Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MAISHA ya mwigizaji staa wa sinema za Bongo, Irene Uwoya bila kuwa na
mumewe, Hamad Ndikumana 'Katauti' yanaonekana kuwa ya aibu tupu
kufuatia siku za karibuni kubadilika tabia, hasa kwenye eneo la
kujiheshimu, Amani linashuka sasa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili siku za karibuni umegundua kuwa
mambo mengi ya aibu ambayo staa huyo anayafanya, yanasababishwa na
kutengana na mumewe ambaye kwa sasa amerudi kwao, Rwanda.
“Yaani
Uwoya sasa hivi hana tofauti na msichana ambaye hafikirii kuolewa,
amechangamka kila idara, hajali cha ndoa wala mume, anaonekana
anajipongeza kwa ndoa yake kuvunjika,” alisema rafiki wa karibu wa
Uwoya.
Tabia nyingine ambayo imegundulika kuwa staa huyo anayo kwa
sasa ni kujiachia na waume za watu pamoja na waigizaji wenzake wa kiume
huku ikidaiwa hachagui mahala popote yeye ni ‘kambi’.
“Siku hizi
Uwoya anaweza kukaa sehemu, akamuegemea mwanaume ambaye ni mume wa mtu
au akamfanyia msanii mwenzake vitendo ambavyo kwa mtu kama yeye aliye
kwenye ndoa hatakiwi kuvifanya (angalia picha ukurasa wa mbele), hata
kama ndoa yenyewe ilivunjika,” aliendelea kuanika rafiki huyo.
Akaendelea:
Lakini bwana hata hao wanaume wenyewe wangekuwa wanaangalia; ya nini
kuchezeana na msanii ambaye siku ikifika, mkatoka magazetini mnapiga
kelele kulalamika?”
Rafiki huyo akaongeza: “Mabadiliko mengine ambayo
Uwoya anaonekana kuwa nayo ni mavazi ambapo inadaiwa licha ya kuzoeleka
kwa kuvaa mavazi ya nusu utupu akiwa na mumewe lakini kwa sasa
amezidisha, anaweza kuvaa kigauni kifupi hadi akikaa nguo ya ndani
inaonekana (picha ya aina hiyo iliwahi kutoka kwenye gazeti dada na
hili, Ijumaa).
Mbali na mavazi, kujiachia na wanaume hadharani,
imebainika kuwa, kwa sasa mwigizaji huyo ndiye anayeongozwa kwa kutetwa
na marafiki zake wa karibu, wengi wakionesha kutomuunga mkono kufuatia
kitendo chake cha kukubali ndoa yake ivunjike.
Hilo lilionekana hivi
karibuni alipotinga kwenye Hotel Hyatt Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar
es Salaam ambapo staa mwenzake, Wema Sepetu alikuwa akizindua filamu ya
Superstar.
Uwoya alitinga ukumbini akiwa amevaa vazi jeusi na la
ajabu, chini alivaa soski nyeusi tu bila viatu huku kucha za vidole vya
mikononi zikiwa ndefu na kupakwa rangi nyekundu hivyo kuonekana kama mtu
wa kwenye filama za kutisha (angalia picha ukurasa wa mbele).
“Hivi Irene amevaaje leo jamani? Ina maana kutoka moyoni ameona vile ni sawa?” alisikika akihoji mmoja wa mastaa wa kike Bongo.
Hata hivyo, Uwoya alipopigiwa simu juzi, Jumanne, hakupatikana.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS