StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 13, 2012

AJALI ZA UZEMBE NA KUTOZINGATIA UMAKINI BARABARANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Daily Gifdump

HEBU ONA JINSI WANAVYOTENGEZA MUVI ZA "ALIPOKUWA MDOGO" NA "BAADAYE AKIWA MTU MZIMA"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

2

3

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

WAFANYAKAZI WA UJENZI WA BARABARA YA ARUSHA MINJINGU WAGOMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Sogea Satom ya nchini Ufaransa inayojenga barabara kati ya Arusha - Minjingu, mkoani Manyara wakiwa nje ya lango la Ofisi eneo la Kisongo, wilayani Arumeru mkoani Arusha jana,baada ya kugoma wakidai kupunjwa malipo na kufanya kazi zaidi ya muda wa kazi.SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Minjingu, mkoani Manyara, wakati akiwa katika ziara yake katika mikoa ya kanda ya Kaskazini, jana wafanyakazi wa Kampuni ya Sogea Satom inayokarabati barabara hiyo waligoma kufanya kazi.


Wafanyakazi hao badala ya kwenda kwenye eneo la Nanja ambako kazi za ujenzi zinaendelea, waliamua kwenda zilipo ofisi za utawala eneo la Kisongo na kushinikiza walipwe stahili zao.


Mara baada ya uongozikubaini mgomo huo,Kampuni binafsi ya ulinzi ya KK Security iliongeza magari ili kuimarisha ulinzi eneo hilo.
Wafanyakazi walisema wanadai kupunjwa malipo yao kwa wasaidizi kutoka Sh7000 hadi 5000 huku wakifanya kazi saa 10 kwa siku badala ya saa 8 walizokubaliana na wakitakiwa kufanyakazi siku za Jumamosi na Jumapili bila malipo ya ziada.


“Hatuwezi kufanyakazi katika mazingira ya namna hii,huu ni unyanyasaji wa hali juu,Rais Kikwete alizindua barabara hii lakini hata wiki mbili hazijaisha tunanyanyaswa,”alisema Omary Athuman.


Mbali na kufanyakazi zaidi ya muda waliokubalina pia wanataka wapate ajira ya kudumu kwa maelezo kwamba wameshamaliza muda wa miezi mitatu kisheria wa kuwa vibarua.

Naye Innocent Bureta alidai Serikali na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayowahudumia imekuwa kimya kuwaambia hatma ya madai yao wakati wao wanafanya kazi ngumu bila kupewa malipo ya muda wa ziada.


Wakati wafanyakazi hao wakizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Sakita Lekibelie alijaribu kuwazuia waandishi wa habari kufanyakazi zao hatua iliyopingwa na wafanyakazi na kuamua kurudi ofisini.


Jitihada za kuupata uongozi kuzungumzia madai ya wafanyakazi hazikufanikiwa baada ya Ofisa uhusiano kudai anayeweza kuzungumzia jambo hilo ni meneja mradi ambaye hata hivyo hakuweza kupatikana kutokana na vikao vya dharura vilivyoitishwa.

Ukarabati wa barabara hiyo yenye kilometa 98 unagharamiwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya Sh75 bilioni.

MWANAFUNZI WA MUCCOBS AJIUA KWA KITANZI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara cha Moshi (Muccobs), mkoani Kilimanjaro, amejiua kwa kujinyonga.

Mwanafunzi huyo, Samson Bena (24), alijinyonga usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, alilithibitishia gazeti hili jana kuhusu tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu ulikutwa ikining’inia juu ya mti katika Kijiji cha Uru Timbirini, Moshi Vijijini.

Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, polisi wameanzisha uchunguzi wa kubaini kiini cha kijana huyo kujinyonga.

Wakati wa uhai wake, kijana huyo alikuwa anasomea shahada ya sanaa katika Menejimenti ya Taasisi ndogo za fedha.

Habari zilisema wananchi wa eneo la mwisho wa lami katika Kijiji cha Uru Timbirini, ndio waliougundua mwili wa mwanafunzi huyo ukining’inia juu ya mti.

Baadaye walitoa taarifa polisi na kufuatiwa na hatua ya askari kwenda katika eneo la tukio na kuushusha mwili na kisha kuupeleka chuoni ambako wanafunzi walimtambua mwanafunzi mwenzao.

Habari zilisema baadaye, mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Mawenzi, ambako umehifadhiwa ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Hili ni tukio la pili kwa mwanafunzi wa Muccobs, kukutwa akiwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha.

Oktoba mwaka juzi, mwanafunzi Lucy Genge (20) aliuawa kikatili baada ya kubakwa na kundi la watu wasiojulikana.

Maiti yake ilitupwa kwenye kichaka kidogo kilichokuwa umbali wa meta 100 kutoka katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa Kilimanjaro na kugunduliwa na wapita njia saa 6:00 mchana.

Marehemu ndio kwanza alikuwa amemaliza kozi ya cheti katika fani ya Utawala na Uhasibu.

ADHA YA USAFIRI NA KUGOMBANIA SITI HUPELEKEA WATU KUTUMIA NJIA MBADALA KAMA HII...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

HII NDIO AJALI ILIYOUA WATU SITA MBEYA JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends






Wakazi wa eneo la Itewe kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijni wakiangalia gari la abiria aina ya Hiace ilivyoharibika baada ya kugongana na lori jana, ambapo katika ajali hiyo abiria sita wanasadikiwa kufariki dunia.





STAY TUNED..

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

ARE YOU READY TO LAUGH, LEARN AND HAVE FUN BY JUST SITTING ON YOUR SOFA??

...THE HOT CORNER ON THE SPORAH SHOW COMING UP SOON 

The Launch is on 10th December 2012 , SKY channel 182 at 10:30pm in The United Kingdom.
Tanzania Coming up soon in January. 

see: youtube.com/watch?v=nqv3WL4spBo

STAY TUNED.



HUYU NDIYE MKURUGENZI MKUU WA BBC ALIYEJIUZULU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa BBC, George Entwistle

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Habari, BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo. George Entwistle amejiuzulu kama Mkurugenzi BBC kwa kile kufanyika makosa katika moja ya vipindi vya shirika hilo la habari Ulimwenguni. Taarifa zaidi zinasema Entwistle amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.

Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative, Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto. Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.

Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchunguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile. Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi, usiku Entwistle alisema; “ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya”.

Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema; “huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma”. “Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika”

“Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amediriki kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika – uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi”.

Askari Polisi 40 Wauawa na Wezi wa Mifugo Kenya

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Kundi la ng’ombe

INAKADIRIWA kuwa askari polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika shambulizi lililofanywa dhidi yao walipokuwa wanajaribu kuokoa mifugo waliokuwa wameibwa.

Taarifa zaidi zinasema maofisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, Kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi. Msemaji wa polisi amesema kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliaji watatu, lakini viongozi wa kijiji wanatofautiana kwa kusema kuwa huenda maiti zaidi wa tukio hilo wakapatikana.

Hata hivyo jana miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi waliouawa kuwa 40. Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho ya mifugo wao Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.

Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake. Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili, inaarifiwa kuwa wakaguzi wawili wakuu wa polisi hawajulikani waliko.

Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini. Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki mbili zilizopita hadi 43.

Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa mishahara.

DIAMOND THE PLATNUM ;ANGALIA PICHA NAMNA DIAMOND THE PLATNUM ALIVYOPATA AJALI!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Juzi Diamond akiwa na gari lake alipata ajali (ya kawaida) ambayo ilisababisha sehemu ya mbele kuharibika. Kwa mujibu wa meneja wake, Raqey Mohamed wa I-View Media ajali
hiyo ilisababishwa na mwendesha pikipiki ambapo hata hivyo amesema hakuna aliyeumia. “There is nothing serious lakini,”

November 12, 2012

HUYU NDIYE MWENYEKITI WA KIJIJI ANAYETUHUMIWA KWA KUUZA ARDHI YA KIJIJI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya picha zinazoonyesha matukio ya mwenyekiti wa kijiji cha losirwa ,George Arpakwa (kulia) akimkwida kiongozi wa kimila akimtuhumu kwamba yeye nimoja ya watu waliohusika kuwaita waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara kijiji hapo juzi.





MWENYEKITI wa kijiji cha Losirwa kata ya Esilalei wilayani Monduli bwana George Arpakwa ametuhumiwa na wananchi wake kujihusisha na ufisadi wa uuzaji wa ardhi kiholela ya kijiji swala ambalo linakwamisha shughuli za kifugaji kijiji hapo.


Wananchi wa kijiji hicho wakizungumza kwa masikitiko makubwa katika mkutano wa hadhara kijiji hapo wamedai kuwa wamechoshwa na uongozi wa mwenyekiti huo kushindwa kuonyesha uwadilifu wake kwa jamiii badala yake kuuza ardhi ya kijiji kinyume na sheria.


Mwenyekiti wa kijiji hicho ambae anatuhumiwa kujihusisha na kuuza ardhi ya kijiji baada ya kubaini kuwepo kwa waandishi wa habari eneo hilo alichukua jukumu la kuvunja mkutano na kuleta vujo kwa baadhi ya viongozi wa kimila akidai kua waandishi wa habari hawaruhusiwi kuhudhuria mkutano huo huko akitokomea pasipo julikana.


Aidha Romeni ole Meiya akiwa mmoja wa kijiji hicho alisema kua alishangazwa sana kuona baadhi ya maeneo ya malisho ya mifugo na mapito ya mifugo sambamba na mabwawa kuwekewa uzio kuashiria kua mifugo hairuhusiwi kuingia eneo hilo licha ya maeneo hayo yakiwa yametengwa kwaajili ya mifugo.


Alisema hawana imani tena na mwenyekiti huyo wa kijiji ambae sasa ameonyesha udhaifu wake katika utendaji wake wa kazi hivyo wanamtaka achie ngazi na kwasasa hawamtambui kama yeye nikiongozi wa jamii hiyo ya kifugaji kwa kujihusisha na kuuza ardhi ya wafugaji kinuyme na sheria za kijiji husika.


Nae Kiteho Richard alisema kunaashiria kijiji hicho kuwepo kwa ufisadi mkubwa wa ardhi huku akihoji kwanini mwenyekiti alipobaini kuwepo kwa waandishi wa habari eneo hilo kutokomea pasipojulikana huku akijua waandishi ni watu wa amani siku zote.


"Kama mwenyekiti hahusiki na kuuza maeneo ya wananchi kwanini amekimbia mkutano hii inaonyesha kua anahusika kwa asilimia kubwa ndio mana alipowaona waandishi wa habari akakimbia akijua siri inafichuka" Alisema Richard"


Wananchi hao waliandamana hadi ofisi ya mwenyekiti huo nakuchukua jukumu kali lakutaka kuifunga ofisi hiyo wakiamini kua ninjia moja wapo ya kupata suluhisho la Ardhi yao kumilikiwa na wenye pesa wachache huku wakiomba serikali kushughulikia tatizo hilo likiwa bado halijaleta hadhari kubwa kwa jamii.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Monduli bwana Jowika Kasunga akizungumza kwa njia ya simu amekiri kupokea taarifa hizo za malalamiko ya wananchi nakuahidi kuwa anazifanyia kazi ilikubaini ukweli wa jambo hilo.

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

MTOTO ANETH AKIWA AMEOKOLEWA NA WASAMARIA WEMA HUKO MAJENGO


HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO


HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH




HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE


MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI


WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI




MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.

Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.

Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .

Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.

Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.

Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.

MWE MWE MWEEE...USICHEZEE PESA YANGU KIJANA....!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

JAMAA KAZIMWA MIA YAKE YA EMBE AAMUA KUANZISHA NGUMI YAANI SASA MAEMBE YOTE YAMETAWANYIKA NA NGUMI ZINAENDELEA


KUSAIDIANA IPO JAMAA MWINGINE AINGILIA UGOMVI KAZI IPO HAYA NDIYO MAISHA YA BAADHI YA VIJANA HUKO MANOW RUNGWE

PRECISION AIR BECOMES FIRST AIRLINE TO OPERATE ATR 42-600 AIRCRAFT GLOBALLY

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

The Precision Air Tanzania Chief Executive Officer Alfonse Kioko (left) receives keys for the company’s newly acquired ATR 42-600 aircraft from the ATR CEO Filippo Bagnato(right) during the official delivery of the aircraft at the ATR Delivery Center in Toulouse, France at the weekend.

The ATR CEO Filippo Bagnato (left) shows the Precision Air Tanzania Chief Executive Officer Alfonse Kioko (right) the interior décor of the new ATR 42-600 aircraft purchased by his company during the official delivery of the aircraft at the ATR Delivery Center in Toulouse, France at the weekend

The Precision Air Tanzania Chief Executive Officer Alfonse Kioko (left) receives a present from the ATR CEO Filippo Bagnato(right) that portrays the company’s newly acquired ATR 42-600 aircraft during the official delivery of the aircraft at the ATR Delivery Center in Toulouse, France at the weekend.

Precision Air Tanzania and ATR staff pose for a group photo in front of Precision Air’s new ATR 42-600 during the official delivery of the aircraft at the ATR Delivery Center in Toulouse, France at the weekend.

MIKOPO YA MWEI KUTOKA VODACOM...

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Buigiri wapata awamu ya pili ya mikopo ya MWEI kutoka Vodacom






POLISI: USALAMA BARABARANI YAKUSANYA BILLION 11 NDANI YA MIEZI 8

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Jeshi la Polisi kitengo la Usalama Barabarani nchini, kimekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 11 katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu kutokana na makosa 388,700 yaliyofanywa na madereva wa magari.

Akizungumza na NIPASHE juzi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Mohamed Mpinga, alisema kiasi hicho kimetokana na kutozwa faini kwa madereva waliopatikana na hatia ya uendeshaji wa uzembe, ubovu wa magari pamoja na makosa mengine.

“Tumekusanya sh.11,975,008,000 kwa kipindi cha miezi tisa tu mwaka huu, hiyo inaonyesha ni jinsi gani madereva wengi wasivyozingatia usalama wa barabara na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine,” alisema SACP Mpinga.

Kamanda Mpinga alisema kiasi hicho ni tofauti ukilinganisha na faini iliyopatikana mwaka uliopita ya zaidi ya sh. bilioni tisa kutokana na makosa 369,800 yaliyofanywa na madereva kwa kutozingatia sheria za barabarani.

Alisema makusanyo ya faini ya mwaka jana yalikuwa sh.9,029,540,000.

Hata hivyo, Kamanda Mpinga alisema makusanyo hayo ni pesa zinazoingia katika mfuko wa serikali, huku akiwasisitizia madereva na wamiliki wa magari kuzingatia ubora wa magari yao pamoja na kuendesha kwa kufuata sheria za usalama barabarani.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mpinga aliwashauri madereva wanaokamatwa na kutozwa faini kutokana na makosa mbalimbali barabarani, iwapo wataamini hawajatendewa haki waende kutoa taarifa kwa Afisa wa Usalama Barabarani wa Mkoa (RTO) ili walalamike huko kuliko kunung’unika… kwani vitabu vya malipo ya adhabu ni vile viliyotangazwa na gazeti la serikali no.257 ya Agosti 2011 na si vinginevyo, alisema.

Pia Kamanda Mpinga alisema vitabu vya adhabu, haviruhusiwi kushikwa na askari ambaye hana cheo zaidi ya mwenye cheo cha koplo na sajenti, hivyo kuwaandikia makosa madereva wakati askari hana cheo ni kosa.

SACP Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kimeanzisha utaratibu wa kupokea faini papo kwa hapo kutokana na madereva wengi kutokuwa waaminifu pale wanapokutwa na makosa na kisha kuachiwa ili wapelekee baadaye kulipa.

November 10, 2012

SIJAKUBALIANA NA MAAMUZI YA SPIKA-JOHN MNYIKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Ikiwa ulipata fursa ya kusikiliza (audio na text ya RIPOTI NZIMA, bofya hapa) Spika alipomaliza kusoma ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mhe. Ngwilizi kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, utakuwa ulimsikia Mhe. John Mnyika akitaka kuzungumza lakini hakupata fursa hiyo.

Baadaye kwenye ukurasa wake wa facebook na twitter, Mnyika aliandika hivi:
Picture
Taarifa ya John Nditi, Morogoro via HabariLeo --

BAADHI ya wastaafu wa utumishi wa umma na sekta binafsi wanadaiwa kufariki Dunia mapema pale wanapostaafu kwa sababu mbalimbali ikiwa ya kuishiwa fedha za kiinua mgongo baada ya ajira zao kukoma.

Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA), umebainisha hayo katika utafiti wake uliofanyika hivi karibuni.

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kupitia Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) imeanza kuwajengea uwezo watumishi wanaokaribia kustaafu kwa kuwapatia mafunzo na mbinu mbalimbali za kufanya shughuli za ujasiliamali. Lengo ni kuwawezesha wakabiliane na changamoto za maisha baada ya ajira zao kutoka kwenye utumishi wa umma utakapokoma.

Mratibu wa Mafunzo kupitia Wakala huo, Anslim Namala, alisema hayo juzi wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka Mashirika ya Umma, Serikali kuu na Taasisi binafsi nchini.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo, hali hiyo inatokana na wastaafu hao kukata tamaa na maisha kutokana na mtazamo hasi, kuwa kustaafu ni kikomo cha maisha.

Hata hivyo alisema, katika utafiti uliofanywa na kabla ya kuanzisha mafunzo hayo imebainika wastaafu wengi walikuwa wakipoteza maisha yao kutokana na hofu ya kushindwa kumudu maisha.
UPDATES from CNN blog

[Updated at 4:52 p.m.] Acting CIA Director Michael Morrell will testify next week before the Senate Intelligence Committee about the fatal attack in Benghazi instead of David Petraeus, according to the office of that committee's chairwoman, Sen. Dianne Feinstein.

[Updated at 4:25 p.m.] U.S. Sen. John McCain extolled Petraeus as one of "America's greatest military heroes," expressing his gratitude for his "decades of work on behalf of our nation, our military and our security." McCain, an Arizona Republican and the ranking member of the Senate Armed Services Committee, added, "His inspirational leadership and his genius were directly responsible - after years of failure - for the success of the surge in Iraq."

[Updated at 3:59 p.m.] Sen. Dianne Feinstein, the head of the Senate Intelligence Committee, said, "I wish President Obama had not accepted this resignation, but I understand and respect the decision."

The California Democrat praised Petraeus for giving the CIA "leadership, stature, prestige and credibility both at home and abroad," calling him reliably in "command of intelligence issues" and "especially cooperative with Congress."

[Updated at 3:53 p.m.] The chairman of the House Homeland Security Committee praised outgoing CIA Director David Petraeus, saying, "I regret his resignation and wish him and his family the very best."

"Gen. Petraeus is one of America's most outstanding and distinguished military leaders and a true American patriot," said Rep. Peter King, a Republican from New York.

[Updated at 3:41 p.m.] David Petraeus met with President Barack Obama on Thursday, at which time the then CIA director offered his resignation, a senior administration official said. The president then formally accepted Petraeus' resignation in a phone call Friday afternoon, according to the same official.

[Updated at 3:38 p.m.] President Obama said, in a statement, that today he accepted Petraeus' resignation as CIA director.

The president added he is "completely confident that the CIA will continue to thrive and carry out its essential mission," now under the leadership of Acting Director Michael Morrell.

Obama lauded Petraeus for his "extraordinary service to the United States for decades," calling him "one of the outstanding general officers of his generation" and praising his work as CIA director.

The president concluded by saying, "Going forward, my thoughts and prayers are with Dave and Holly Petraeus, who has done so much to help military families through her own work. I wish them the very best in this difficult time." Holly Petraeus led the Consumer Financial Protection Bureau’s Office for Servicemembers Affairs.

[Updated at 3:17 p.m.] Shortly before Petraeus' resignation was announced, White House press secretary Jay Carney told reporters that "the president thinks Gen. Petraeus has done an excellent job."

When asked about the general's job status, Carney reiterated that President Obama approves of the job done by the CIA director while adding, "I don't have personnel announcements to make from here today."

[Updated at 3:13 p.m.] Petraeus issued a statement announcing his resignation, saying, "After being married for over 37 years, I showed extremely poor judgment by engaging in an extramarital affair.

"Such behavior is unacceptable, both as a husband and as the leader of an organization such as ours. This afternoon, the president graciously accepted my resignation."
Picture
(photo courtesy, the library of politico.com)
WASHINGTON (AP) -- David Petraeus has resigned as director of the CIA after admitting he had an extramarital affair.

According to his letter of resignation, Petraeus asked President Barack Obama on Thursday to allow him to resign and on Friday the president accepted.

Petraeus said in a statement that he had shown "extremely poor judgment" in having the affair.

Petraeus has been married for 37 years to Holly Petraeus, whom he met when he was a cadet at the U.S. Military Academy at West Point.

The retired four-star general led the military campaigns in Iraq and Afghanistan, then took the helm of the CIA in September 2011.

The CIA had no immediate comment.

source: The Associated Press
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.

Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.

Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.

Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @HudumambayaTz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.

Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.

Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani.

Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo - hudumabongo@gmail.com

Novemba 9, 2012
Picture
Hiki kipeperushi kiliokotwa Dodoma hoteli (picha: Lukwangule blog)
Picture
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Agustino Matefu akiongea na waandishi wa habari Mjini Dodoma. Anasema bilioni tano zimetengwa kumng'oa Mwenyekiti wa CCM (picha: Lukwangule blog)
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Kikwete akiteremka kwenye ndege leo Dodoma.
Picture
Rais Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dodoma leo.
Picture
Rais Kikwete akiwasili Dodoma leo,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma via HabariLeo

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ameibua tuhuma nzito na kusema kuwa kuna mpango mchafu unaosukwa kwa lengo la kuhakikisha Mwenyekiti wa Taifa Rais Jakaya Kikwete anang’olewa nafasi hiyo kwa kupigiwa kura za hapana.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Mjumbe huyo Agustino Matefu alisema kuwa wamegundua baadhi ya vipeperushi ambavyo vitasambazwa siku moja kabla ya uchaguzi na kuwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kutounga mkono uchafu huo na uhuni unaoongozwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

Mmoja wa vipeperushi hivyo ambavyo gazeti hili lina nakala yake kilikuwa Kimeandikwa: “Ndugu Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Chama chetu kinayumba eti kwa pamoja tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais kwa kumvua kofia moja ya Uenyekiti, kwa pamoja tutashinda piga kura ya hapana kwake,” kilisema moja ya kipeperushi hicho chenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kuwa moja ya vipeperushi hivyo kilikutwa Dodoma Hotel ambapo Hussein Bashe na wenzake watatu walipokuwa kwenye kikao usiku wa kuamkia jana na walifika hapo baada ya kupata taarifa ya kikao hicho na kufuatilia.

Aliwataja wengine hao kuwa Beno Malisa, Martine Shigela na Fred Lowassa. Alipohojiwa Bashe alikanusha kuhusika na kampeni za kumng’oa Kikwete wala vipeperushi hivyo na kusema kuwa hizo ni fitina za kisiasa.

Mjumbe huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa, mafisadi wametenga jumla ya shilingi bilioni tano kwa lengo la kupitisha wajumbe wao wa NEC ambao watasimamia maslahi yao ya Urais.

Alisema kuwa kuna haja ya kukataa na kupinga mipango michafu kama hiyo yenye lengo la kukifedhehesha chama na kukitia aibu na kuonekana kuwa ni chama cha watu fulani.

Mjumbe huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa yuko tayari kutoa ushahidi kutokana na hayo anayoongea kwani ana ushahidi nayo.

“Mimi ni mwanasheria ninajua ninachokiongea kwani wakati mwingine ni lazima tukisaidie chama kule kinakopelekwa siko,” alisema.

Matefu alisema kuwa, kwa niaba ya Umoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa nane wa UVCCM wanaopinga matokeo ya uchaguzi huo wanaendelea kusikitishwa na vitendo viovu vinavyopangwa kufanya usiku wa kuamkia uchaguzi mkuu na watahakikisha wanawaibua na kuwatangaza wanaofanya hivyo ili njama zao zijulikane.

Mgeja akanusha kumhujumu JK

Naye Kareny Masasy akiandika kutoka Shinyanga, anaripoti kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamisi Mgeja ameibuka na kukanusha uvumi anaozushiwa kwamba amezunguka katika baadhi ya mikoa kuwagawia fedha wajumbe watakaopiga kura siku ya Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho (NEC) ili kumuangusha Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga alisema: “Kuna maneno yamezushwa kuwa nimeonekana na wajumbe mkoani Tabora na Zanzibar nikigawa Sh milioni tatu kwa wajumbe. Wanaozusha uvumi huo ni kundi la wahuni waliokaa na kutaka kuleta fitna, nakiomba chama kiwe macho na watu hao”.

Alisema kuna pepo mbaya ambaye anakiandama chama hicho na kuwaomba wanaCCM wote kukiombea chama hicho ili kuondoa pepo hilo.

“Hii inataka kujirudia tena, hata mwaka 2002 tuliwahi kushushwa kwenye treni wakati tukisafiri kuelekea kwenye uchaguzi kama huu tukiwa mimi, John Shibuda na Edward Ng’wani na tukaelezwa kuwa ni agizo la Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwa vile eti kulikuwa na tetesi kwamba tunataka kufanya fitna dhidi ya Mwenyekiti mstaafu Benjamini Mkapa.”

“Kwa bahati nzuri chama kimeruhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutuchunguza, naomba nichunguzwe ili ibainike ukweli wa jambo hili maana nimechoshwa na siasa uchwara, sababu wanayoieleza mbona hawasemi kuwa tukimng’oa Rais Kikwete tutamuweka nani?
Taarifa ifuatayo imeripotiwa na GSengo kwenye blogu yake:

Habari za sasa toka chumba cha uchaguzi zinamtaja diwani aliyepitia vigingi vingi huku akiwaburuza wenzie kortini mara kadhaa akidai haki zake mh. Henry Matata wa kata ya Kitangiri Ilemela jijini mwanza ameukwaa umeya wa Ilemela ...

Wajumbe wenzake wote kupitia CHADEMA walisusia kushiriki uchaguzi  wakabakia wa CCM na CUF, akidi ikawa imetimia nusu, sheria na kanuni ikaruhusu uchaguzi kuendelea, amini usiamini akashinda kwa 100%

Naibu wake ni Swila Dede (CCM) ambaye ni Diwani wa kata ya Sangabuye.
Picture
Bango pekee lililokuwepo wakati Rais Jakaya Kikwete akizindua ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Lindi kwenda Kinyerezi, Dar es Salaam. Katika gazeti moja linalotoka kila siku limetoa habari kuwa Rais Kikwete alakiwa kwa mabango wakati lililokuwepo ni hilo tu. Aliyeshika bango hilo kwa lengo la kufikisha malalamiko kwa Rais, hakupata kashikashi yoyote kutoka kwenye vyombo vya usalama. (picha: Kamanda wa Matukio)
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.

Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.

Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:

1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo

2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
  1. Ridhiwani Kikwete                                    Mwenyekiti
  2. Ahmed Seif (Magari)                                Mjumbe
  3. Nassoro Bin Slum                                      Mjumbe
  4. Henry Tandau                                            Katibu
  5. Ahmed Mgoyi                                            Mjumbe
  6. Aboubakar Bakhresa                               Mjumbe
  7. Angetile Osiah                                           Mjumbe
  8. Kassim Dewji                                             Mjumbe
  9. Abdallah Bin Kleb                                   Mjumbe
  10. Salim Said                                                   Mjumbe

Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012
Picture
Eliakim Maswi

Tafadhali bofya kifute cha pleya hapo kumsikiliza Spika wa Bunge, Anne Makinda akisoma Bungeni leo, ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyochunguza kashifa iliyomhusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi akiwatuhumu baadhi ya Wabunge kula rushwa kutoka kwenye makampunmi ya mafuta.

Baada ya kusoma ripoti, Spika alitoa uamuzi wake.

Ripoti hiyo ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa (Mlalo-CCM), Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi iliundwa Julai 2 mwaka huu na ilishakamilisha kazi yake na kuiwasilisha kwa Spika, Septemba 20, 2012.

Pamoja na Mwenyekiti Ngwilizi, wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma.

00:00
00:00
Ripoti ya Kamati ya Bunge - Spika, Anne Makinda
Text document (maandishi) ya kilichopo kwenye audio imepachikwa hapo chini (embedded document).


Source: http://www.wavuti.com/index.html#ixzz2BnIQzYRa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat