Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu Dk Hellen
Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa
amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano
wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt.
Ulimboka:Dkt.
Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya
Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka
Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja
watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao
walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea
barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na
miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda
mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa. ---
UPDATE:
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------
Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa ( tekwa) jana usiku.
Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.
Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.