StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

June 30, 2012

Daktari: Hali ya Ulimboka mbaya

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
ASEMA FIGO ZAKE ZIMESHINDWA KAZI, ZATAKIWA DOLA 40,000 KUMPELEKA INDIA
AFYA ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka imebadilika na kuwa mbaya, baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi ya kuchuja sumu ya mwili na kusababisha apatiwe huduma ya kusafisha damu yake.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na kiongozi wa jopo la madaktari wanaoendelea kumtibu, Profesa Joseph Kahamba, zilieleza kuwa hali ya Dk Ulimboka ilibadilika na kuwa mbaya na hivyo kuwapo mikakati wa madaktari wenzake kukusanya fedha ili kumpeleka nje ya nchi.

Dk Ulimboka ambaye amelazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alipatiwa huduma hiyo jana asubuhi kwa kutumia mashine maalumu, iliyoko katika Kitengo cha Watoto cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Daktari huyo ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari unaoendelea nchi nzima kutokana na Serikali kushindwa kutimiza madai yao mbalimbali, amelazwa kutokana na majereha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kisha kupigwa, kung'olewa kucha, meno mawili na kutupwa katika Msitu wa Pande, usiku wa kuamkia Jumatano.

Tangu alazwe MOI baada ya kuokotwa na wasamalia wema, katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya Jiji la Dares Salaam, hali ya afya ya Dk Ulimboka imekuwa tete na jana ilizidi kuwa mbaya.

Kauli ya Dk Kahamba

Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Kahamba alisema kutokana na tatizo hilo, mgonjwa huyo jana alilazimika kusafishwa damu.

Alieleza hayo alipotakiwa kuthibitisha taarifa zilizolifikia gazeti hili kuwa afya ya Dk Ulimboka haikuwa nzuri na madaktari wanachangishana fedha kumpeleka kwenye matatibu ya kusafishwa damu katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam au nje ya nchi.

"Taarifa hizo zina ukweli, lakini siyo jambo rahisi kiasi hicho kwamba anatakiwa kusafishwa damu. Kama ni damu amesafishwa leo (jana) asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Profesa Kahamba na kuendelea:

"Suala lake ni complicated (tata) zaidi, lakini ili watu waelewe, siyo mbaya mkisema figo zimefeli(zimeshindwa kufanya kazi)."

Alipotakiwa kueleza sababu ya tatizo hilo, Profesa Kahamba alisema, "Siwezi kueleza kwa undani ila haya maumivu ya kupigwa na kuteswa yanachangia kwa kiasi kikubwa."

Alipotakiwa kueleza yeye anaonaje hali ya sasa ya Dk Ulimboka, Profesa Kahamba alisema: “Ni uongo tukisema anaendelea vizuri."

Aliendelea, "Unajua alipofikishwa hapa Muhimbili juzi (Jumatano) afya yake ilikuwa mbaya, na jana (Alhamisi) alionekana kuendelea vizuri, lakini jana hiyohiyo, hali yake ilianza kubadilika na vipimo vilionyesha kuwa ana complications (matatizo) za figo.

"Sasa figo ni kitu sensitive (muhimu) sana, anahitaji uangalizi wa karibu na kimsingi hatuwezi kusema kwamba anaendelea vizuri. Ni vyema tukisema tu afya yake ni mbaya," alieleza.

Taarifa za awali kutoka kwenye chanzo chetu hospitalini hapo, zilieleza kuwa Dk Ulimboka ambaye alipata tatizo linalojulikana kama “Acute renal failure”, alifanyiwa tiba inayojulikana kama Dialysis, ambayo ni kitendo kutumia mashine maalumu kufanya kazi ya kuchuja sumu ya mwili kwenda kwenye mkojo, baada ya figo ambazo hufanya kazi hiyo kushindwa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Dialysis inaweza kumsadia mgonjwa ambaye figo zake zimeshindwa kufanya kazi, kuishi kama kawaida, lakini kwa Dk Ulimboka haikutoa matokeo mazuri.

Michango ya madaktari

Jana ulifanyika Mkutano wa Madaktari Bingwa wa MNH, Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ocean Road (ORCI) na kuazimia kukusanya Dola za Marekani 40,000 (Sh64,000,000) ili Dk Ulimboka asafirishwe kwenda India kwa matibabu zaidi.

Taarifa za maazimio hayo zilitangazwa kwa waandishi wa habari na Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitega, kuwa afya ya Dk Ulimboka haikuwa nzuri hivyo zikipatikana fedha hizo angepelekwa nje ya nchi.

Dk Chitega aliwataka wanataaluma hao na wananchi kwa ujumla kuchangia safari hiyo ili kuokoa maisha ya daktari huyo, huku akitaja namba za mawakala wa simu za Vodacom na Tigo, ambazo zitatumika kukusanya michango hiyo.

Habari zilizopatikana baadaye wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa, Dk Ulimboka alitarajiwa kusafirishwa kwenda Nairobi, Kenya kwa matibabu zaidi.


TANNA MOI watoa tamko
Katika hatua nyingine, Chama cha Wauguzi (Tanna), Tawi la MOI kilitoa tamko la kulaani kitendo cha kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na kutaka uchunguzi wa kina na haraka ufanyike ili kubaini watu waliohusika.

Mwenyekiti wa Tanna, Tawi la Moi, Prisca Tarimo alisema katika tamko hilo kuwa, kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka ni cha kinyama na kisicho cha kiutu.

Katika tamko hilo, Tanna imeomba Serikali kutafuta suluhu ya mgomo huo haraka kwa kuwa unaathiri maisha ya watu na kuwaongezea mzigo wa kiutendaji wauguzi.

Mgomo wa madakati unaingia siku ya saba leo, huku suluhu ya kuaminika ya kutatua tatizo hilo, ikiwa bado haijapatikana.

Polisi wakanusha
Katika hatua nyingine, James Magai anaripoti kuwa, Jeshi la Polisi limekanusha kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka, huku likipinga pia taarifa za daktari huyo kumtambua mmoja wa askari walio katika jopo la uchunguzi wa tukilo hilo alipokwenda kumtembelea hospitalini.

Pia jeshi hilo limetoa wito kwa madaktari hao walioko katika mgomo kuwa na busara na kutii amri ya Mahakama, ya kuwataka wasitishe mgomo wao.

Pia limeonya kuwa ikiwa wataendelea kukaidi na kupuuza amri ya hiyo ya mahakama, linao wajibu wa kuwachukulia hatua kwa kuwafikisha mahakamani, ili wajibu mashtaka hayo.

Msimamo huo ulitolewa jana na Kamishna wa Oparesheni Maalumu, Kamishna wa Polisi (CP), Paul Chagonja wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano alioitisha kuzungumzia matokeo ya operesheni ya jeshi hilo ya majuma matatu katika kuzuia uhalifu nchini.

Alisema madai hayo ni uvumi ambao unalenga kulifanya jeshi hilo lisiaminike na kufifisha juhudi zake za kuwasaka waliohusika na unyama huo.

Source: Mwananchi

Wageni watekwa wakiwa kambini Kenya

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
DadaabPolisi nchini Kenya wamesema kuwa wafanyikazi sita wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Ifo ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
kambi hiyo inatoa hifadhi wakimbizi nusu milioni
Waliotekwa ni wafanyikazi wa shirika la Norwegian Refugee Council, ambalo linatoa huduma kwa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi kwenye kambi hiyo.
Msemaji wa Shirika hilo, amedhibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa katibu mkuu Elizabeth Rasmussen alikuwemo kwenye msafara uliovamiwa lakini amenusurika.
Hata hivyo shirika hilo halijatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na watu waliotekwa.
Mkuu wa wilaya ya Lagdera ambako kambi hiyo ipo Robert Kimanthi amesema waliotekwa ni raia wa Canada, Norway, Mfilipino, Mpakistani na Wakenya wawili. Wote ni wanaume.
Kulingana na polisi watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walishambulia msafara wa magari katika kambi hiyo ambayo inatoa makaazi kwa zaidi ya wakimbizi nusu milioni kutoka Somalia. Mtu mmoja aliuawa kwenye tukio hilo.
Polisi wanashuku kuwa wapiganaji wa kiisalamu wa Al shaabab walihusika na shambulio hilo.
Visa vya mashambulio ya kigaidi vimeongezeka katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya, baada ya wanajeshi wake kuingia nchini Somalia mwaka jana kupambana na wanamgambo wa al shabaab.
Katika miezi ya hivi karibuni, wafanyakazi kadhaa wa mashirika ya kutoa misaada wametekwa nyara katika kambi hiyo ya Daadab.
Wawili kati yao ni wanawake wawili raia wa uhispania ambao walitekwa nyara mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Source: BBC swahili

June 29, 2012

ULIMBOKA ANA SIRI NZITO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya  usiku wa kumkia juzi, kisha kutupwa  Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili.

Dk Ulimboka aliokotwa na wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha akiwa katika Viwanja vya Klabu ya Leaders, Kinondoni.

Jana, Dk Ulimboka ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili huku hali yake ikiwa haijatengemaa vyema, alitoa kauli akisema ingawa ana maumivu makali anaendelea vizuri ikilinganishwa na siku ya kwanza.

Dk Ulimboka alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa aeleze mkasa huo uliomfika wa kukamatwa, kuteswa na kutupwa msituni.

DR ULIMBOKA AKIWA ICU

Hata hivyo, hadi sasa wingu zito la nani alimteka na watekaji walitaka kujua nini kutoka kwa kiongozi huyo wa madaktari, bado limetanda.

Siri nzito
Akisimulia mkasa huo kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema, akiwa katika klabu hiyo ya Leaders alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alikuwa atokee Tandika na baada ya kumsubiri ndipo alipofika kwenye klabu hiyo, lakini, alianza kujisikia vibaya tofauti na siku nyingine na kuongeza;  "Yaani  sikuwa na amani."

Alisema, "Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk Ulimboka)," alieleza na kuongeza:

"Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini halikuwa na namba."

Hata hivyo, jana Dk Ulimboka hakuonana na mwandishi wa habari hii, badala yake alirekodiwa, na Mwananchi kupata sauti yake  akijibu swali kuhusu hali yake na tukio hilo,  baada ya uongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kuzuia watu kumwona.

Daktari huyo wa magonjwa ya binadamu, amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).

"Kidogo najisikia nafuu ikilinganishwa na nilivyokuja ingawaje, bado nina maumivu makali. Kwa hivyo, ingependeza niendelee na mapumziko na mtu yeyote anayetaka kuniona pengine hilo jambo lisifanyike sasa. Hivi sasa ni vizuri nipumzike," ilisikika sauti hiyo ya Dk Ulimboka.

Lakini, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo.
 DR ULIMBOKA AKIWA ICU

Madaktari wanaolinda eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao.

Kiongozi jopo la madaktari

Katika hatua nyingine, kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili mzima.

“Ingawa kwa sasa anaendelea vizuri, Dk Ulimboka  ameumia sana, kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza:

“Aliumia mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole na kichwani  na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema.

Alifafanua kwamba, kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha yake.

 DR ULIMBOKA AKIWA ICU

Uongozi wa Moi watoa neno

Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (Moi) umeeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha taasisi hiyo.

Msemaji wa Moi, Almas Jumaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya hali yake kuendelea vizuri, lakini  haingewezekana kwa waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba alikolazwa na kumwona Dk Ulimboka.

“Mgonjwa anaendelea vizuri ukilinganisha na jana (juzi), anaongea, anawatambua watu wanaokwenda kumwona, lakini utaratibu wa kwenda kumwona kwa ninyi imeshindikana kwa sababu yupo (ICU) ni chumba chenye utaratibu wake,”alisema Jumaa.

Jumaa aliongeza kwamba ili mtu aweze kuingia wodini   analazimika kuvaa vazi maalumu na mavazi yaliyopo, yasingetosha, lakini pia wapo watu wanaoendelea kumpatia huduma ya matibabu.

Tamko la Jumuiya ya Madaktari

Wakati hali ya Dk Ulimboka ikiwa hivyo, madaktari wameipinga tume ya uchunguzi iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza suala hilo, wakidai mazingira ya tukio hayaliondoi jeshi hilo kuhusika.

Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa wangependa kuundwa kwa tume huru itakayofanya kazi ya kuchunguza tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma.

“Madaktari kwa ujumla wetu tunalaani tukio la kutekwa nyara,kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande, lakini pia hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi kwa sababu mazingira ya tukio hayaondoi kuhusika ama kutohusika kwa jeshi hilo,”alisema Dk Chitage.

Chitage alitoa msimamo wa madaktari kuwa ni kuendelea na mgomo, huku akionya Serikali kuacha vitendo vya kuwatisha, kwa madai kuwa vitendo hivyo haviwezi kuwa suluhu ya mgogoro kati ya pande hizo mbili.

“Kumekuwa na vitisho kwa madaktari katika maeneo mbalimbali nchini, hususan Dodoma, Mbeya, Arusha na Mwanza. Tunaionya Serikali kuacha mara moja na itambue kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizwa kwa namna nyingine yoyote bali ni kwa Serikali kutekeleza madai ya madaktari,”alisema Chitega na kuongeza:

“Sisi madaktari kwa umoja wetu, tumechoka kushuhudia Watanzania wakipoteza maisha kwa magonjwa tunayoweza kuyatibu, kufanya kazi katika mazingira magumu huku kukiwa hakuna mipango ya kuboresha mazingira ya kazi, kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.”

Mgomo huo wa madaktari leo unaingia siku ya saba tangu ulipotangazwa na mwenyekiti huyo kuwa, ungeanza rasmi Jumamosi iliyopita.

SERIKALI YASITISHA KUTOA TAMKO JUU YA MADAKTARI LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo.
Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma.
Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.
Kuhusu Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.

Madaktari bingwa nao wagoma

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

TUKIO la kutekwa nyara, kupigwa na kujeruhiwa vibaya, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, limechochea kasi ya mgomo baada ya madaktari bingwa kutangaza kujitosa rasmi kwenye mgogoro huo.Awali madaktari hao hawakushiriki mgomo huo, lakini jana walieleza kwa nyakati tofauti kuwa, wameamua kuungana na wenzao kutokana na unyama aliofanyiwa kiongozi wao akiwa katika harakati za kutetea na kupigania haki zao.

Madaktari hao wa hospitali za Muhimbili, Moi, KCMC, Mbeya, Bugando na Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, jana walitangaza rasmi kuwa wameingia kwenye mgomo huo kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali kutoa tamko kuhusu utata wa tukio hilo.

Tukio hilo la aina yake kutokea nchini, limeathiri upatikanaji wa huduma zote za matibabu katika hospitali hizo, huku madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Moi, wakielekeza nguvu zao kunusuru maisha ya mwenzao aliyeumizwa.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yao.

"Tunaitaka Serikali kuacha vitisho kwa madaktari nchini, tunaitaka itambue kwamba mgogoro huu hauwezi kumalizwa kwa njia yoyote vikiwemo vitisho bali ni kwa kukaa meza ya majadiliano na kukubaliana na madaktari," alisema Dk Chitega na kuongeza:

"Ninawashukuru madaktari wote nchi nzima, wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya afya kwa ujumla wao kwa kusitisha huduma baada ya kupigwa mwenzetu. Tunaomba mshikamano huu uendelee," alisema Dk Chitega.

Gazeti hili lilishuhudia wagonjwa wakiwa wamekaa katika makundi bila kujua la kufanya, huku wengine wakiamua kuondoka na kwenda hospitali binafsi.

Waliliambia Mwananchi kwamba kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka ni cha kinyama na kuungana na madaktari hao kuitaka Serikali kutatua mgogoro huo haraka.

Wagonjwa waliofika katika eneo hili pia walielezwa bayana na maofisa wa Moi kwamba huduma zimesitishwa  kutokana na madaktari kugoma.

Ocean Road

Madaktari bingwa katika Taasisi ya Ocean Road nao waligoma kutoa huduma hatua iliyozua taharuki kwa wagonjwa waliofika kwa ajili ya matibabu.

Gazeti hili lilishuhudia ofisi za madaktari hao zikiwa zimefungwa na hata zile ambazo zilikuwa wazi, madaktari hawakuwapo.

Mmoja wa wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Joyce Dachi, alisema kuwa, wagonjwa wengi wamekuwa wakiandikishwa mapokezi, lakini wanachukua muda mrefu kumuona daktari.


Mgomo huo pia umeendelea katika Hospitali ya Amana wilayani Ilala huku uongozi wa hospitali hiyo ambao uligoma kuzungumza na vyombo vya habari, ukihaha kunusuru hali hiyo.

Katika Hospitali za Temeke na Mwananyamala huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.

Mbeya

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ,madaktari bingwa ambao awali hawakugoma jana waliingia kwenye mgomo na kusababisha wagonjwa katika hospitali hiyo hususan kitengo cha wazazi, kusota bila matibabu.

Habari kutoka katika hospitali hiyo zilieleza kuwa hivi sasa madaktari bingwa wanatoa huduma kwa kujuana.

Mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema kitendo alichofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya yao kimewakatisha tamaa.

Alisema kuwa, hali hiyo sasa imehamia hadi katika Kituo cha Wazazi cha Meta na kufafanua kuwa hali ni mbaya, tayari wajawazito wametakiwa kuhamia katika Hospitali ya Mkoa ambayo imefurika wagonjwa.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Rufaa, Dk Eliuter Samky hakuweza kuzungumzia tukio hilo jana kutokana na kile kilichoelezwa na katibu wake muhtasi kwamba ana kazi nyingi.

Mwanza
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza nao wamegoma, huku kiongozi wa Kamati Ndogo ya hospitali hiyo inayoshughulikia migomo, akikataa kuzungumzia hali hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu baada ya kutoonekana katika maeneo ya hospitali, mmoja wa viongozi wa Kamati hiyo, Dk Geogre Adrian, alisema kwa sasa hawezi kulitolea ufafanuzi suala hilo na kwamba kufanya hivyo, ni kwenda kinyume na maagizo aliyopewa na Kamati Kuu.


Akizungumzia huduma katika hospitali hiyo alisema kuwa hajui lolote kwa kuwa hawajagusa maeneo ya kazi kwani  wapo kwenye mgomo.

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia huduma katika hospitali yake, hakupatikana.

Watimuliwa
Jana Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alitoa tangazo la kuwataka madaktari waliopo mafunzoni ‘Interns’ katika hospitali hiyo kurejea kazini na kama watakiuka agizo hilo, watakuwa wamejifukuzisha wenyewe.


Manyara
Mkoani Manyara, madaktari kumi katika Hospitali ya Haydom Wilaya ya Mbulu wamegoma tangu juzi.Idadi ya wagonjwa katika hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), inaongezeka siku hadi siku.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa masharti ya kutotaka kutajwa majina yao, madaktari hao ambao wanafanya mafunzo ya vitendo katika hospitali hiyo, wamesema kuwa hawatatibu wagonjwa mpaka madai yao yatekelezwe.


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, alithibitisha kutokea kwa mgomo huo na kufafanua kwamba wanaendelea kufanya mazungumzo ili kupata ufumbuzi.

Choya alisema kuwa madaktari wanaoendelea na kazi, wameelemewa  kutokana na wagonjwa kuwa wengi.

Alisema kati ya madaktari 11 wanaosoma kwa vitendo hospitalini hapo, mmoja tu anayesomeshwa na hospitali hiyo, ndiye hajagoma.

KCMC
 Hali katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro imezidi kuwa tete na kuwafanya ndugu kuwahamishia wagonjwa wao katika hospitali binafsi.

Mwananchi lilitembelea wodi za hospitali hiyo na kukuta vitanda vikiwa wazi.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya madaktari ambao wapo kwenye mgomo kwa sharti la kutotajwa majina, walisema hawako tayari kurudi kazini kwa kuhofia usalama wa maisha yao.

Dodoma
 Wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma jana walijikuta wakipata taabu baada ya madaktari wa hospitali hiyo kusitisha huduma kwa takriban saa sita kuanzia asubuhi.

Muda wa mchana utoaji huduma katika hospitali hiyo uliendelea ingawa kwa  kusuasua.

Tofauti na siku zote, jana chumba cha daktari kilichokuwa wazi ni kimoja tu hali iliyosababisha msongamano mkubwa.


Arusha

Mjini Arusha, madaktari wameendelea na mgomo katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na kusababisha kudorora huduma huku wagonjwa kadhaa wakiondolewa hospitalini hapo.

Mgomo huo, ulianza saa 1 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, ambapo madaktari na wauguzi,waligoma kutoa huduma wakitaka kujua hatima ya Dk Ulimboka. Walitaka pia kuzungumza na uongozi wa hospitali hiyo na waandishi wa habari, kuhusu mgogoro wao.

Askari anyimwa huduma

Askari wa Usalama Barabarani ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye alipata ajali jana, alijikuta akishindwa kuhudumiwa katika hospitali ya Mount Meru na kuondolewa kutokana na mgomo huo.

Askari huyo, aliyevaa sare, alifikishwa hospitalini hapo saa 5:00 asubuhi akiwa kwenye teksi, lakini wauguzi waliokuwa zamu walishauri apelekwe sehemu nyingine.

Hata hivyo, uongozi wa hospitali ya mkoa, ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Omar Chande, jana ulifanya kazi ya ziada ya kuwabembeleza madaktari hao, kurejea kazini, kusubiri uamuzi wa Serikali.



Mgomo, Dk Ulimboka
vyateka Bunge

Mgomo wa madaktari na kutekwa kisha kupigwa Dk Ulimboka jana vilitawala mjadala wa Bunge hadi pale Spika Anne Makinda alipotoa mwongozo kwamba suala hilo lisijadiliwe kwani liko mahakamani.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilazimika kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa juzi pale alipokuwa akizungumzia mgomo wa madaktari na kuhitimisha kwamba Serikali ilikuwa inajiandaa kutoa kauli na msimamo wake hivyo “liwalo na liwe’.

Pinda alilazimika kutoa maelezo kutokana na swali aliloulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyetaka kufahamu maana ya kauli ya Waziri Mkuu ambayo aliita kuwa ni nzito na iliyozua mjadala mkali nchini.

Kadhalika, Mbowe alitaka kufahamu hatua ambazo Serikali imechukua kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma za tiba kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba madaktari katika hospitali kadhaa walikuwa wakiendelea na mgomo.


Kadhalika Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alimuuliza Pinda kwamba haoni kwamba ni busara kujiuzulu wadhifa wake kutokana na ahadi yake kwamba mgomo wa madaktari usingetokea, lakini ahadi hiyo imeshindwa kutekelezeka.

Akimjibu Mbowe, Pinda alikiri kutoa kauli hiyo ndani ya Bunge juzi na kusema alifanya hivyo akiamini kuwa jambo hilo lilikuwa mahakamani na akasema asingeweza kusema jambo lolote kwa kuwa hana tabia ya kuwa na utovu wa nidhamu wa kuingilia mambo ya mahakamani.

Hata hivyo, alijitetea kuwa kabla ya kutoa kauli hiyo bungeni juzi, hakuwa na taarifa kuhusu tukio la kupigwa kwa Ulimboka na akasema kuwa, kauli yake haihusiani kabisa na Serikali kuhusika katika jambo hilo kwa namna yoyote ile.

Waziri Mkuu alisema tayari amekwishaagiza vyombo husika kufanya uchunguzi wa kina na kutoa majibu ya haraka ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki mara moja.

“Kwanza namtakia afya njema ndugu Ulimboka, na mimi nataka Watanzania waamini kuwa tulikuwa katika mazungumzo mazuri na madaktari chini yake Ulimboka hivyo tukio hilo ambalo limetokea katika mazingira magumu limetushtua kweli, kama ni Serikali basi ingekuwa ni Serikali ya ajabu kweli,’’alisema Pinda.

Kuhusu namna ya kusaidia Watanzania wasiathirike na mgomo huo, alisema tayari Serikali imeshaagiza madaktari kutoka wizarani kutumika na kuwaomba waliostaafu kutoa huduma katika kipindi hicho kigumu.

Mkakati mwingine ni pamoja na kutumia hospitali za Jeshi ikiwamo Lugalo waanze kutoa huduma hizo wakati Serikali inaendelea kuzungumza kwa utaratibu na madaktari.

Lissu aliuliza swali la nyongeza kumtaka Pinda kuachia ngazi hali iliyosababisha mvutano kwani Waziri Mkuu alikosoa uulizaji wa swali hilo kuwa halikustahili.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala la madaktari akitaka taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambayo ilifanyia kazi suala la mgomo wa madaktari ijadiliwe bungeni.

Hata hivyo, Spika Makinda alisema ripoti hiyo haiwezi kujadiliwa kwani tayari Serikali ilishakabidhiwa kwa ajili ya kuifanyia kazi na kwamba mapendekezo ya Bunge kupitia ripoti hiyo yamefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa.


Habari hii imeandaliwa na Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma, Godfrey Kahango,Mbeya, Joseph Lyimo,Mbulu, Sheilla Sezzy,Mwanza, Rehema Matowo, Moshi, Masoud Masasi,Dodoma, Fidelis Butahe, Geofrey Nyang'oro Dar, Mussa Juma, Arusha, Bakari Kiango na Victoria Mhagama

REDDS MISS MARA 2012 LEO JIONI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


 Washiriki wa shindano la Redds Miss Mara 2012 wakiwa katika picha ya pamoja katika ufukwe wa Ziwa Victoria, mkoani Mara baada ya mazoezi yao jana. Warembo hao wanataraji kupanda jukwaani leo, Juni 29, 2012 kuchuana vikali kuwania taji la mkoa wa mara na tiketiketi ya Kushiriki shindano la Redds Kanda ya Ziwa.

Pinda: Tukio la Ulimboka lina utata

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda , amesema tukio la kupigwa kwa  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Stephen Ulimboka, lina utata na kuongeza kuwa uchunguzi utakaofanywa na vyombo vya usalama ndio utakao maliza utata huo.

Pinda aliyasema hayo jana bungeni alipokuwa akijibu swali  lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

“Mazingira ya tukio hili bado yana utata mwingi, yanahitaji uchunguzi wa kina, kila mtu anasema lake, mwingine hili  na wengine wanasema Serikali ndiyo imehusika,” alisema na kuongeza:

“Mimi nasema kama ni Serikali basi tutakuwa ni watu wa ajabu sana, Serikali tufanye ili iweje.”
Pia Pinda alisema kuwa, Serikali imefanya juhudi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanaweza kuokoa maisha ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutumia hospitali za Lugalo pamoja na matawi yake, kutumia madaktari waliostaafu na wengine walio wizarani.

“Tumezungumza na wenzetu wa Lugalo ili wananchi waweze kutibiwa katika hospitali hiyo na matawi mengine,” alisema Pinda.

Baada ya maelezo hayo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Tundu Lisu, alimuuliza Pinda kwa nini asiwajibike katika suala la mgomo wa madaktari kwani ni yeye amekuwa akilishughulikia kwa muda na halionekani kupata ufumbuzi.

Baada ya swali hilo, Pinda alisema kuwa, yapo mazingira yanayoweza kumlazimu kuwajibika lakini siyo, haya ya mgomo wa madaktari kwani amejaribu kwa kiasi kikubwa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
“Yapo mazingira yanayoweza kunifanya nijiuzulu, lakini hili la madaktari nimejaribu kwa uwezo wangu, lakini be what it is (kwa jinsi lilivyo), kuna changamoto nyingi katika suala hili,” alisema Pinda.

Baada ya majibu hayo, Lisu alipewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na kusema “If you have tried your very best and  you failed,  why don't you resign?” (kama umejaribu kufanya kila linalowezekana ukashindwa, kwa nini usijiuzulu??)

Baada ya swali hilo, Spika  Anne Makinda alimtaka Waziri Mkuu kutojibu swali hilo la nyongeza kwa maelezo kuwa, linafanana na swali la msingi.

Hata baada ya maelezo ya Spika, Waziri Mkuu alijibu kwa kumueleza Lisu kuwa, anamuheshimu sana lakini lugha aliyotumia katika kuuliza swali lake siyo nzuri.

Mbunge Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Martha Mlata, aliyesema kuna uvumi kuwa, kuna watu wanawapa baadhi ya madaktari fedha ili wahamasishe wenzao kugoma.

Alisema kuwa, lengo la kikundi hicho ambacho hakukitaja, ni nchi isitawalike.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema na wao (Serikali) wamesikia uvumi huo na  wameviagiza vyombo vya usalama vilifanyie uchunguzi.

Wapinzani wa Yanga Kagame kutajwa leo

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

WAPINZANI wa Yanga, mabingwa watetezi Kombe la Kagame watajulikana leo wakati ratiba ya michuano hiyo itakapowekwa hadharani tayari kwa michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Cecafa, Nicholaus Musonye alisema jana kuwa ratiba hiyo itakuwa hadharani baada ya timu zote kuthibitisha kushiriki michuano hiyo.

Yanga inayotetea ubingwa wake, huenda ikafungua dimba la michuano hiyo. Itasindikizwa na timu za Simba (bingwa Bara) na Azam iliyoshika nafasi ya pili.

Musonye alisema kuwa michuano itafanyika kama ilivyopangwa jijini Dar es Salaam na ule wa Azam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 7,000.

Timu zitakazoshiriki ni APR (Rwanda), Yanga, Simba, Azam (Tanzania), Tusker (Kenya), Wau Salam (Sudan ya Kusini) na Atletico ya Burundi.

Timu nyingine ni Mafunzo (Zanzibar) Mamlaka ya Mapato (Uganda), Elman (Somalia), Ports (Djibouti), Red Sea (Eritrea) na Coffee ya Ethiopia.

Naye Rais wa Cecafa, Leodegar Tenga wamemshukuru Rais Paul Kagame kwa jitihada zake za kuinua soka katika ukanda huo. Rais Kagame amekuwa akidhamini michuano ya Cecafa tangu 1999.

Musonye aliwataka wadhamini wengine kujitokeza kusaidia kufanikisha michuano ya 2012 kama ilivyofanya Supersport ambayo imeahidi kuonyesha 'live' mechi za michuano hiyo.

Wakati huo huo, Dynamos ya Zimbabwe imetupilia mbali mwaliko wa Cecafa kushiriki michuano yake kwa kuwa inajiandaa na mechi za Kombe la Caf dhidi ya Inter-club ya Angola.

Dynamos itacheza mechi yake kati ya Julai 14 na 16 siku ambayo michuano itaanza. Mbali na mechi hiyo, pia inakabiliwa na mechi ya ligi dhidi ya Hwange na Highlanders pamoja na michuano ya Banc ABC Super Eight inayoanza Julai 21.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ray Kazembe alisema kuwa hawataweza kwenda Tanzania kutokana na majukumu hayo.

Mbali na timu hiyo, Musonye alisema pia kuwa wanatarajia Vita Club ya DRC pamoja na   Bloemfontein Celtics, Platinum FC na Silver Stars za Afrika Kusini kushiriki michuano hiyo.

Awali ilielezwa kuwa Orlando Pirates ilialikwa lakini huenda isije kutokana na majukumu ya ligi wakati TP Mazembe iliyoalikwa, imechomoa kwa kuwa inabanwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Kwa sasa tuko katika mchakato kuhakikisha tunapata timu tatu kutoka nje ya ukanda wa Cecafa. nafasi ya timu kuja ni kubwa, na tunapigana kupata timu moja kutoka DR Congo," Musonye alisema.

"Madhumuni ya Cecafa kualika timu hizi ni kuipa sura michuano hii kwa kuwa ni mikubwa katika ukanda huu."

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSIANA NA TUME YA POLISI ILIYOUNDWA NA JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA TUKIO LA DR. ULIMBOKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Tamko la jumuiya ya madaktari kuhusiana na tume iliyoundwa na jeshi la polisi kuchunguza tukio la dr ulimboka.



KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
                                                                                                                                                                                                                
YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012 
Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.
Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.
Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.
Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka, Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.
Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma. Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.
Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.
Imetolewa na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

Bodi ya Hospitali ya Rufaa Mbeya yawasimamisha kazi Madaktari 72

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Madaktari hao ni 54 wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na Madaktari 18 walioajiriwa na Wizara ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

"Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.

Imeelezwa kuwa, siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu (Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19 (Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 imethibitika kuwa Interns Doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012. Tarehe 25/6/2012, bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.

Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali iliwaandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi.

"Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii," alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumla madaktari hao waligomea barua zote mbili, yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti huyo wa bodi alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.

June 28, 2012

BREAKING NUUUZ: KOVA AZUNGUMZIA UTEKAJI WA DK. STEVEN ULIMBOKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo 

Tukio kamili la Kilicho tokea baada ya Dr. Ulimboka kufikishwa hospitalini Madaktari wengi wajitokeza kumpa msaada

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
 Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiisukuma gari iliyokuwa imempaki Dk. Stevan Ulimboka.
 Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompaka mwenzao.


 Wanahabari wakitafuta taswira.










SOURCE: MICHUZI MATUKIO

CHADEMA YALAANI DK. ULIMBOKA KUSHAMBULIWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimelaani kukamatwa na kushambuliwa kwa viongozi wa madaktari ikiwamo Dk Ulimboka Steven ikieleza kuwa hatua hiyo haiwezi kuwa suluhu bali itachochea zaidi mgogoro wa madaktari na Serikali. Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika inaeleza pia kwamba udhaifu wa Serikali kuharakisha kwenda mahakamani kabla ya Bunge kupewa fursa ya kujadili madai ya madaktari na kuisimamia Serikali umelifikisha taifa katika hali iliyopo sasa.

"Nalaani uamuzi wa Serikali wa kutumia vyombo vya dola kukamata na kushambulia viongozi wa madaktari ikiwemo Dk Ulimboka Steven kwa hauwezi kuwa suluhu bali utachochea zaidi mgogoro kati ya madaktari na Serikali," ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo ya Mnyika na kuongeza:

 “Nichukue fursa hii kuwaomba madaktari kufanya kila kinachowezekana kuokoa uhai wa wagonjwa katika kipindi hiki kigumu.” Mnyika alisema kuwa ameomba wabunge wapewe nakala ya Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu madai ya madaktari na hoja ya taarifa husika iwekwe katika orodha ya shughuli za Bunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea ili ijadiliwe na kupitisha maazimio, kuwezesha hatua za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kuupatia ufumbuzi mgogoro huo na kuboresha sekta ya afya nchini.

 “Natarajia kwamba Spika atawezesha kamati kuwasilisha taarifa yake na Bunge kujadili baada ya Serikali kutoa kauli yake bungeni,”alisema.  Mnyika alisema ikiwa wabunge wataelezwa ukweli na kupewa taarifa kamili wataweza kuisimamia Serikali na kuwaeleza ukweli madaktari kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.  

Alisema kuwa ingawa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa maelezo bungeni kuwa Serikali itatoa kauli bungeni kuhusu mgomo huo, Bunge halitaruhusiwa kujadili kauli husika, hivyo kukoseshwa fursa ya kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi.


MADAKTARI WATANGAZA VITA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 (Picha na maktaba)
KITENDO cha kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka, kumeibua hisia kali kwa madaktari waliopo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, huku wakisema kuwa Serikali haiwezi kukwepa kuhusiana na kitendo hicho.

Wakizungumza na Mwananchi, madaktari waliogoma hospitalini hapo huku wakikataa kabisa kuandikwa majina yao walisema, watanzania wanatakiwa kutambua wazi kwamba Serikali imetangaza vita na madaktari hao na kwamba wameitaka Serikali kutolea ufafanuzi yakinifu kuhusiana na kupigwa kwa kiongozi huo.

 Walisema kitendo cha kutekwa kwa Dk Ulimboka, kamwe hawapo tayari kurudi kazini licha ya kuwa baadhi yao walikuwa tayari kurejea kazini lakini kutokana na hilo  hawawezi kumsaliti Ulimboka kwa kitendo alichofanyiwa, na kudai kuwa ndio kwanza  mgomo huo  umeanza rasmi sasa uliopita haukuwa mgomo.

“Kamwe sisi hatupo tayari kurudi kazini tena, kwanza ndio mgomo umeanza rasmi na kutokana na hali hii watanzania watambue wazi kwamba serikali imechoka, tumetoka vijijini tutarudi kulima, lakini hatutamsaliti Ulimboka” alisema mmoja wa madaktari hao huku akitokwa machozi.

Daktari huyo ambaye yupo katika mafunzo ya vitendo alisema kuwa kumpoteza Dk Ulimboka siyo mwisho wa kudai haki kwa kuwa ulimboka ni kiongozi tu na suala la kudai maslahi yao yapo mikononi mwao hivyo wataendelea na harakati zao hadi kitakapo eleweka.
“Kumwagika kwa damu ya Ulimboka  kumetengeneza  akina Ulimboka wengi na damu yake italipwa na sisi kwa kutomsaliti kwa namna yoyote ile na hiyo damu ya mpigaji mwenzetu ndio kwanza imefumbua makucha yetu kuanzia sasa” alisema daktari huyo.

Hata hivyo, Daktari bingwa ambaye pia hakutaka  jina lake liandikwe alisema, kitendo cha kutekwa kwa Dk Ulimboka hata wao ambao hawakuwapo katika mgomo huo sasa, wanaingia kwenye mgomo huo rasmi kwa kile alichodai kuwa ulimboka ni daktari kama wao.

Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania asherehekea miaka 35 ya nchi yake

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiongea machache kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi kutoka sehemu mbalimbali,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo nyumbani kwa balozi huyo,jijini Dar.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo,Pichani kati ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo,wakisherehekea hafla fupi ya  kutimiza miaka 35 ya jamhuri ya Djibout iliyofanyika jioni ya leo jijini Dar.


 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akimpokea mgeni rasmi wa hafla hiyo,Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi alipokuwa akiwasili nyumbani kwa balozi huyo.


 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo  akimkaribisha Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) mara alipokuwa akiwasili kwenye hafla hiyo.


Sir Andy Chande akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi jioni ya leo kwenye viunga vya balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo







HATIMAYE UHISPANIA YATIGA FAINALI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mabingwa watetezi Uhispania wamefuzu kuingia fainali ya Euro 2012, baada ya kuishinda Ureno magoli 4-2, kupitia mikwaju ya penalti, baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 na dakika 30 za ziaida kumalizika kwa timu hizo mbili kushindwa kufungana.

Bao la mwisho la mikwaju ya penalti kwa Uhispania lilitiwa wavuni na Cesc Fabregas, na kuwapa wenzake matumaini ya kutetea ubingwa wao kikamilifu, watakapocheza aidha na Ujerumani au Italia katika fainali ya Jumapili.
Fabregas, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Barcelona, alipiga mkwaju ambao baada ya kugonga mwamba upande wa kushoto, ulitambaa wavuni, na ikawa ni tiketi ya Uhispania kufanya mipango ya kusafiri hadi Kiev, Ukraine, kwa fainali.
Mchezaji wa Ureno, Bruno Alves, alielekea kuwa na wasiwasi, na kushindwa kufunga mkwaju wake, baada ya mpira kugonga mwamba, na Ronaldo, akiwa amepangwa na timu yake katika nafasi ya tano kwa wapigaji penalti, hakupata hata nafasi ya kutimiza wajibu huo.

Wengine waliokosa kufunga kupitia mikwaju ya penalti ni mchezaji wa Ureno, Joao Moutinho, wakati kipa wa Uhispania, Casillas, alipoweza kuokoa kwa kuruka upande wa kkulia.

Awali mchezaji wa Uhsipania Xabi Alonso naye alikosa kutumbukiza wavuni mkwaju wa penalti, licha ya kwamba ulikuwa ni mkwaju wa kasi na uliopigwa kwa nguvu, lakini kipa Rui Patricio akauzuia.

CHANZO:  http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo

KONA YA UDAKU: DIAMOND, WEMA WANASWA HOTELINI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

NDIVYO ilivyokuwa, staa mkali wa filamu Bongo, Wema Sepetu na mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa yupo juu, Nasibu Abdul a.k.a Diamond ‘Plantinum’ wamenaswa katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano Giraffe iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam.
MESEJI YA KWANZA KWENYE SIMU YA PAPARAZI
Asubuhi ya Juni 26, 2012, ujumbe mfupi wa maneno (sms) uliingia kwenye simu ya paparazi wetu ukidondosha madai mazito kuwa, mastaa hao waliowahi kuwa wachumba na baadaye kumwagana kinomanoma, wako kwenye hoteli hiyo ‘wakiponda raha kwani kufa kwaja’.
Meseji hiyo ikafafanua: “Tena wapo toka jana, Wema yeye yupo toka alipomaliza ile shughuli yake na Omotola yule mdada wa Naijeria (Nigeria).”
MAPAPARAZI WAINGIA MZIGONI
Baada ya kupata ujumbe huo, waandishi wetu walikaa kama kamati mbele ya mhariri wao, wakaandaa zana mbalimbali zikiwemo kamera na vifaa vya kurekodia kwa ajili ya kufuatilia ukweli wa meseji hiyo.
GARI LA DIAMOND NJE YA HOTELI
Waandishi wetu walifika hotelini hapo saa 3:46 ambapo nje ya hoteli hiyo, mapaparazi hao walianza kuamini Platinum yupo ndani baada ya kuliona gari lake aina ya Toyota Prado, lakini katika kuzungusha makengeza yao hawakuweza kulitia machoni gari la Wema.
MBELE YA MAPOKEZI YA HOTELI
Mbele ya kaunta ya mapokezi, waandishi waliomba kuonana na Wema Sepetu.
Mtu wa Mapokezi: Nimwambie nani?
Musa: Mwambie baby wake.
Mtu wa Mapokezi: Baby wake yupi?
Musa: Musa Mateja.
Mtu wa Mapokezi alimtwangia simu Wema ambapo alipoambiwa ni Musa Mateja aliamuru asubiri eneo hilo mpaka atakapoitwa kwenda chumbani.
DIAMOND HUYO!
Waandishi wakiwa wamepiga kambi wakisubiri kuitwa, ghafla Diamond alishuka akiwa mbiombio kuelekea kwenye gari lake kama mtu anayewahi. Mapaparazi wetu walimfuata hadi kwenye gari ambapo alikuwa ameshaingia.
MSIKIE ALICHOSEMA
Bila kupoteza muda alisomewa mashitaka yake ‘eituzedi’ ambapo alivuta pumzi kwa nguvu kisha akafunguka:
“Mimi hata sijui kama Wema yupo hapa hotelini, kwani yupo hapa? Chumba namba ngapi? Mimi nilikuja kwenye mambo yangu, kwa sasa natunga mashairi ya wimbo mwingine kwa hiyo nilikuja tangu jana ili kufanya kazi yangu kwa ufanisi, unajua napenda kuwa sehemu yenye utulivu mkubwa.
“Unajua nini, nilikuwa Morogoro, nimerudi jana, nikaja hapa kumfuata Jeff, si unajua yule mshikaji wangu sana? Kuna wakati pia huwa nakuja pale kwenye hoteli moja ipo jirani na ofisini zenu, pale napo pazuri sana, nimewahi kulala. Ha! Ha! Ha! Musa bwana!”
MENEJA WA WEMA
Meneja wa Wema, Martin Kadinda naye alikutana na waandishi wetu ambapo alishtuka kumwona Diamond kwenye gari lake.
Martin: Khaa! Diamond unaweza kuja hapa hotelini halafu unaondoka usinitafute wakati unajua mimi nipo na tuna ishu yetu?
Diamond: (kicheko tu).
WAANDISHI WARUDI MAPOKEZI, WAITWA KWA WEMA
Baada ya kumalizana na Diamond waandishi wetu walirudi mapokezi ambapo walipelekwa kwenye chumba alichomo supastaa mwenye chemchemi za skendo Bongo, Wema na kumkuta akiwa na rafiki yake kipenzi (lakini asiyekubalika na mama yake), Snura Mushi.
Wema, baada ya kusomewa mashitaka yake alishtuka sana na kuonesha mshangao kusikia Diamond alilala hotelini hapo.
Alisema kuwa yeye ndiyo kwanza yuko kitandani na alikuwa amelala na Snura, habari ya Diamond kuwepo hotelini hapo anasikia kutoka kwa mapaparazi lakini yeye hajui chochote.
“Jamani mnavyoniona mimi hapa ndiyo kwanza nimeamka, hata nje sijatoka na watu wa kwanza kuongea nao ni nyinyi, mimi sijui kabisa kama huyo mtu yuko hapa. Kwanza alifuata nini hapa jamani?”
Amani: Sisi tulivyosikia alikuwa na wewe, sasa wewe tena unatuuliza sisi, tutajua vipi? Si ndiyo maana tumekuja?
Wema: Jamani kusema kweli… (akachukua simu na kumpigia mwanaume aliyedai ni mpenzi wake) dady, wamekuja waandishi hapa wanasema wamesikia nimelala na Diamond, we si tumeongea hadi usiku sana?
MASWALI MAGUMU
Inawezekana Diamond akafika hotelini hapo bila Wema kuwa na taarifa?
Ni kweli kwamba, Wema aliweka kambi pale kwa lengo la kujipumzisha tu akiwa na shoga yake Snura?
Utulivu anaodai Diamond aliufuata pale hotelini ulikosekana sehemu nyingine yoyote (hasa nyumbani) ikiwemo ufukweni?
Kwa nini Wema aliharakisha kumpigia simu huyo aliyemuita mpenzi wake kumwambia kuhusu waandishi kufuatilia habari ya kulala na Diamond wakati akidai walizungumza hadi usiku sana?
UKWELI UPO KWA WEMA, DIAMOND
Kwa maelezo yao hayo, bado ukweli unabaki kuwa siri yao. Hata hivyo, penzi halina siri, kama wanaficha, mapaparazi wapo macho kuwafuatilia na kama ni kweli wanatoka, siku moja mambo yatakuwa hadharani.

CHANZO: GLOBAL PUBLISHER

MWAKYEMBE AKAGUA MAGARI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu Manispaa ya Morogoro na kufanya ukaguzi wa mabasi ya abiria ambapo  mabasi matatu aliyaamrisha yalipe faini ya Sh250,000 kila moja kutokana na makosa mbalimbali likiwamo la kutokuwa na dereva wa akiba.

Ziara hiyo aliifanya mapema wiki hii  asubuhi kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambapo lengo la waziri huyolilikuwa kukagua mabasi yanayofanya safari za mikoani na nje ya nchi na kuona kama yanakidhi vigezo vya Sumatra katika shughuli ya kusafirisha abiria.

Katika ziara hiyo, Dk  Mwakyembe alifika katika kituo hicho cha mabasi na kuegesha gari mbali kidogo kisha kuelekea kwenye mabasi huku akijifanya abiria na kuingia ndani ya mabasi hayo kisha kuanza kukagua leseni za madereva na vitambulisho vya kampuni za mabasi wanavyotumia madereva.

Ukaguzi mwingine alioufanya ni ratiba za safari pamoja na usalama wa mabasi na baadaye Dk Mwakyembe aliamrisha madereva walioonekana kuwa na makosa kulipa faini Sumatra.

Mabasi yaliyolipishwa faini ni pamoja na Royal Coach linalofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba ambalo dereva wake hakuwa na kitambulisho cha kampuni, basi la Super Najimunisa na Muro Investiment yanayofanya safari zake Dar es Salaam kuelekea Mwanza ambapo mabasi hayo yalikuwa na kosa la kutokuwa na dereva wa akiba.

Baada ya kubaini makosa hayo Waziri Mwakyembe aliwataka madereva ambao walionekana kuwa na makosa kulipa faini ya papo hapo kwa Sumatra, vinginevyo aliwataka Sumatra kuwafikisha mahakamani hata hivyo madereva hao walikubali kulipa faini hiyo waliwasiliana na wamiliki wa mabasi wanayofanyia kazi.
Akizungumza na maofisa wa Sumatra pamoja na madereva, Dk Mwakyemba alisema makosa kama hayo yanaweza kusababisha ajali za barabara na hivyo kupoteza maisha ya watu, kusababisha ulemavu wa kudumu kwa abiria.

Alisema pia ajali zinasababisha uharibifu wa  mali na kwamba ataendelea kufanya ziara za namna hiyo mara kwa mara ili kubaini makosa mengine.

Aidha aliwataka Sumatra pamoja na kikosi cha usalama barabarani kusimamia sheria za usalama barabarani na kutowaonea aibu madereva watakaonekana kuwa na makosa kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa ni tishio hapa nchini.

Kwa upande wake, mkuu wa usalama barabarani mkoani hapa, Leonard Gyindo alisema kuwa kikosi cha usalama barabarani kimejipanga katika kudhibiti ajali za barabarani kwa kufanya ukaguzi kabla ya gari halijaondoka katika kituo hicho.

Gyindo alimpongeza Waziri Mwakyembe kupitia Wizara ya Uchukuzi kwa jitihada zake katika kusimamia sheria hasa za usalama barabarani na kuahidi kuwa kikosi cha usalama barabarani kitampa ushirikiano na kutekeleza maagizo yote atakayotoa.

Kwa upande wa wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya ziara hiyo walimwomba Waziri huyo kufanya ziara nyingine kituoni hapo hasa nyakati za usiku na kushuhudia hali ya giza lililopo katika kituo hicho.

JANA MAANDALIZI YA MABANDA KABLA YA KUANZA KWA MAONYESHO YA BIASHARA YA SABASABA RASMI LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mafundi wakiendelea na usafi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya maonyesho ya biashara vya Saba Saba jijini Dar es salaam JANA ambapo maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza rasmi  juni 28/ 2012.
 Msimamizi wa banda la Home Shopping Centre BW.Faiz Mahamood Said akiongea na waandishi wa habari leo katika banda hilo viwanja vya SABA SABA pia Bw.Faiz Mahamood Said alisema amewataka washiriki wa maonyesho hayo kujitokeza wa kwa wingi pia watembelee banda la Home shopping centre wajionee bidha mpya mbalimbali.
 
Mafundi wakiweka bango katika banda la kampuni ya simu TTCL katika viwanja vya saba saba 
 Mafundi wakiweka mabango katika viwanja vya maonyesho ya biashara vya Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat