StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 31, 2012

Haya sasa :Wasanii wapiga marufuku matumizi ya ringtone zao, wayapa makampuni ya simu siku saba

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Umoja wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rhumba, Dance, muziki wa Injili na aina zingine leo umetoa agizo kwa makampuni yanayouza miito ya simu nchini pamoja na makampuni ya simu kuiondoa miitio hiyo ndani ya siku saba kuanzia leo mpaka pale watakapokubaliana mikataba mipya.

Katika barua hiyo iliyoandikwa kwenda kwa waandishi wa habari na iliyosainiwa na wasanii zaidi ya 150 nchini, wasanii hao wameyataka makampuni ya simu kuondoa matangazo ya ringtone hizo kwenye radio, magazeti, tv, website na kwenye ujumbe mfupi wa simu.

Hatua hiyo imechukuliwa na wasanii hao baada ya kubaini kuwa makampuni ya simu yanawanyonya kwa kiasi kikubwa kwa kuwalipa chini ya asilimia 10 ya mauzo ya ringtone hizo huku yenyewe yakibaki na zaidi ya asilimia 80.

Wiki iliyopita mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe aliliibua suala hilo bungeni na kudai kuwa imeundwa kamati itakayoangalia upya utaratibu wa mauzo ya ringtone.

Press Release ndio hii.

YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.

Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.

Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.

Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.

Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.

DIAMOND ALAZWA KWA MUDA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Hii ni picha ya Diamond akiwa hospitali baada ya kubanwa ghafla na kifua na hivyo kwenda kufanyiwa uchunguzi ili kujua tatizo. Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz ambaye ni mshikaji wake wa karibu tayari msanii huyo amesharuhusiwa lakini majibu ya vipimo vyake yatatoka kesho. 

Miezi ya hivi karibuni Diamond amefululiza kufanya show katika mikoa mbalimbali bila kupata mapumziko ya kutosha na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu.

Kupitia Twitter Diamond ameandika "Dah hali yangu si nzuri, naumwaaa."

Tunamwombea Diamond apone haraka.

HALI YA DR. ULIMBOKA HUKO S.A

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Na Mwandishi Wetu
Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.
Dk.Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.
Chanzo chetu kimetoa taarifa kuwa, Dk. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.
Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: “He’s recovering slowly.” (Anapona taratibu).
Alipomuuliza Watanzania wamtegemee lini daktari huyo kurudi nchini, alijibu: “Itachukua muda kupona. Muhimu kwa sasa ni Watanzania na wote wanaompenda, wamuombee kwa Mungu ili matibabu yaende sawa.”
VIPI USALAMA WAKE?
Chanzo chetu kilibainisha kuwa usalama wa Dk. Ulimboka ni wa uhakika, kwani watu wanaomlinda hospitalini hapo wapo makini.
“Nani asiyejua mazingira ya hatari aliyonayo Steven (Dk. Ulimboka)? Hii inasababisha maisha yake hospitalini yawe chini ya ulinzi mkali.
“Kwanza si kila mtu anaruhusiwa kwenda kumuona. Hospitali yenyewe aliyolazwa hatutaki itangazwe. Maisha ya Steven ni siri,” alisema mtoa habari wetu na kutoa siri hii:
“Wiki iliyopita pale hospitali alipolazwa, alitokea mtu fulani hivi Mwafrika. Muonekano wake ukawafanya watu wahisi ni Mtanzania. Watu wanaohusika na usalama wa Steven walikuwa makini sana.
“Kilichosababisha yule mtu aonekane ni Mtanzania ni fulana aliyovaa, kifuani ina ramani ya Tanzania. Watu wanaomlinda Steven wakaogopa sana, wakamfuatilia hatua kwa hatua bila mwenyewe kujua. Bahati nzuri naye alikuwa amekwenda kwa shughuli zake na akaondoka salama.
“Kwa kifupi, hali ilivyo pale hospitali ni kwamba ulinzi ni mkali, tena afadhali mtu awe wa taifa lingine, Watanzania ndiyo wanaogopwa zaidi, kwani huwezi kujua nani mzuri wa Steven na adui yake ni yupi.”
TATIZO LILIPOANZIA
Dk. Ulimboka, akiwa kwenye harakati za kuendeleza mgomo wa madaktari ili kuishiniza serikali iridhie madai yao, alitekwa kisha akavunjwa mbavu, miguu yote, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo, linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana ambapo kabla ya kufanyiwa unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kisha kumtelekeza katika eneo la Msitu wa Mabwepande, nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Chanzo gazeti la uwazi

July 30, 2012

NEW! NEW! NEW!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

July 28, 2012

Highlights from the 2012 Olympics Opening Ceremony

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Getty Images

The Queen officially declared the 2012 Olympic Games open Friday in London, setting in motion a 4-hour, $42.2 million opening ceremony. The epic event featured over 10,000 athletes from 204 countries and lots and lots of music from Queen, David Bowie, and the Beatles. Plus, appearances by David Beckham, Lord Voldemort, Mr. Bean, Will & Kate, and more!

2012 Olympic Games - Opening Ceremony
A performer in a giant ball is passed around during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England. 2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Basketball player Lauren Jackson of Australia carries her national flag into the stadium during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England.
2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Performers with a jetpack takes part in the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England. 2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Tower Bridge is seen before the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games on July 27, 2012 in London, England.
2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Queen Elizabeth II (R) and Jacques Rogge (L), President of the International Olympic Committee, attend the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London 2012 Olympic Games - Opening Ceremony
(L-R) Prince William, Duke of Cambridge, Catherine, Duchess of Cambridge and Samantha Cameron watch on during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England.2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Performers pay tribute to British music during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England. 2012 Olympic Games - Opening Ceremony
The Olympic rings are assembled above the stadium in a scene depicting the Industrial Revolution during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England.
2012 Olympic Games - Opening Ceremony
 
David Beckham drives a speedboat carrying the Olympic flame to the London 2012 Olympics opening ceremony on July 27, 2012 in London, England. Athletes, heads of state and dignitaries from around the world have gathered in the Olympic Stadium for the opening ceremony of the 30th Olympiad. London plays host to the Olympic Games which will see 26 sports contested by 10,500 athletes over 17 days of competition. 2012 Olympic Games - Opening Ceremony
Performers in the role of Mary Poppins float inside the stadium during the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium on July 27, 2012 in London, England. (Getty Images)more pic

Milioni 1.6 wanahitajia msaada wa chakula Zimbabwe

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mpango wa Chakula Duniani WFP umetangaza kwamba kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Zimbabwe watu milioni 1.6 wanahitajia msaada wa chakula nchini humo mwaka huu. Felix Bamazon Mkurugenzi wa WFP amesema, tayari maafisa wa shirika hilo wameripoti dalili za njaa katika maeneo ya vijijini kutokana na kilimo duni suala lililosababishwa na mvua zisizokuwa na uhakika na ukosefu wa mbegu na mbolea. Suala hilo pia limepelekea Waziri wa Fedha Tendai Biti atabiri kwamba ukuaji wa uchumi wa Zimbabwe utashuka toka asilimia 9.4 hadi asilimia 5.6 mwaka huu wa 2012. Mwezi Disemba pia Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa watu milioni 1.45 watahitajia msaada wa chakula nchini Zimbabwe.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA JIJINI ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati leo Julai 27, 2012 akitembelea mazingira ya Chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya mkoa huo wa Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo Julai 27, 2012 kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati akimfafanulia kuhusu kazi za maabala mpya inayoandaliwa katika Chuo hicho wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo Julai 27, 2012 kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kuhusu matuzmi ya baadhi ya majengo yaliyopo katika Chuo hicho, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo Julai 27, 2012 kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.

July 27, 2012

BancABC YASAINI MKATABA NA TFF WA MASHNDANO YA BancABC SUP8R

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

 Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah wakibadilishana mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wa mashindano ya mpira wa miguu utakaotambulika kama BancABC SUP8R katika Ukumbi wa TFF Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah (kulia) akisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa BancABC wa mashindano ya SUP8R yanayotarajiwa kuanza rasmi 4Julay2012.Mkataba huo ulifanyika TFF Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni
 Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni (kushoto) akisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa BancABC wa mashindano ya SUP8R yanayotarajiwa kuanza rasmi 4Julay2012.Mkataba huo ulifanyika TFF Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah.
 Katibu Mkuu wa TFF akizungumza na waandishi wa habari
 Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa BancABC,Mwalimu Zuberi akizungumza na waandishi wa habari
 Katibu akizungumza
Waandishi wakisikiliza

Wanasayansi wataja kinga, tiba za Ukimwi

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


WANASAYANSI wanaohudhuria  Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa Ukimwi wameweka hadharani baadhi ya tafiti ambazo zimetoa mwanga wa mapinduzi katika kupata dawa za kinga, tiba na chanjo ya ugonjwa huo.

Wanasayansi hao wamezitaja baadhi ya tafiti hizo kuwa ni HPTN 052 iliyowezesha upatikanaji wa dawa ya kuzuia maambukizo na ya pili, ni upandikizaji wa dawa kwenye mifupa, ambao ulionyesha kutibu Ukimwi.

Tafiti ya tatu ni ile ya uwezekano wa chanjo, ambapo baadhi ya makundi maalumu ya watu wamegundulika kujijengea wenyewe kinga dhidi ya virusi.

Wanasayansi hao walieleza hayo katika siku ya tatu ya mkutano huo unaofanyika Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu zaidi 22,000 miongoni wao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Mkutano huo na gazeti hili kupata nakala yake, wanasayansi hao walisema dawa za kuzuia maambukizo ni moja ya silaha kubwa kuelekea kupata ushindi dhidi ya kupiga vita Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Walitoa mfano wa utafiti uliopewa jina HPTN 052 ambao umeonyesha kuwa, unawezesha kupunguza maambukizo ya VVU kwa asilimia 96.

Katika utafiti huo, dawa hiyo imeonekana kufanya kazi vizuri zaidi pale mwathirika anapotumia dawa hiyo mapema wakati seli nyeupe za kinga aina ya CD4 zikiwa kati ya 350 na 550 kwa kila milimita za ujazo za damu.

“Tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ni sayansi ambayo imechangia mapinduzi makubwa katika kukabili VVU tangu dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV) zianze kutumika duniani mwaka 1996,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira na kuongeza kuwa, “ARV zimeweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani.

Dk Katabira aliongeza: “Mpango mzuri uliohamasishwa na wanasayansi katika matumizi ya ARV, hasa katika nchi zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo, umewezesha matokeo chanya ya mkakati wa kukabiliana na Ukimwi.”

Kuhusu upatikanaji wa tiba ya Ukimwi, wanasayansi hao walizindua mpango kabambe wa dunia wa namna ya upatikanaji wa tiba.

Naye Makamu Mwenyekiti wa mkutano huo, Dk Diane Havlir akasema: “Huu ni mkutano ambao wanasayansi wamethibitisha kuwa tiba ya Ukimwi ipo karibu kupatikana.”

Naye Dk Havlir ambaye pia ni Mtaalamu wa Tiba katika Chuo Kikuu cha Calfornia, Marekani aliongeza: “Matumaini ya wanasayansi kwenye mkutano wa mwaka huu kwamba upatikanaji wa tiba yanaashiria hatua iliyopigwa na wataalamu hao katika miaka michache ya karibuni.”

Dk Havlir alifafanua; “Ndiyo maana tunazungumzia kuhusu ufumbuzi wa kisayansi wa kutatua tatizo hili, ambao hatukuthubutu kuutamka miaka kadhaa iliyopita,”

Dk Havlir alieleza kuwa, matokeo kadhaa ya tafiti hizo za kisayansi yameleta mapambazuko mapya katika kupata tiba.

Dk Havlir aliuzungumzia utafiti ambao alifanyiwa mwathirika wa VVU wa Ujerumani, Timothy Brown ambaye dawa iliyopandikizwa kitaalamu na wanasayansi kwenye mifupa yake ilimwezesha kumponya kabisa na hana tena VVU.

Utafiti wa Tanzania
Wataalamu hao pia walizungumzia utafiti ambao pia madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi, Tanzania walichangia kwa kiwango kikubwa katika kuufanikisha.

Dk Havlir aliuelezea utafiti huo kuwa ni ule uliobaini kuwa, kuna baadhi ya watu ambao baada ya kuambukizwa VVU walijijengea kinga madhubuti na wameendelea kuishi pasipo matatizo.

Gazeti la Mwananchi toleo la Desemba 2, mwaka jana liliripoti juu ya utafiti huo ambapo wanasayansi wa Tanzania walishiriki katika kuufanikisha.

Kiongozi wa ushirikiano wa kitafiti kati ya KCMC na Chuo Kikuu cha Afya cha Duke nchini Marekani, Dk Elizabeth Reddy alinukuliwa akisema; “KCMC ilisaidia sana kufanikisha utafiti huo ambao utawawezesha wanasayansi kupata chanjo.”

Katika siku hiyo ya tatu ya mkutano huo ulioanza Jumapili wiki iliyopita, wanasayansi kadhaa walitoa hoja zao kuhusu mapambano ya Ukimwi na kuhimiza juhudi za kisayansi za kupata tiba kamili.

Katibu Msaidizi wa Idara ya Afya Marekani, Dk Howard Koh alisema nchi yake ina mpango kabambe wa kitaifa kuokoa maisha ya waathirika kwa ushirikiano na mataifa mengine duniani.

Mtaalamu kutoa Taasisi ya Utafiti wa Ukimwi ya IrsiCaixa, Javier Martinez-Picado alisisitiza kuwa ajenda ya upatikanaji wa tiba ya ugonjwa huo ndiyo mbinu madhubuti zaidi inayopaswa kufanikishwa na wanasayansi.

Mtaalamu wa utafiti wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta iliyopo Nairobi nchini Kenya, Dk Nelly Mugo alizungumzia juu ya umuhimu wa matumizi ya dawa za ARV kuzuia maambukizo kwa watoto wakati wa kujifungua.

Alisema mpango huo umesaidia kwa kuokoa maisha ya watoto wengi waliozaliwa kuambukizwa VVU.

Katika siku ya pili ya mkutano huo, watafiti hao waliweka bayana kuwa VVU siyo tishio tena kwa dunia kwa sababu wanazo nyenzo zote za kukabiliana nao ila kinachotatiza ni fedha.

Walisema fedha zitawaongezea nguvu katika kufanikisha mipango ya kisayansi pamoja na uwekaji wa sera zitakazosaidia mapambano thabiti dhidi ya VVU.

July 26, 2012

YANGA YATINGA FAINALI ZA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUITANDIKA APR 1-0

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

 Kiiza akipambana na mchezaji wa APR
 Wachezaji wa yanga wakishangilia walipopata bao
 Said Bahanuzi 'Spider Man' akiwa amembeba Kiiza baada ya kufunga bao
Kiiza akipambana

BAO pekee la mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110, limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa itamenyana na Azam FC keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kiiza alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.
 
Yanga waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.

Vigogo wagawiwa viwanja Dar

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama
WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI  ‘ZIMEENDA NA MAJI’

MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama  wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na  Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe;  Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan  Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema  kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

“Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wananchi walalama

Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

“Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo,” alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

“Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato”.

Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: “Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi!  Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

Aliongeza: ”Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe.”

Mgawo wa Viwanja

Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na  kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

“Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana,” linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.

ALIYEKUWA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO ZANZIBAR HAMAD MASOUD AKIKABIDHI OFISI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Waziri Mpya wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif kulia akikabidhiwa Ofisi yake na Waziri wa Wizara hiyo aliyejiuzulu karibuni Hamad Masoud Hamad kufuatia ajali ya kuzama kwa MV.Skagit.
(Picha na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar)

July 25, 2012

Watu wazidi kujinyakulia zawadi za promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO ya SBL

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchezesha droo ya 12 katika promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL, kulia ni Tumainieli Mlisa kutoka PWC na kushoto ni Bakari Maggid kutoka bodi ya taifa ya bahati nasibu.Washindi katika droo hiyo ni Kosmas George Bugomora 41 kutoka mkoa wa Mwanza na bw.Sebastian Temu 48 kutoka Dar es Salaam ambao wote kwa pamoja wamejishindia jenereta huku bw.Deo Mkama 47 kutoka mkoani kilimanjaro ambaye  amejinyakulia bajaj mpya.
Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo katikati akiongea na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL, kupitia simu ya mezani,kulia ni Bakari Maggid mkaguzi kutoka bodi ya taifa ya bahati nasibu, wengine ni wasimamizi kutoka PWC. Hii ni droo ya 12 katika promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa takriba wiki 15 sasa.

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aongoza Watanzania Kuadhimisha Siku Ya Kumbukumbu ya Mashujaa Jijini Dar es Salaam

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Askari wa Jeshi Wakiwa na Mkuki na Ngao sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,akifurahia jamabo na mkuu wa majeshi nchini jenerali Davidi Mwamunyage   kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Julai 25, 2012 kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na mkuu wa majeshi nchini jenerali Davis Mwamunyage na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalamakatika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Askari wa JWTZ wakiwakumbuka Mashujaa kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Baadhi ya Vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoshiriki kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao  na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange akitoa heshima zake wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa DRC Nchini Mhe Khalfan  Mpango akiweka shada la maua wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
  Meya wa Jiji la Dar es salaam Mstahiki Dkt Didas Masaburi akiweka upinde na mshale wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es salaam Mzee Rashidi Bakari Ngonja akiweka shoka wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 CCT Mchungaji  John Kamoyo akisoma sala wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Roman Catholic: Monsinyori Deogratias Mbiku akisoma sala wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
   Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na Askofu wa  Roman Catholic: Monsinyori Deogratias Mbiku wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Sehemu ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
Sehemu wa Wageni mbalimbali Walioudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012.
 Kutoka (kushoto) Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa DRC Nchini Mhe Khalfan  Mpango, Meya wa Jiji la Dar es salaam Mstahiki Dkt Didas Masaburi,Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es salaam Mzee Rashidi Bakari Ngonja Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq,  wakiwa katika viwanja vya Mnazi  Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012.
 Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mkuuw Wa Majeshi Meja Jenerali Davis Mwamunyange katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
 Rais Jakaya Kikwete Akigana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.
Sehmu wa Wapiga Picha Mbalimbali wa Vyombo vya Habari Wakifwatilia na Kupiga picha kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.Picha Zote na IKULU
--
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Juli 25, 2012 ameongoza Watanzania katika kuadhimisha siku ya Mashujaa Kitaifa katika Bustani ya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
Zifuatazo ni taswira ya hafla hiyo ya kila mwaka
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat