, 2012 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mkoani Mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu.

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Baba Askofu William Pascal Kikoti wa Jimbo Katoliki la Mpanda akiwa bado na umri mdogo wa miaka 55 wakati ndiyo kwanza utumishi wake ulikuwa ukihitajika zaidi”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake na kuongeza,

“Ni dhahiri kwamba kifo cha Baba Askofu Kikoti kimeacha pengo kubwa la kiuongozi siyo tu kwa Kanisa Katoliki hapa nchini, bali pia Jumuiya ya Waamini wa Kanisa hilo kote duniani”.

Rais Kikwete amesema anatambua jitihada kubwa za Marehemu Baba Askofu William Pascal Kikoti enzi za uhai wake katika kuwatumikia Waumini wa Kanisa lake, na hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, tangu alipopata Daraja la Upadre mwaka 1988, kuteuliwa kwake kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda mwaka 2000, na hatimaye alipowekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo mwaka 2001.

“Kutokana na msiba huo mkubwa, ninakutumia wewe Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Salamu zangu za Rambirambi, na kupitia kwako kwa Kanisa Katoliki na kwa Waumini wote wa Kanisa hilo hapa nchini hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, kwa kumpoteza mmoja wa Viongozi muhimu na wa ngazi ya juu wa kiroho, Marehemu Baba Askofu William Pascal Kikoti”, ameongeza kusema Rais Kikwete.

Amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipumzishe mahala pema peponi Roho ya Marehemu. Amewahakikishia wote waliofikwa na msiba huo kuwa yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2012

WATAALAM WA AFYA KUTOKA INDIA WAITEMBELEA TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

Mshauri wa Ubalozi wa India, Kunal Roy akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya kitalii ‘’ Utalii wa Afya‘’ itakoyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 30 na 31 Augusti. Moja ya lengo ikiwa ni kujuana kwa wasomi na kuelimishana na kuboresha huduma.

Mkurugenzi wa Shirikisho Kanda ya India Chemba ya Biashara na Viwanda (FICCI), Lt. Vivek Kodikal (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ubalozi wa India uliopo jijini Dar es Salaam jana kuhusu ziara ya kitalii ‘’ Utalii wa Afya‘’ itakoyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 30 na 31 Augusti. Moja ya lengo ikiwa ni kujuana kwa wasomi na kuelimishana na kuboresha huduma.

NJAMA ZA T.I.D KUTAKA KUMUUA ALLY KIBA ZATHIBITISHWA NA...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




 TID

Jana kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.

Leo kupitia chanzo chetu, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo zilizo zagaa mtaani.

Ali Kiba

Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua Ali Kiba.

"Baada sasa ya taarifa hizo kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale anapoishi Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kupeleleza eneo lile.
Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata.

Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hilo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndio anahusika.
Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."

Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba.

Christina Aguilera: Cheki hii:- 'Your Body' Dress Doesn't Leave Much To The Imagination

Tweeted this Like this, be the first of your Friends christina aguilera your body

Christina Aguilera is perhaps not the most demure of celebrities. She's gone without pants, worn nip-slip-threatening necklines and has managed to make body con dresses her wardrobe staple -- all on national television. But, while filming her...

QUEEN ELIZABERTH AKIENDESHA RANGE "IN THE HOODIE" LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Queen Elizabeth II is cooler than any of us. She raises corgis, parachutes from planes with James Bond (sort of) and hangs out with some awesome girlfriends. Should we even keep trying?

Her Majesty took to the wheel in Balmoral over the weekend -- home of the infamous corgis vs. Princess Beatrice's terrier smackdown -- rollin' in a Range Rover on her way...

TO READ MORE CLICK HERE...

UNBELEIVABLE!!! ANGALI HUYU 86 YRS COCOOO ON BIKINI...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
duchess of alba bikini

The 86-year-old noble, who is famous for holding more titles than anyone else in the world (and for having fabulously eccentric style), hit the beach this weekend in her favorite summer style: a bikini. The Duchess of Alba and her husband, 61-year-old Alfonso Diez, have been enjoying the sun and sand in...

TO READ MORE CLICK HERE...

SUPER STAR HOLLY MADISON NI MJAMZITO...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 

Holly Madison is going to be a mom!

The former "Girls Next Door" star and Playboy Playmate tells the new Us Weekly, out now, that she is expecting her first...


CLICK HERE TO READ MORE...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat