StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 28, 2012

RICK ROSS KUTUA BONGO KUIPAMBA FIESTA!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Msanii nyota kutoka nchini Marekani,ambaye alizaliwa mnamo Januari 28 mwaka 1976 nchini Marekani,akitambulika kwa jina la kisanii kama Rick Ross,lakini jina halisi akiitwa William Leonard Roberts II,atatua nchini Tanzania hivi karibuni na kutumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la Kimataifa la Serengeti Fiesta 2012 litakalofanyika Oktoba 6 ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.

Katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa bin sawia kwa kila idara kuhusiana na tamasha hilo, waandaaji ambao ni Prime Time Promotions Ltd wakishirikiana na Clouds Media Group huku mdhamini wao mkubwa ikiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti,wameandaa shamara shamra mbalimbali za kuhakikisha tamasha hilo mpaka linafika kileleni,linaamsha na kuacha gumzo la kipekee kabisa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake, ikibidi mpaka Kigoma mwisho wa reli kwa namna moja ama nyingine.

Msanii huyo mwenye umahiri mkubwa wa kufloo awapo jukwaani mpaka sasa anatamba na nyimbo/albamu kadhaa kama vile Hold Me Back 2012 God Forgives, I Don't, Hustlin' 2006 Port of Miami Diced Pineapples 2012 God Forgives, I Don't So Sophisticated 2012 God Forgives, I Don't 911 2012 God Forgives, I Don't Stay Schemin 2012 Rich Forever Aston Martin Music.

Nyinginezo ni 2010 Teflon Don DJ Khaled 2008 Trilla Lemme See 2012 So Sophisticated Amsterdam 2012 God Forgives, I Don't Black Magic 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire The Boss 2008 Trilla You the Boss 2011 You the Boss
Touch'n You 2012 Touch'N You Bag of Money 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire.

September 27, 2012

DKT SHEIN AWAASA MASHEHE WASIJIHUSISHE NA MIGOGORO YA ARDHI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya Madiwani na Masheha wa Shehia mbali mbali za Pemba, wakiwa katika Semina ya siku tatu Kuhusu Uimarishaji uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa, iliyoanza chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika Ukumbi Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

VIONGOZI wa Serikali za Mitaa wakiwemo Masheha wametakiwa kutojihusisha na migogoro ya ardhi kwani inaathiri maendeleo ya kilimo, utalii na makaazi ya watu na wakati mwengine huathiri hata amani na usalama katika maeneo yao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa semina ya siku tatu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa, inayofanyika katika hoteli ya Misali, iliyopo Wesha Pemba. Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa semina hiyo, Dk. Shein alisema kuwa ni bahati mbaya kwamba mara nyingi Masheha na viongozi wengine wa Serikali za Mitaa ikiwemo Wizara husika, huwa wanajihushisha na migogoro hiyo.

Alisema kuwa kwa hakika migogoro hii inavuruga ustawi wa uchumi pia, kutokana na ukosefu wa maadili pamoja na kutokuzingatia sheria ziliopo kwa baadhi ya watendaji matokeo yake ni kuwanyima haki zao wananchi wanaostahiki na kupelekea kunungunika.

“Katika yatakayozungumzwa hapa ni suala la ardhi, jambo lenye kuleta utata na migogoro katika jamii Unguja na Pemba na pia ijulikane kuwa tatizo hili si la Zanzibar pekee bali ni la nchi nyingi duniani”,alisisitiza Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa katika mfumo wa utawala wan chi, viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Masheha na Madiwani wana jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba misihgi ya utawala bora inatekelezwa.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiendesha Semina ya siku tatu ya Mashehe na Madiwani wa Shehia za Pemba katika ukumbi wa Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba, (kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, (kushoto) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame na katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
“Kama nilivyosema kule Unguja, nyie hapa ndio mlioko mashinani na mti wenye shina bovu hauwezi kusimama. Kwa kuzingatia haya, tumeamua kuendesha semina hii maalum kwenu ili kukupeni na nyinyi maelekezo na fursa kamili katika kujadili utawala bora,” alisema Dk. Shein.

Dk Shein alisema kuwa Utawala Bora ni kiini cha ustawi wan chi, amani na utulivu wake na kusisitiza kuwa malengo yote ya nchi yakiwemo uchumi na huduma za jamii yanalenga katika kuleta Utawala Bora kwa wananchi.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa katika awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, suala la utawala bora lina umuhimu wa pekee. Pia, alitoa shukuran kwa UNDP kwa kufankisha semina hiyo. Pia, kwa upande wa Masheha na Madiwani wametakiwa kuwa na mashirikiano na uhusiano mkubwa katika kutunza amani na usalama ndani ya shehia zao.

Aidha wameelezwa kuwa ulinzi unaotolewa na vyombo vya dola au Polisi Jamii ambao unawapa usalama wananchi utafanikiwa tu kwa mashirikiano yao na wahusika wengine. Viongozi hao pia, wametakiwa lazima watambue kwamba utekelezaji wa mipango ya maendeleo unaofanywa na Serikali kwa kupitia kwenye Idara na Wizara zake huwa unatekelezwa katika shehia, zikiwemo upelekaji huduma za afya, elimu, maji na nyenginezo.

RAIS JK ATOA RAMBIRAMBI KIFO CHA JENERALI ANATORY KAMAZIMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es Salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano Septemba 26, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.


RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki Septemba 25, 2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nimepokea kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni pigo kubwa sana kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika salamu hizo.



Marehemu Meja Jenerali Kamazima
Mchana wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji wafiwa.
Marehemu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.

Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003. Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.

“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.

“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.
Marehemu ameacha mjane, watoto na wajukuu.

MATUKIO KATIKA PICHA YA KUAPISHWA KWA LUTENI JENERALI SAMUEL NDOMBA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dk. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Mkuu wa Jeshi la Polisi (wa pili kutoka kulia) na Paul Chagonja kamishina wa Oparesheni. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

SAKATA LA ARV BANDIA SERIKALI YABANWA-SOMA UPATE UNDANI WAKE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



Na: Ibrahim Yamola,Mwananchi

BARAZA la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA), limeitaka Serikali kuwaeleza wananchi madhara watakayoyapata baada ya kutumia dawa bandia za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV), ambazo zimesambaa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbali na hilo, wameitaka ikiri uzembe ambao umejitokeza katika utaratibu wa kuagiza, kununua, kusambaza na kuzigawa dawa hizo kwa watumiaji. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji wa NACOPHA, Deogratius Peter alisema Serikali inapaswa kutoa ufafanuzi wa kina juu ya hali ya baadaye ya watu ambao walikuwa wanatumia dawa halali kisha wakatumia bandia.

Peter alisema Serikali inawajibika kuwasaka wahusika wa kashfa hiyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria, vinginevyo watumiaji wa dawa hizo watapoteza matumaini na kuvuruga juhudi za taifa za kukabiliana na maambukizo ya Ukimwi.

“Kupitia NACOPHA tunaitaka Serikali itoe elimu na taarifa sahihi ili watumiaji wapate uwezo wa kuzitambua zipi ni dawa bandia na zipi ni halali,” alisema Peter. Alisema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo la dawa bandia, Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kwa kuanzisha utaratibu wa watumiaji wa dawa hizo kuzirejesha kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya na kutolewa kwa dawa halisi.

“Tiba hii ina kiambatanisho kimoja tu, wakati tiba kamili ina viambatanisho vitatu, hii ndiyo iliyopitishwa na Serikali itumike hapa nchini,” alisema Peter. Alisema NACOPHA inaendelea na uchunguzi ili kubaini idadi halisi ya mikoa ambako dawa hizo zilifika mbali ya Dar es Salaam, Mara na Tanga ambako Serikali ilikiri kuwa zilifika. Kauli hiyo ya NACOPHA inakuja siku chache baada ya Mkuu wa Idara ya Dawa katika Kitengo cha Ukimwi, Hospitali ya Amana, Dar es Salaam, Charles Lyimo kuitaka Serikali kujichunguza yenyewe kwa kuwa dawa hizo hazisambazwi na watu binafsi.

“Siyo rahisi kujua kwamba hii ni dawa halisi au bandia, lakini tuna uhakika na dawa tunazotumia kwa sababu zinaagizwa na Serikali peke yake. Hakuna mtu binafsi aliyepewa tenda (zabuni) ya kuziagiza. Inapeleka oda kiwandani na ndiyo inayozigawa dawa hizo na kuzisambaza kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Lakini pia dawa hizi zinatengenezwa Arusha kwenye kiwanda kilichopewa kibali na Serikali. Kama kuna dawa bandia, basi Serikali ijihoji...

Tangu sakata hili limeanza, wizara inajigongagonga tu… hawatuhusishi wala kutuuliza… na sisi tunaendelea tu kugawa dawa…” Awali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilisema haijajua kiasi halisi cha dawa hizo zilizoingia sokoni, lakini ikisisitiza kwamba athari zake ni kidogo huku Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ikibaini makopo 1,360 ambayo yako mikononi mwa wagonjwa.

TANZANIANS URGED TO USE FIRST PAN AFRICAN TOURISM CONFERENCE TO MARKET TOURISM INDUSTRY.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


The Minister for Natural Resource and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (left) and the Secretary General of the United Nations World Tourism Organization (UNWTO) Taleb Rifai at the Headquarters of UNWTO in Madrid, Spain. (Picture by Pascal Shelutete).



The Minister for Natural Resources and Tourism (second left) leading a Tanzanian delegation in a discussion with the secretariat of the UNWTO in Madrid, Spain. (Picture by Pascal Shelutete).




The Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (fourt left) with the secretariat of the UNWTO led by Secretary General Taleb Rifai (fifth left) at the UNWTO Headquarters in Madrid, Spain. (Picture by Pascal Shelutete).

The Secretary General of the United Nations World Tourism Organization Mr. Taleb Rifai has urged Tanzanians to use the first forthcoming Pan African Conference to promote tourist attractions in the country. The call was made here yesterday when he met the Tanzanian Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki.

Mr. Rifai who welcomed Ambassador Kagasheki in to the UNWTO Headquarters in Madrid said that this is the golden opportunity for Tanzanians to disclose its tourism potential to the more than 350 participants of the conference which will be held from 15th-18th October this year in Tanzania’s tourism hub, Arusha.

‘Tourism industry is the future of the economy of Tanzania and therefore opportunities like this one must be effectively used by tourism stakeholders in the country to showcase what they could offer to the world so as to increase the number of tourist arrivals in the country which is now below one million a year,` said Rifai.

He further told Ambassador Kagasheki and his delegation that tourism sector in the country should be taken seriously as the more you invest on it the more the positive impact will appear in the country’s economy. Rifai stressed that UNWTO will offer maximum support to Tanzania to ensure that it attains its goal of reaching a number of one million tourist arrivals in a short period of time and mentioned the upcoming conference as an opening of a new chapter between his body and the government of Tanzania.

On his part, Ambassador Kagasheki welcome the initiative by UNWTO to choose Tanzania as a host country of the said conference the first ever in Africa and pledged his maximum support to ensure that the conference attains its goals.

‘The Government of the United Republic of Tanzania will work hard to ensure that the conference bear fruitful results to the tourism sector in the country` committed Ambassador Kagasheki.

Ambassador Kagasheki told the UNWTO Secretariat that Tanzania has all the potentialities as far as tourist attractions is concerned and ensured the body that the government will work closely with the private sector in the country to keep the ball rolling for the betterment of the country’s economy.

Ambassador Kagasheki and his delegation made a visit to UNWTO Headquarters to discuss among other issues the preparation status of the forthcoming conference.

The First Pan African Conference with a focus on Challenges and Opportunities on Sustainable Tourism Management in African National Parks and Protected Areas to be held in Arusha in Mid October this year will look in to the balance between environmental and cultural protection and tourism development specifically on policy and management issues as well as regulatory framework in order to sustain high quality visitor experience.

This focus is a result of the fact that despite high potential for a sustainable tourism development, many of Africa’s National Parks and Protected areas suffer from constraints and limitations concerning public policies, integrated planning, effective governance with the involvement of the private stakeholders, management and commercial skills, scientific expertise, infrastructure and transport, tourism product development, quality, consumer image and safety.

Various tourism experts and conservationists both locally and internationally will get chance to deliver their experiences in the fields of tourism and conservation and make a resolution on the way forward.

TAASISI YA MAWASILIANO YA AFRIKA MASHARIKI YAFUNGUA OFISI ZAKE KIGALI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

TAASISI ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) imefungua ofisi za sekretarieti yake mjini Kigali, Rwanda ili kuratibu na kurahisisha utendaji kazi wa taasisi hiyo. Taasisi hiyo iliichagua Rwanda kuwa makao yake makuu ya kudumu karibu miezi 14 iliyopita katika mkutano wake wa 18 uliofanyika mjini Kigali, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki linaripoti.

Kufuatia uamuzi huo, ofisi hiyo iliyofunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuanza rasmi kazi zake ni inahusisha wajumbe wa bodi ya wakurugenzi tu. EACO ni taasisi ya kikanda inayoshughulika na udhibiti wa masuala ya posta, mawasiliano na utangazaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Sekretarieti hiyo itafanyakazi zake katika makao yake makuu ya muda yaliyomo ndani ya ofisi za Taifa za Mamlaka ya Mawasilino nchini Rwanda zilizopo katikati ya jiji la Kigali. Lakini mipango ipo mbioni ya kujenga ofisi zake za kudumu kwa ajili ya masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ya taasisi hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Waziri wa Masuala ya EAC wa Rwanda, Monique Mukaruliza alielezea uzinduzi huo kuwa ni hatua moja kubwa katika mwenendo mzima wa kuleta mtangamano wa jumuiya hiyo.

‘’Kila wakati tunapofanya vikao vya Baraza la Mawaziri huangalia itifaki tulizotia saini, maamuzi tuliyotoa na hujiuliza sisi wenyewe ni maendeleo gani tumeyafikia. Tuna uhakika kwamba wananchi wa Afrika Mashariki wameanza kunufaika na mtangamano tunaouzungumzia? Huu ni mfano hai kwamba wanaafrika Mashariki wanaweza kujipanga wenyewe na kufanya jambo la maana,’’ alisema.

Waziri Mkaruliza ameahidi kutoa ushirikiano unaohitajika kwa EACO ili kufanikisha malengo yake.

‘’Ndoto yetu katika mtangamano ili kupata umoja, maendeleo na ushirikiano sasa inaendelea kuwa ya kweli kupitia uzinduzi wa ofisi za sekretarieti ya EACO,’’ alisema Salvatory Nizigiyimana, Mwenyekiti wa EACO.

Nizigiyimana ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Burundi (ARCT) alielezea matumaini yake kuwa taasisi hiyo itakuwa chachu ya kuleta maendelea kwa kukuza mawasiliano katika kanda hiyo.

JULIUS MALEMA: SITISHWI NA HATUA YA MAHAKAMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Julius Malema akizungumza na wafuasi wake wanaomuunga mkono

JULIAS Malema amewaambia wafuasi wake kuwa hatishiki na uamuzi wa Mahakama kusema kuwa ana kesi ya kujibu. Mahakama nchini Afrika ya Kusini ilimwachilia kwa dhamana Malema anayekabiliwa na shtaka la kuhaulisha pesa.

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa Malema ambaye aliwahutubia wafuasi wake nje ya Mahakama, pia anatuhumiwa kwa kutumia nafasi yake ya zamani kama kiongozi wa tawi la vijana la ANC kujitajirisha yeye na washirika wake wa biashara.

Washirika wake wengine wanne nao walikabiliwa na mashtaka sawa na hiyo katika kesi yao iliyosikilizwa hapo jana. Katika hotuba yake kwa mamia ya wafuasi wake nje ya mahakama mjini Polokwane, bwana Malema alisema ataendelea na juhudi zake za kutetea maelefu wanaoishi katika umaskini nchini humo.

Seng’enge zilizungushwa katika eneo la mahakama hiyo iliyopo Polokwane, mji mkubwa wa jimbo analotokea mwanasiasa huyo, Limpopo. Wafuasi wake wanasema mashtaka hayo yameshinikizwa kisiasa.

Wakiimba na kucheza nje ya mahakama hiyo wafuasi wengi wa chama hicho cha ANC tawi la vijana walishikilia mabango yaliosema ‘Muacheni kiongozi wetu’. Maofisa wa usalaman walidhibiti ulinzi na kulikuwa na utulivu mkubwa.

Julius Malema na washirika wake wa kibiashara wanashutumiwa kwa kufaidi kutokanana na mikataba ya serikali katika jimbo la Limpopo, tuhuma ambazo anazikana. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 31 pia anachunguzwa katika kesi tofauti ya ukwepaji kulipa ushuru.

Malema ni maarufu sana Afrika Kusini kwa ukakamavu wake wa kutetea maslahi ya wananchi na maisha yake ya kifahari, huku akijitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa uchumi. Alitimuliwa kwenye chama hicho tawala mnamo mwezi Aprili akishutumiwa kwa kuzusha migawanyiko katika chama hicho.

Ni mkosoaji mkali wa a Jacob Zuma, hivi karibuni akimshutumu rais huyo kwa alivyoushughulikia mgomo wa wachimba migodi wa Marikana. Kwa mujibu wa mwandishi wa masuala ya Afrika, Andrew Harding, baadhi ya watu Afrika kusini wanaamini anafikishwa haraka mahakamani, ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake, ili kuimarisha nafasi ya kisiasa ya Zuma.

Mwandishi wetu anaeleza kwamba huenda ikawa ni kesi ya muda mrefu, ambayo huenda ikatoa nafasi ya kujulikana ukweli kuhusu suala hilo la rushwa, ambalo watu wengi wanaamini inaitia nchi hiyo doa.
-BBC

KOFFI ANNAN MEETS KIKWETE FOR AFRICAN GREEN REVOLUTION FORUM 2012 IN ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the Chairman of the Alliance for a Green Revolution in Africa(AGRA) at Ngurdoto mountain lodge yesterday evening.

The Chairman for Alliance for a Green Revolution in Africa(AGRA) Kofi Annan hands over to President Dr. Jakaya Mrisho Kiwete his autobiography titled,” Interventions, A life in war and Peace,” the book he co authored with Nader Mousavizadeh. Annan gave the President the book at Ngurdoto Mountain lodge in Arusha shortly before the opening of the African Green Revolution Forum yesterday evening. The main focus of the forum is Scaling investment and Innovation for Sustainable agricultural growth and Food Security.

MEMBE & OTHER SADC MINISTERS PREPARING FOR MEETING CONCERNING SITUATION ON EASTERN DRC IN NEW YORK

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in talks with his counterpart Minister Raymond Tshibanda of Democratic Republic of Congo yesterday at Helmsley Hotel in New York, USA prior to the SADC Ministerial Preparatory Meeting for High-Level Meeting on the situation in Eastern DRC.

Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation (2nd left) having talks with Hon. Oldemiro Balói (right), Mozambique Minister for Foreign Affairs and Cooperation and Hon. Mohlabi Kenneth Tsekoa (2nd right),Minister for Foreign Affairs and International Relations of the Kingdom of Lesotho. Left is Lieutenant-Colonel (Rtd) Tanki Mothae, Director of SADC Organ on Politics, Defence and Security.

The SADC Ministerial Preparatory Meeting for the High-Level Meeting on the situation in Eastern DRC held yesterday at Helmsley Hotel in New York, USA under the Chairmanship of Hon. Oldemiro Balói (right), Minister for Foreign Affairs and Cooperation of Mozambique.

Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation gives report on Madagascar during the SADC Ministerial Meeting. Tanzania is a Troika SADC organ Chair on Politics, Defence and Security.

Hon. Raymond Tshibanda, Minister for Foreign Affairs of Democratic Republic of Congo speaks during the SADC Ministerial Preparatory Meeting.

H.E. Ephraim Mganda Chiume, Minister for Foreign Affairs of the Republic of Malawi listens to the SADC Chair (Mozambique) during the meeting.

Hon. Bernard K. Membe (MP) in a tête-à-têtes with H.E. Jan-Paul Adam (left), Foreign Minister of the Republic of Seychelles and H.E. Arvin Boolell (center), Mauritius Minister of Foreign Affairs.
H.E. Ambassador Tuvako Manongi, Permanent Representative of the United Republic of Tanzania speaking at the SADC Ministerial Preparatory Meeting held yesterday at Helmsley Hotel in New York, USA. Listening attentively are Ambassador Liberata Mulamula (2nd right), Senior Advisor to President Kikwete (Diplomatic Affais) and Dr. Justin Seruhere (1st right), Minister Plenipotentiary at the Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations

JUMUIYA ZA UINGEREZA-TANZANIA ZASHEREKEA MIAKA 50 YA UTAIFA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mh Balozi Dr Diodorus Kamala akifanunua kuhusu maendeleo katika nchi ya Tanzania wakati wa hafla hiyo ya kusherehekea miaka 50 utaifa kati ya Tanzania na Uingereza.

Salam,

Siku ya jumanne tarehe 25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, London.

Wageni mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla hii fupi ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania. Mojawapo ya wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter Kallaghe pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL.

UTEUZI WA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamis Hubert Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania.
 Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 26, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 21 Septemba, 2012.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Septemba, 2012

September 26, 2012

HUU NDIO UJUMBE WA RIHHANA KWA CHRIS BROWN KABLA YAKUTINGA KIZIMBANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rihanna.


Kama unakumbukumbu Chris Brown alishtakiwa kwa kumpiga Rihanna mwaka 2009,na kutokana na kosa ilo alitakiwa kufanya kazi za kijamii kwa kipindi cha miezi sita.

Siku ya Jumatatu Chris alipandishwa kizimbani kutoa nyaraka za kuwa ameshamaliza adhabu aliyopewa ya kuihudumia jamii kwa kipindi cha miezi sita.




Wakati bado wengi wanajiuliza mambo aliyofanya Chris Brown kwa miaka mitatu iliyopita, but masaa machache kabla ya kuingia mahakamani, Ex- girlfriend wa Chris Brown, Rihanna alitweet directly massage kwa Chris akisema:



 

Chris akuchukua muda alijibu hivi:


 

Baada ya Chris kujibu, Rihanna alituma massage ya jumla ikisema hivi: 



Na kama tunavyokumbuka week kadhaa zilizopita Rihanna alimwambia Oprah kuwa bado anampenda Chris kupitia kipindi chake cha next chapter , na sasa yamejitokeza haya, Isn’t it time for them to just get back together?

MAGAZETI YA LEO SEPT. 26

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

MELINDA GATES NA KOFFI ANNAN NDANI YA ARUSHA LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

 

GatesMagreth Munisi
MKE wa Tajiri Mkubwa Duniani Bill Gates, na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watu maarufu watakaohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Kilimo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema mkutano huo utakaohudhuriwa na Melinda Gates ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates, utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo ambao ni Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF), utahudhuriwa pia na mawaziri wa kilimo na wakuu wa nchi nyingine za bara hili.

Ofisa Uhusiano wa AGRA Sylvia Mwichuli, alisema maandalizi yote ya mkutano huo yameshakamilika.

Watu wengine maarufu wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano pamoja na Tanzania ni  Rais wa IFAD Dk Kanayo Nwanze na  Waziri wa Kilimo wa  Nigeria  Dk  Akinwumi Adesina.

Mkutano huo ambao lengo lake ni kujadili usalama wa chakula katika bara la Afrika, utaongozwa na Rais Kikwete akishirikiana na Koffi Annan.

“Lengo ni kujadili jinsi ya kuwa na usalama wa chakula katika bara hili, katika mijadala itakayofanyika suluhisho la kuwa na usalama wa chakula litafikiwa,” alisema.

mwananchi

NAIBU WAZIRI AMFUKUZA MWALIMU WA SEKONDARI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Naibu waziri wa elimu na ufundi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilboru

Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mwalimu wa shule ya Sekondari ya vipaji Maalumu ya Ilboru Mkoani Arusha mara baada ya kukutwa akiwa amelewa wakati wa kazi shuleni hapo

Hatua hiyo imekuja mara baada ya waziri huo kufanya ziara ya kawaida shuleni hapo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi kupelekea kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kugoma kuingia darasani hivi karibuni

Majaliwa alilazimika kufanya hivyo wakati akiongea na walimu wa shule hiyo juu ya nini chanzo cha mgogoro huo,ambapo mwalimu huyo,Potin Jovita Sumawe, alinyanyuka na kuanza kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa mbele ya Waziri huyo

“Nimemuagiza afisa utumishi kumpeleka hospitalini kwaajili ya kupimwa kama anamechanganyikiwa na ripoti iliyoletwa kwangu nikuwa alikuwa amelewa hivyo tunamsimamisha kazi na kuanza kupitia faili lake tuone kama anaweza kuonyeka ama laa!”alisema Majaliwa

Aidha aliongeza kuwa watumishi wote hawatakiwi kwenda kazini wakiwa wamekunywa au wametumia kilevyi cha aina yeyote huku akisisitiza kuwa mahali pa kazi sio mahali pa kunywa pombe kwa kufanya hivyo nikuvunja sheria ya utumishi wa umma

“Kama mtumishi wa umma anavunja sheria kwa kunywa pombe kazini atachukuliwa sheria kwa kuwa hata Yule mtoto aliyekabidhiwa kumfundisha anamfundisha kwa misingi ipi?wafanye kazi kwa maadili mema”alisema Majaliwa

Aliongeza kuwa hii sio hapa tu bali sehemu yeyote mfanyakazi wa serekalini au sekta binafsi haruhusiwi kufanya kazi akiwa amelewa hivyo mtu yeyote akikutwa hivyo anastaili kufukuzwa kazi.

BIBI BOMBA AKABIDHIWA ZAWADI NA NMB

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 

Washindi wa Bibi Bomba wakiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa NMB na Clouds tv baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Clouds Media. 


Mshindi wa tatu wa kipindi kilichokuwa kinaitwa Bibi Bomba Bi. Nasra M. Abdullar (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa NMB Bi. Josephine Kulwa akishuhudia katikati ni Mratibu wa vipindi vya Clouds tv Bw. Wasiwasi Mwabulambo. 



Mshindi wa pili wa kipindi kilichokuwa kinaitwa Bibi Bomba Bi. Anna S. Indina (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa NMB Bi. Josephine Kulwa akishuhudia, katikati ni Mratibu wa vipindi Clouds tv Bw. Wasiwasi Mwabulambo. 



Mshindi wa kwanza wa Bibi Bomba Bi.Veronika Mpandala Matia akipokea mfano wa hundi baada ya kujishindia zawadi ya fedha taslim shilingi milioni 5. Akikabidhi mfano wa hundi ni Meneja Mawasiliano NMB Bi. Josephine Kulwa (kulia), katikati akishuhudia ni Bw.Wasiwasi Mwabulambo, Mratibu wa vipindi Clouds tv na Babu wa Kitaa – Mtangazaji wa kipindi cha Bibi Bomba
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat