StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

October 3, 2012

Ajali yagari yauwa watu Mbeya, magari yateketea kwa moto

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mdau mwenzetu kutoka Mbeye Yetu Blog,Bwa. Joseph Mwaisango ametuletea habari ya kuvunjika vunjika hivi punde kutoka mkoani Mbeya,kuwa kuna ajali mbaya imetokea muda si mrefu maeneo ya Mbalizi ambapo zaidi ya magari manne yamegongana na mawili kuteketea kwa moto na kupelekea zaidi ya watu kumi kupoteza maisha na wengine 26 kujeruhiwa  akiwemo mbunge wa viti maalum Mary Mwanjelwa baada ya lori la mafuta kungonga magari kadhaa katika eneo la Mbalizi,Wadau kwa picha zaidi ya tukio hili zima ingia http://mbeyayetu.blogspot.com/

 
Baadhi ya maiti zikiwa chini baada ya kutolewa katika magari hayo.

RUFANI YA LEMA YATIKISA ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Na: Mussa Juma, Arusha,Mwananchi.

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwahutubia wafuasi wake baada ya Jaji MKuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman kuahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.Picha Zote na Jackson Odoyo Mussa Juma, Arusha MAWAKILI wanaomtetea aliyekuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema wamedai mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa mteja wao yuko huru kwa kuwa mahakama haikutengua ubunge wake.Katika kesi hiyo, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande anawaongoza wenzake wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati na Natalia Kimaro kusikiliza maombi ya rufani hiyo, inayopinga Lema kuvuliwa ubunge.

Mawakili hao wa Lema jana walitoa hoja ya kupinga hukumu hiyo kufuatia mabishano baina yao na upande wa utetezi kwa maelezo kuwa taratibu za ufunguaji wa rufaa hiyo zimekosewa. Awali wakili Alute Mughwai aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali rufani hiyo kwa kile alichoeleza kuwa ina upungufu mwingi wa kisheria na kikanuni. Wakili huyo alitaja baadhi ya kasoro za rufani hiyo kuwa ni hati ya kukaza hukumu (tuzo) ambayo imewasilishwa mahakamani hapo kutokuwa na mhuri wa Jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa hukumu ya kesi hiyo.

Alidai kuwa katika rufani hiyo pia kuna upungufu kuhusu tarehe za kuwasilishwa kwa rufani, pia baadhi ya vifungu vimekosewa.Wakili Mughwai alitoa kumbukumbu ya kesi kadhaa ambazo mahakama ya rufani ilizitupa baada ya kukosa hadhi ya kisheria kusikilizwa.

“Mawakili wa Lema walipaswa kabla ya kuwasilisha mahakamani rufani yao, kujiridhisha kama kuna upungufu katika nyaraka ambazo wanawasilisha mahakamani.” Alisema kubwa katika makosa ambayo amebaini katika rufani hiyo ni kuwasilishwa bila kuwekwa mhuri hati ya kukaza hukumu (tuzo) iliyotolewa na Jaji aliyetoa hukumu katika kesi ya awali. “Hapa nani ambaye anajua sahihi ya Jaji? Alihoji. Hawa mawakili walipaswa kushinikiza kuwekwa mhuri wa mahakama katika hukumu hiyo ili kuthibitisha uhalali wake,” alisema Alute. Hata hiyo, wakili huyo alisema badala yake, mawakili hao waliwasilisha mahakamani rufani hiyo ndani ya siku 29 tu baada ya hukumu, badala ya siku 60 ambazo walipewa.

“Kwa kuwasilisha mahakama ya rufani, hukumu ambayo bado haina mhuri wa Jaji ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mahakama.” Mughwai alidai kuwa katika mazingira ya sasa hakuna cha kurekebishwa katika rufani hiyo, badala yake itupwe na kuwataka wakata rufani kulipa gharama zote za kesi. Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na mawakili wa Lema ambao ni Tundu Lissu na Method Kimomogoro, ambao walidai kuwa hawakuwa na mamlaka ya kumlazimisha Jaji Rwakibarila kuweka mhuri.

Lissu alidai "Kama inaonekana sasa kuwa ni batili, basi hata uamuzi wa kumvua ubunge Lema ni batili," alisema. Wakili Kimomogoro Kwa upande wake, Wakili Kimomogoro alisema kisheria kasoro hizo ya mhuri wa mahakama na tarehe, haziwezi kusababisha rufani hiyo kutupwa kwani haziathiri madai ya msingi katika rufani.

Alidai kesi hiyo ya Lema ilikuwa ya kipekee kwani mara tu baada ya hukumu kutolewa faili lilipelekwa jijini Dar es Salaam na maombi ya nyaraka kadhaa za kesi hiyo yalitumwa kutoka Dar es Salaam. “Katika mazingira kama haya hatuwezi kuepuka makosa ya kibinadamu ambayo yanatambulika kisheria,” alidai Kimomogoro. Aliongeza kuwa katika hoja hiyo, waliandika kifugu namba 114 badala ya 113 kimakosa ya kiuchapaji, lakini hakipotoshi kitu chochote kwani kifungu hicho hakipo. Wakili Kimomogoro alisema wakili mwenzake, Mughwai ameshindwa kuzungumzia uamuzi ya kesi ambazo, hazikufutwa kutokana na kuwa na upungufu mdogo wa aina hiyo ambao kimsingi hauathiri rufani.

Hata hivyo, alisema kama wakili huyo alibaini makosa hayo, katika uwasilishaji wa hoja zake, alipaswa pia kurekebisha kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2009 ya mahakama. Kimomogoro pia aliwasilisha mahakamani hoja kadhaa za kisheria na uamuzi ya Mahakama ya Rufani za ndani na nje ya nchi, ambazo hazikutupilia mbali rufani ambazo zilikuwa na upungufu mdogo, kwani lengo la mahakama hizo ni kutafuta haki.

“Siyo kila kasoro au usumbufu kwenye hukumu unaweza kusababisha kutupwa rufani kwani kasoro zote zilizotajwa ni za makosa na uchapaji na nyingine ni za kiutaratibu tu,” alisema. Alifafanua kuwa makosa ambayo yanaweza kusababisha rufani kutupwa ni kama aina namba ya kesi, majina na wadhifa wa wadau katika shauri husika, mambo yanayolalamikiwa na mahakama imeamua nini.

Wakili huyo alifafanua kuwa jambo la kukosekana mhuri wa mahakama wa Jaji siyo kubwa na kusababisha kutupwa rufani kwani hakuna ambaye anapinga hukumu iliyowasilishwa mahakamani. Kwa upande wake, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Vitalis Timoth alisema anaunga mkono hoja za mawakili wa Lema, kuwa pingamizi ya wakili Mughwai haina msingi wa kisheria.

Alisema hati ya kukaza hukumu (Tuzo) inatolewa chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na siyo chini ya sheria ya masijala za mahakama. Alisema siyo kazi ya jaji aliyetoa hukumu, kuweka mhuri hukumu yake bali hiyo ni kazi ya msajili wa mahakama na masijala za mahakama.

“Kama hati ya kukaza hukumu ina matatizo anayepaswa kulaumiwa siyo mawakili bali ni mahakama ambayo ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuweka mhuri,” alisema. Alidai kuwa pingamizi ya awali ya rufani inapaswa kuwa na sifa mbili, kwanza iwe na suala la kisheria na pili iendane na kesi ya msingi. “Katika hoja za wakili Mughwai ni wazi inathibitika pingamizi hili halina matakwa ya kisheria kwani hata kama ikipitwa siyo kuwa itazuia kurejeshwa tena na kusikilizwa kwa rufani ya msingi.” Alidai ni busara kuacha kuwa na pingamizi ambazo zinaongeza gharama za kesi na muda wa kusikiliza.

“Ushauri wangu kila shauri liamuliwe kwa mazingira yake na uamuzi wa sasa uzingatie mahakama katika kutenda haki,” aliongeza. Alidai kwamba kutupwa kwa hoja ya kutaka waomba rufani wachapwe mijeledi kwani kazi ya mahakama siyo kuchapa watu bali ni kutoa haki. “Tunashauri kusikilizwa rufani kwa kuzingatia sheria na ushahidi,” alisema. Jopo la Majaji Baada ya kutolewa kwa hoja za pande zote za mawakili, Jaji Chande na Jaji Massati waliwauliza maswali kadhaa mawakili hao na kujieleza na baadaye Jaji Chande alitangaza kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi hapo itakapotangazwa. Jaji Chande alisema vikao vya Mahakama ya Rufani Kanda ya Arusha vimemalizika jana, hivyo uamuzi wa kutupwa kwa pingamizi la rufani hiyo au la utatolewa siku itakayopangwa na mahakama.

Baada ya uamuzi huo umati wa wafuasi wa Chadema, uliokuwa ndani na nje ya mahakama ulianza kuimba nyimbo mbalimbali kama vile Lema Jembe na bila Lema patachimbika. Katika hatua ya kuepuka vurugu, Lema alizungumza na wafuasi hao nje ya mahakama na kuwataka kuondoka kwa amani kwenda katika ofisi ya Chadema iliyopo Ngarenaro kwa amani bila vurugu.

Warufaniwa katika kesi hiyo ni makada wa CCM, Happy Kivuyo, Mussa Mkanga na Agnes Mollel ambao walishinda kesi ambayo hukumu yake ilimvua ubunge Lema Aprili 4, mwaka huu.

October 2, 2012

Watoto Wa Wassira Kujiunga CHADEMA; Ufafanuzi

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU

Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1). Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Lilian Wasira 0719 604156 Esther Wasira 0655 048797

MAGAZETI YA LEO OCT. 02

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

.



.

.





.

.

.

.

.



.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

RIPOTI YA MAUAJI YA MWANGOSI KUWEKWA HADHARANI HIVI PUNDE, PATA HABARI KAMILI HAPA!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mwakilishi wa kituo cha televisheni ya Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi, uliofanywa na timu ya waandishi wa habari watatu kutoka Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), itawekwa hadharani Oktoba 9, mwaka huu.

Azma hiyo ilitangazwa jana Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, baada ya timu hiyo kukamilisha uchunguzi wake hivi karibuni.

Mukajanga alitangaza azma hiyo alipotakiwa na NIPASHE kueleza lini ripoti hiyo itatangazwa.

Akijibu swali hilo kwa njia ya maandishi, Mukajanga alisema kwa kifupi: “Jumanne Oktoba 9, 2012 Inshallah.”

Awali, NIPASHE ilizungumza na Katibu Mtendaji wa TEF, Neville Meena, ambaye alisema uchunguzi wa timu hiyo umeshakamilika na kwamba, ripoti yake imekabidhiwa kwa Bodi ya MCT.

Timu ya waandishi hao iliyoundwa Septemba 4, mwaka huu, iliongozwa na Meneja wa Utafiti na Machapisho wa MCT, John Mirenyi, wajumbe wakiwa ni Mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti la Mwananchi, Hawra Shamte na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Simon Berege.

Timu hiyo ilipewa siku nane na ilianza kazi yake Septemba 6, mwaka huu, kubaini ukweli wa tukio hilo na kuweka kumbukumbu sahihi ya tukio hilo.

Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, alikataa kuzungumzia timu ya jeshi hilo iliyoongozwa na Mkuu wake, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, umekwisha au nini kinaendelea, akisema hawaruhusiwi kufanya hivyo kwa kuwa liko mahakamani kisheria.

“…Waziri wa Mambo ya Ndani alishalisemea,” alisema Senso.

Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu lililosambaratisha mwili wake wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 3, mwaka huu.

Tayari askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mwenye namba G2573, Pasificus Cleophace Simon (23), amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.

HABARI KWA HISANI YA NIPASHE

SHIRIKIANA NA LIONS CLUB KUSAIDIA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Taasisi ya Lions Club ya jijini Dar es Salaam inaendesha zoezi la kukusanya michango ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wasio na uwezo wenye matatizo ya moyo kupata matibabu. Unaweza kutoa mchango wako hata kwa njia ya hundi kuiongezea nguvu Lions Club. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Rais wa Lions Club Nimira Gangji kwa nambari +255715979966.

HII NDIO MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.

Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.

Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.

Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.

Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).

Na Father Kidevu Blog, Zanzibar
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.

Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.

Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

October 1, 2012

Membe Praises Tanzania On MDG'S

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Tanzania Government has said it has made progress in the achievement of the Millennium Development Goals (MDG) whereby it attained goal two that of universal primary education. This was said recently by the Tanzania Minister for Foreign Affair and International Co – operation Bernard Membe (MP) when he was giving his statement to the 67th Session of the United Nation Assembly held in New York. Membe said Tanzania has registered considerable gains on goal three which is promoting gender equality and empowerment of women and goal six of combating HIV/AIDS, Malaria and other diseases. “We have also achieved moderate results on other goals, however much remains to be done to emancipate our people from poverty traps,” he said. The goals to achieve better livelihood for Africa must go far beyond 2015, thus it is necessary to consider the post MDGs agenda, one that complements instead of diverting the whole focus from the current MDGs. Membe insisted that it is not worth it to divert the attention from these goals when most developing countries, especially in Sub – Saharan Africa are unlike to achieve them by 2015. “It is equally important that the development needs of our people should feature prominently in all post MDGs consultations and decisions undertaken in various multilateral fora”, he noted. The time is right to discuss the future of MDGs and consider the proposed sustainable development goals in the light of the MDGs targets. At the 67th Session of the United Nation General Assembly, Bernard Membe addressed a wide range of topics including multilateral development Agenda, Sustainable development, United National Reforms and Unilateral Sanctions and embargos.

HAYA NDIO ALIYENENA BABA MZAZI WA MSANII LINAH KUHUSU MWANAE NA KAZI YAKE YA MUZIKI...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


. Mwimbaji Linah ambae juzi alitangaza kwamba ameamua kuwazawadia wazazi wake nyumba aliyoijenga Mpiji Mbezi Dar es salaam kwa thamani ya milioni 30 za kitanzania, amesema pamoja na wazazi wake kufahamu kwamba matunda hayo yametokana na muziki peke yake, amekubali kwamba baba yake mzazi mpaka sasa bado hakubaliani na mavazi anayoyavaa Linah.

Namkariri Linah akisema “nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe litakapotokea tatizo lolote itakua ni bahati mbaya tu lakini sio kwa makusudi, baba anaona pia kwenye magazeti huwa navaa hivi najitahidi kumwambia hivyo ni vitu vya bahati mbaya huwa vinatokea na mimi kama msanii ndio maana tunakula tunaishi lakini ndio kazi”

Kwenye line nyingine Linah kasema “nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na yeye ni mavazi, kuna show na show.. siwezi kwenda kufanya show ufukweni alafu nimevaa magauni, show nyingine tunatakiwa kubang siwezi kuvaa migauni kama niko kanisani”

BURIANI JENERALI ANATOLY KAMAZIMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Edward Hosea akitoa za mwisho kwa mwili wa mtangulizi wake Meja Jenerali Mstaafu Anatory Kamazima, wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika nyumbani kwake Tegeta Dar es Salaam jana. Kamazima alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza TAKUKURU alifariki dunia mwanzoni mwa wiki katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Bugashani, Maruku, Mkoani Kagera LEO.

KARIBUNI CHADEMA...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, akiwakabidhi kadi ya uwanachama wa chama hicho kwa Lilian Wassira na ndugu yake Esther, baada kujiunga na chama hicho. Lilian na Esther ni watoto wa George Wassira Kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wassira.

SEKTA YA RELI KUFUFUKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Rais Jakaya Kikwete, akionesha njia za reli katika ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC), uliomtembelea Ikulu, Dar es salaam jana, kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli nchini. Picha na Ikulu

Wakulima wampa Zawadi Rais Kikwete

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mkulima wa mpunga katika kijiji cha Usa River,Mkoani Arusha Bwana Vincent Urassa akimpa zawadi Rais Dkt.Jakaya Kikwete kwa niaba ya wakulima wa Tanzania kwa kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini kwa manufaa ya wananchi.Bwana Urassa alikabidhi zawadi hiyo mwishoni mwa mkutano wa African Green Revolution Forum 2012 uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge mjni Arusha

MAONYESHO YA ASALI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Maandalizi ya MAONYESHO YA ASALI YA DAR ES SALAAM (DAR ES SALAAM HONEY  EXHIBITION) ambayo yatafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Dar es Salaam tangu tarehe  3 hadi 7 Oktoba 2012 yamekamilika. Wananchi wanakaribishwa kuhudhuria maonyesho hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio. Katika maonyesho hayo watu wataelimika kuhusu manufaa yatokanayo na asali, pia watapata utaalam wa kufuga nyuki na wataonja na kununua asali bora kwa bei nafuu.
Kaulimbiu ya maonyesho hayo ambayo ni ya kitaifa ni ASALI KWA AFYA NA USTAWI (HONEY FOR HEALTH AND PROSPERITY). Maonyesho hayo yameandaliwa  kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  na wadau wengine wa Sekta ya Ufugaji Nyuki. Lengo kuu la maonesho ni kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki.
Tarehe 3 Oktoba ni siku iliyotengwa maalum kwa ajili ya kufanyika Kongamano la Ufugaji Nyuki. Hivyo wafugaji nyuki, wataalam na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wanakaribishwa kuhudhuria kungamano hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa J. M. Kikwete ulioko kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere .
Ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo utafanyika tarehe 5 Oktoba 2012  ambapo Mgeni Rasmi anategemewa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb).
Waonyeshaji waliothibitisha kushiriki ni Halmashauri za Wilaya zote, kampuni zinazonunua asali, watengenezaji wa mizinga na vifaa vingine vya kisasa  vya ufugaji nyuki, na watengenezaji wa bidhaa zinaotumia asali na nta kama malighafi.
Inategemewa kuwa katika maonyesho hayo waonyeshaji watajitangaza ili waweze kupata wanunuzi wa asali na mazao mengine ya nyuki. Pia wanunuzi wa mazao ya nyuki watapata fursa ya kuwafahamu wafugaji. Aidha inategemewa kuwa utaundwa mtandao ambao utawaunganisha wazalishaji, wafanyabiashara, wataalam na wadau wa sekta ya nyuki.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
30 Septemba 2012
                                                   Simu: +255 784 468047

USAFIRI WA TRENI YA TAZARA ITAKAYOTUMIKA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jna mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.


Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.


Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat