StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

October 31, 2012

HILI NDILO TUKIO ZIMA LA WANAFUNZI WA SEKONDARI WALIONDAMANA JANA WAKAPIGWA MABOMU NA KUOKOTA MOJA LIKIWA HALIJALIPUKA MJINI ARUSHA JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KAMANDA wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, akiwa amemnyang'anya bomu
hilo, mwanafunzi huyo, baada ya kuonyesha, huku akisikika akisema
halijalipuka na ni hatari kuendelea kulishika, sababu lilianguka kwa
bahati mbaya


MMOJA wa wanafunzi hao ambaye hakujulikana jina lake mara moja, akiwa
anaonyesha wenzake bomu linalodaiwa kutolipuka, mbele ya Mkuu wa Mkoa
Arusha,ambalo alidhani ni ganda limeangkuka baada ya kulipuka.


WANAFUNZI wakiwa mbele ya jengo la Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa
mulongo, wakimsubiri kumpa malalamiko yao.

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kimnyaki, Wilayani Arumeru, wameandamana wakiwa na mabango mbalimbali hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na kusababisha vurugu kubwa kutokea barabara ya Ngaramtoni, nje kidogo ya Jiji la Arusha, hali iliyolazimisha jeshi la Polisi kutumia nguvu kwa kuwatawanya kwa kuwapiga mabomu ya machozi.

Aidha katika vurugu hizo, mmoja wa wanafunzi aliokota bomu lililokuwa halijalipuka, akidhani kuwa ni ganda la bomu lililotumika, huku akimwonyesha mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, hali iliyosababisha Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla kumnyang’anya haraka, kabla ya kuleta madhara.

Maandamano hayo yalikuwa ya kushikiza kufukuzwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule Marium Chamle kwa sababu ya kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha nne kutoingia chumba cha mitihani.

Blog hii ilishuhudia wanafunzi hao katika hali isiyo ya kawaida kila mmoja alikuwa na chupa ya maji, ambayo walikuwa wakinawa wakati wa mabomu hayo na kusonga mbele hadi ofisi hizo. Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa mulongo,kwa niaba ya wenzake, Mesharck Lomnyaki alisema mwalimu mkuu huyo amesababisha baadhi wa wanafunzi wa kidato cha nne kuchelewa kufanya mitihani yao ya baraza la mitihani (NECTA), kwa kuzuia kuingia katika chumba cha mitihani toka saa mbili asubuhi na kuwaruhusu kuingia saa 4.30.

Aidha alisema Oktoba 16 mwaka huu, walinyimwa mwongozo wa kujibu swali la tano, lenye alama kumi, kwenye somo la Chemia , ambao hawakupata kulingana na muda na kusababisha usumbufu ndani ya chumba cha mtihani na kusababisha kukata tamaa kwenye somo la Fizikia. Pia alidai tatizo la kufanana na hilo limejitokeza kwa wanafunzi wa kidato cha pili, kwenye mtihani wa Moko, ambapo aliwafukuza wanafunzi hao kutomaliza mtihani huo, kwa sababu ya kutolipa michango na kusababisha wanafunzi 46 kutofanya kabisa mtihani huo. Alisema matokeo ya kuzuia wanafunzi hao yalisababisha kushuka kwa
kiwango cha ufaulu, hali iliyosababisha mwalimu huyo kutoa lugha za kashfa na kujenga woga kwa wanafunzi  hao wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili, utakaofanyika mwaka huu.
“Lakini tunasikitika badala ya kutusikiliza kero zetu, Polisi wanatupiga mabomu barabarani ili tusiandamane na baadhi yetu tumeokota ganda hili hapa la bomu,”alisema Mara baada ya kuonyesha ganda hilo, ndipo Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, aliposhituka na kumnyang’anya bomu mtoto aliyeshika, akidai hilo lilikuwa ni bomu halikulipuka na lilikuwa na hatari ya kulipuka endapo lingeshikwa shikwa kwenye chuma maalum cha kushitua.
Alisema bomu hilo lilianguka kwa bahati mbaya, katika vurugu za kuwatuliza kuandamana, ambapo wanafunzi hao waliwapiga mawe Polisi hao na kulazimisha kutumia nguvu ndogo tu ya kujaribu kuwatuliza, lakini hawakusikia, waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Naye mwanafunzi mwingine Ezekiel Memiri, alitaja kero zingine kuwa ni unyanyasaji wa wanafunzi, ambapo wengi hufukuzwa kwa makosa madogo
madogo, bila udhibitisho wa bodi ya shule. “Hili limesababisha wanafunzi aidi ya 20 kufukuzwa shule na baadhi kusimamishwa na baadhi ya waalimu kuwatumikisha wanafunzi majumbani mwao kwa kuwafulia nguo hadi za waume zao,”alisema.
Alisema kutokana na hilo wameomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati na kumbadilisha Mkuu wa shule hiyo kwa sababu matokeo yao yanazidi kushuka kitaaluma. Naye Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo, aliwasikilia wanafunzi hao, huku akigeuka kuwa mbogo na kuamuru Polisi kukamata wanafunzi wao wawili waliokuwa wanatoa maelezo kwa niaba ya wenzao ambao ni Mesharck Lomnyaki na Daudi aliyeptikana jina moja, kwa madai wao ndio viongozi wa maandamano hayo .
Alisema kuwa kwa sasa anashangaa kumezuka tabia ya wanafunzi shuleni Mkoani Arusha kuandamana hata kwa makosa yasio na sababu hadi ofisini kwake jambo ambalo amelikemea na kutoa onyo kwa shule zote Mkoani hapo kuacha tabia hiyo vinginevyo atazifungia. “Shule zitakazoandamana kuanzia leo nitazifungia ili mkose kabisha masomo, maana hamtaki kusoma na leo ningefanya hivi, lakini nimeonea huruma watoto wa kike walio wengi ambao tunapigania wapate elimu, ila hawa viongozi wenu wapelekwe ndani iwe fundisho la tabia hii,”alisema. Mulongo alitoa hadi kufika saa tisa jioni ya jana, wanafunzi hao wawe wamerejea shuleni kwao, kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Elimu, vinginevyo atawafungia shule yao.

“Nashangaa kupigwa mabomu, mnashangaa nini wakati mmeandamana bila kibali, mlitegemea nini mnavunja sheria na mkivunja sheria kwa kudai haki, hata haki mnayotaka hamtapata,sababu ya kuvunja sheria”alisema.

Hata hivyo ilichukua muda wanafunzi hao kutawanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao wawili waliokamatwa na Polisi, hadi pale Polisi walipoamua kutoweka kwa gari namba PT. 1834 na kuwaacha kwenye mataa wanafunzi hao wakibaki hawana cha kufanya,zaidi ya kuondoka hadi makao Makuu ya Polisi kusubiri wenzao kuachiwa.

PICHA ZA MAZISHI YA THOMAS MADIGAGE, KOCHA MSAIDIZI WA BAFANA BAFANA YA AFRIKA KUSINI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends











Bwana Gordon Igesund kocha wa Bafana Bafana akimwaga machozi



Marehemu Thomas madigage alikuwa kocha msaidizi wa Bafana Bafana timu ya taifa South Africa, Madigage amefarikiki kwa ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 41 na kuzikwa Limpopo, South africa.

WAZIRI WA ELIMU DR. SHUKURU KAWAMBWA KATIKA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA SHULE YA MSINGI ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akila chakula cha mchana na wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha. alipofanya ziara ya kushtukiza ,kujionea huduma za chakula inayotolewa kwa wanafunzi shuleni hapo.


Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akifurahia chakula cha mchana na wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha.


Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akijilamba chakula cha mchana na wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha.Huku waandishi wa habari wakipata matukio.

SERIKALI YASALIMU AMRI JUU YA MAFAO YA KUJITOA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Hatimaye, Serikali imesalimu amri na kukubali yaishe baada ya kufuta tangazo lake la Agosti mwaka huu la kusitishwa kwa fao la kujitoa.
Hata hivyo, habari zilizopatikana zinaeleza kuwa hatua hiyo ya Serikali inatokana na kelele za wabunge na wanaharakati ambao kwa zaidi ya miezi miwili, wamekuwa wakihoji juu ya sheria hiyo.
Suala hilo la fao la kujitoa liliibuka katika kikao cha wabunge wakati wakipewa taarifa ya shughuli za Bunge katika Mkutano huu unaendelea kilichokaa jana mchana katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Spika Anne Makinda alilitolea ufafanuzi kwa kueleza kuwa Serikali itawasilisha muswada bungeni kufanya marekebisho ya fao hilo.
Jaffo ambaye alikuwa amewasilisha kwa Spika kusudio la kuwasilisha hoja binafsi kupinga kuondolewa kwa fao hilo, alimwambia mwandishi wetu jana kuwa amepokea barua ya kumpa taarifa kuwa Serikali itawasilisha bungeni muswada wa marekebisho.
Alisema marekebisho hayo yataruhusu mifuko yote ya jamii kuendelea kutoa mafao ya kujitoa kama ilivyokuwa awali.
Mbunge huyo alisema amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Serikali ili wafanyakazi waendelee kunufaika na mifuko hiyo ya jamii.
“Nashukuru kilio changu kimesikilizwa na Serikali kwangu mimi huu ni ushindi, kwani wafanyakazi wengi nchini hawana kazi za uhakika,” alisema
Alisema wafanyakazi wengi hususan wa sekta ya madini, hawana uhakika wa ajira hivyo kuondolewa kwa fao la kujitoa kungewapa wakati mgumu.
Mnyika pia alikuwa amewasilisha kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kupinga fao la kujitoa kuondolewa katika bunge hili.
Katika Mkutano wa Nane wa Bunge, Jaffo alipinga sheria hiyo ya kufuta fao la kujitoa alipoomba mwongozo wa Spika na mara baada ya kuwasilisha hoja zake, aliungwa mkono na wabunge wengi isipokuwa Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola ambaye alisimama na kutetea sheria hiyo.

chanzo: Mwananchi

PICHA ZA TAARIFA YA MTOTO WA DARASA LA TATU ALIYEJINYONGA MPAKA KUFA KWA KAMBA ZA VIATU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8) jinsia ya kiume ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao. (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)




Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.

Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila (52) na Bi Subira Patrick (30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick (10) waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.

Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga Bwana Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.


Mama mzazi wa marehemu Kervin Patrick (8)Bi Subira Patrick(38) akiwa katika hali ya majonzi kufuatika kifo cha mwanae aliyejinyonga. (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)

Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8), (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)

TAARIFA KAMILI KUHUSU MBUNGE JOSHUA NASARI KUFYATUA RISASI SIKU YA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari

MBUNGE wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amekanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika jana ambapo mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.

Nassari ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.

Nassari amedai kuwa katika uchaguzi wa jana yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!

Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usala avinavyohusika na maswala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.

October 30, 2012

Ajali ya kutisha ya Nsa Job!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


MPIRA tena basi mimi! Ndivyo alivyosikika mshambuliaji wa Coastal Union, Nsa Job akilia kwa uchungu alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuteguka mguu wa kushoto baada ya kugongana na kipa wa JKT Ruvu, Patrick Muntari katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi.

Aliumia sehemu ya chini ya goti na kusababisha mguu kupinda lakini amefanyiwa matibabu na kuwekewa bandeji ngumu (P.O.P).

Ilikuwa katika dakika ya 66, Nsa alipokuwa akifanya mashambulizi kwenye lango la Kaskazini la uwanja na kukutana uso kwa uso na Muntari.

Tukio hilo liliibua madudu ya udhaifu wa uendeshaji wa Ligi Kuu kwa mechi ambazo hazifanyiki Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hakukuwa na gari la wagonjwa (ambulance) hali iliyosababisha mchezaji huyo asote uwanjani hapo kwa zaidi ya nusu saa huku ukitafutwa usafiri wa kumfikisha hospitali baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Hata hivyo, huduma ya kwanza aliipata katika zahanati ya klabu ya Azam ambayo timu hiyo huitumia kuwahudumia wachezaji wake wanapopata matatizo.

Inashangaza kuona mechi za ligi zinachezwa bila kuwepo kwa gari la wagonjwa na kuna siku maafa makubwa zaidi yanaweza kutokea katika viwanja vya soka.

Hata hivyo, baada ya Nsa kupata huduma ya kwanza, alipelekwa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) kwa msaada wa gari binafsi huku wakisindikizwa na gari la polisi ili kukwepa msongamano wa magari.

Nsa anavyoelezea
"Ilikuwa mbaya, nimelia sana nilikuwa nasikia maumivu makali mno kwenye mguu na niliteseka zaidi barabarani nilipokuwa nakwenda hospitalini pale gari ilipokuwa likidunda kwenye mashimo,"anasema Nsa ambaye alishuhudiwa na Mwanaspoti katika chumba cha huduma ya kwanza akilia maumivu kama mtoto.

"Lakini kilio kingine nilikuwa nawaza maisha yangu, huenda mpira kwangu ndiyo basi tena kila nilipokuwa nauangalia mguu wangu ulivyopinda, lakini nashukuru kwa sasa baada ya kupatiwa matibabu maumivu yamepungua,"anaeleza Nsa, ambaye alikaa MOI kwa saa nne juzi Jumapili usiku akipatiwa matibabu na baada ya hapo alirudishwa kwenye hoteli iliyofikia ili kujiunga na wenzake.

Taarifa rasmi kuhusu Balotelli kumuibukia upya Nicki Minaj

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


NYOTA wa Manchester City, Mario Balotelli amepanga kukutana na mwanamuziki Nicki Minaj Ijumaa wiki hii baada ya kushindwa kuonana naye wiki iliyopita.

Mwanamuziki huyo atafanya shoo katika Ukumbi wa MEN Arena Jumaa hii na Balotelli ambaye alilia kukutana naye bila mafanikio, atahakikisha wanaonana.

Habari zinasema kuwa nyota wa Manchester City alitaka kukutana na Nicki Minaj, lakini mwanamuziki huyo alikataa kwa kuwa alikuwa amechoka na pia alikuwa na hasira.

Minaj alitumbuiza katika ukumbi wa News (MEN) Arena wiki iliyopita na Balotelli aliwasili katika shughuli hiyo akiwa na rafiki zake.

Kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo alipanga kukutana na nyota huyo kabla ya shoo lakini Minaj aligoma "Mario alisikitishwa na kitendo hicho," alisema mtu wake wa karibu.

Imefahamika kuwa Mario mwenye miaka 21 alikuwa ameandaa kamera kwa ajili ya kumpiga picha dada huyo lakini mambo hayakwenda vizuri.

Balotelli ni nyota katika soka lakini umaarufu huo haukutosha kumtoa ndani Minaj.

Huyu ndiye Binti aliyewagonganisha Ronaldo, Boateng

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MADRID, HISPANIA
HABARI kutoka Hispania zinasema kuwa Kevin-Prince Boateng amemtaka Cristiano Ronaldo aache kuwasiliana na mpenzi wake, Melissa Satta.

Mwanzoni mwa mwezi huu kulikuwa na habari kwamba nyota wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid alikuwa akiwasiliana na mwanamke huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu lengo likiwa ni kumnasa kimapenzi.

Lakini watu wa karibu na Boateng wamesema kuwa mchezaji huyo hajafurahishwa na jambo hilo na amemtaka Ronaldo aache tabia hiyo.

Habari zilizochapishwa katika gazeti la Novella 2000 la Italia zinasema kuwa katika siku za karibuni mchezaji huyo alionekana akiomba namba ya dada huyo.

Cristiano Ronaldo ni mpenzi wa Irina Shayk ambaye amekuwa naye kwa miaka miwili sasa.

Boateng anatarajia kufunga ndoa na Satta mwakani.

Picha na habari za kimbunga kilichoua watu 16

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy huko nchini Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokana na watu hao kuangukiwa na miti.

IDADI ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy huko nchini Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokana na watu hao kuangukiwa na miti.

Vifo hivyo kwa ujumla wake vimeripotiwa katika majimbo ya New York, New Jersey, West Virginia, Connecticut, Pennsylvania na Maryland. Lakini kuna vifo vingine pia vimeripotiwa kutokana na kukatika kwa umeme na ajali ya gari katika balaa la kimbunga hicho.

Kuna ripoti ya mwanamke mwingine kufariki dunia kutokana na kimbunga hicho na mwili wake kuonekana ukielea katika maeneo ya bahari,huko Toronto nchini Canada jumapili. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha CNN Kimbunga hicho mpaka sasa kimeacha zaidi ya raia milioni 6.5 nchini Marekani pasipo nishati ya umeme katika eneo la Pwani ya Mashariki.

New York yaathirika zaidi
Vehicles are submerged on 14th Street near the Consolidated Edison power plant, Monday, Oct. 29, 2012, in New York. Sandy continued on its path Monday, as the storm forced the shutdown of mass transit, schools and financial markets, sending coastal residents fleeing, and threatening a dangerous mix of high winds and soaking rain. (AP Photo/ John Minchillo) Jiji la New York

New York ni miongoni mwa mji ulivurugwa vibaya na kimbunga hicho ambacho rekodi zinaonesha kiliambatana na mawimbi ya urefu wa meta 4 katika eneo la kusini la Manhattan. Katika eneo hilo maji yalifurika mpaka katika njia kubwa kabisa ya reli. Na soko la hisa la New York limeendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo.

Duru nyingine zinaeleza kwamba moto uliowaka usiku kucha umeteketeza takribani nyumba 50 katika kitongoji cha Queens. Taarifa hizo zimesambazwa na kitengo cha zimamoto kupitia ukurasa wake wa Twiter ambapo hata hivyo hakikutoa maelezo zaidi kufuatia mkasa huo. Lakini kama inavyofahamika kwamba mkasa huo umetokea baada ya kimbunga Sandy kuyakumba maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani ukiwemo mji wa New York.

Hata hivyo balaa la kimbunga hicho bado halijafika kikomo ambako wasiwasi bado upo katika maeneo ya mbali ya majimbo ya Wisconsin na Ilinois. Ishara ya tahadhari imetolewa kuanzia Chicago mpaka Maine na Canada mpaka Florida. Tahadhari hiyo inaonesha kimbunga Sandy kitaendelea kuwa tatizo katika siku kadhaa zijazo na kitaambatana na mvua kali, theluji na mafuriko. Wakaazi walio katika eneo la Michigan na Ontario wametahadharishwa kuwepo kwa mawimbi makubwa. Na pia theluji zaidi kama ilivyo katika baadhi ya maeneo ya Atlantik ya kati.

Hali hiyo imezorotesha kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani ambapo Rais Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wanafuatilia kazi ya uokozi katika maeneo ya yalikumbwa na kimbunga hicho.

Serikali yaridhia Wafanyakazi kujitoa kwenye Mifuko ya Jamii

Tweeted this Like this, be the first of your Friends BAADA ya wafanyakazi na baadhi ya wabunge kulalamikia Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 inayozuia mwanachama kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, Serikali imeridhia wafanyakazi kujitoa kwenye mifuko hiyo na kupewa mafao yao kama ilivyokuwa awali.

Chanzo cha habari kutoka serikalini, kimebainisha kuwa katika mkutano wa tisa wa Bunge la 10 unaoanza leo, Serikali itawasilisha tamko lake la kuruhusu fao hilo la kujitoa.

Taarifa hizo zinabainisha, kuwa Tamko la Serikali litakalotolewa bungeni, litafuta barua ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka iliyobainisha kuwa Serikali imefuta fao hilo la kujitoa na kuzuia wanachama kuchukua mafao yao.

“Serikali imeona kisheria haiwezekani kuzuia mfanyakazi kujitoa kwenye mfuko wowote, hivyo imeamua kuwasilisha taarifa yake rasmi ya kufuta muswada wake iliokuwa iuwasilishe ambao ulionekana una upungufu na hivyo kuifuta barua ya SSRA,” kilisema chanzo cha habari.

Barua ya SSRA itakayofutwa na tamko hilo, iliyokwenda kwenye mifuko hiyo ya hifadhi za jamii, ilikataza wafanyakazi kupewa mafao wanapojitoa hadi watimize miaka 55 ya kustaafu kwa hiari au kwa lazima miaka 60.

Gazeti hili (HabariLeo) Jumatatu Oktoba 29, 2012 lilipomtafuta Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka kwa ajili ya ufafanuzi, simu zake hazikupatikana.

Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alipoulizwa kuhusu taarifa za fao hilo kuwasilishwa bungeni alikataa kusema lolote, akidai taarifa za shughuli za Bunge zitatolewa leo kwa wabunge na waandishi wa habari na hapo ndipo itakapojulikana.

Hatua ya Serikali imekuja baada ya Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jafo (CCM), kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka Bunge liazimie kuitaka Serikali iruhusu fao la kujitoa liendelee.

Hata hivyo, wabunge waliazimia mambo manane ikiwamo fao hilo la kuzuiwa kujitoa lirekebishwe pamoja na barua ya Mkurugenzi Mkuu wa SSRA kufutwa.

Mbali na hoja binafsi pia Jafo alitaka kuwasilisha muswada binafsi wa kutaka fao hilo lirejeshwe, lakini muswada huo ulikataliwa kwa sababu Azimio la Bunge lilishapitishwa na kamati inayohusika na masuala ya hifadhi ya jamii ndiyo ilitakiwa ipeleke muswada.

Hata hivyo Jumatano iliyopita, wabunge walipewa muswada wa Serikali wenye lengo la kuufanyia marekebisho Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 lakini marekebisho hayo yalihusu Mfuko wa Pensheni wa PPF pekee, kuruhusu wanachama kujitoa na kupewa mafao.

Mbunge Jafo aliliambia gazeti hili kwamba; “muswada huo tuliona una upungufu na hatukukubaliana nao, kwani ulikuwa unaletwa bila hati ya dharura, maana yake utasomwa kwa mara ya kwanza na baadaye Bunge lijalo utasomwa tena, lakini tumepanga kesho (leo) tupinge hilo.”

Hata hivyo, tayari Serikali imeonekana kubaini upungufu wa muswada huo na ndiyo maana inatarajia kueleza wabunge nia ya kupeleka tamko bungeni kuruhusu wafanyakazi kujitoa na kupewa mafao kama ilivyokuwa awali kabla ya aheria hiyo ya mwaka 2012.

Minja alisema jana kuwa, Kamati ya Uongozi chini ya Mwenyekiti wake, Spika Anne Makinda imeshakaa na kupanga shughuli za Bunge na leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, vikao vya kamati mbalimbali za Bunge na za vyama vya siasa zitakutana na baadaye wabunge wataelezwa ratiba ya shughuli za Mkutano wa Tisa wa Bunge la 10.

October 29, 2012

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU HATIMA YA MWANAHALISI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bidamu (THRD-Coalition), wadau wanaounda mtandao huu na mwanachama mwanzilishi wa Mtandao likiwa ni shirika lenye majukumu ya ya kutetea uhuru wa habari kusini mwa Afrika (MISA-Tan) tunaendelea kwa pamoja kuonyesha kusikitishwa kwetu kwa kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi.

Kwa mara kadhaa sasa tunawakutanisha tena lengo likiwa ni kuendelea kuishawishi serikali ilifungulie gazeti la Mwanahalisi. Kwa vile hoja yetu ya kutaka kuliona gazeti la Mwanahalisi likiwa mitaani haijatimia basi na sisi kwa upande wetu kazi yetu bado haijatimia.

Tunatambua umuhimu wa kuheshimu sheria za nchi, lakini kwa upande mwingine tunaona kwamba ipo haja ya sisi watetezi wa haki za binadamu kupitia kwenye vyombo vya habari na pia kwenye mashirika mengine yanayounda mtandao huu kuishawishi serikali kuachana na sheria gandamizi ambazo ni za kidikteta kama sheria hii ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo hukiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora. Pia kwamba maendeleo ya kiteknolojia na kisiasa hapa nchini yanaiweka rehani sheria hiyo gandamizi.

Tumebaini kuwa kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi siyo tu kwamba kunawaathiri kwa kiwango kikubwa wasomaji wake ndani na nje ya nchi bali pia kunaathiri uhuru wa kutafuta, kupata na kueneza habari, kunawaathiri waajiriwa wa gazeti hilo na familia zao na pia kunaiweka katika hati hati hata kampuni nzima ya Halihalisi ambayo ndiyo mchapishaji wa gazeti hilo.

Tunaendelea kusisitiza kuwa sababu walizotumia viongozi wa wizara ya habari kulifungia gazeti la mwanahalisi sio za kweli kwani kilichoandikwa na Mwanahalisi ni ukweli mtupu ambao hivi karibuni umethibitishwa na tamko la Dr Steven Ulimboka.

Pia, hivi karibuni Dkt Stephen Ulimboka, kupitia kwa wakili wake Mheshimiwa Nyaronyo Kicheere aliweka wazi kwamba Afisa wa Usalama wa Taifa Ramadhan Ighondu alihusika katika kutekwa kwake kwa kuwa mazingira yote kabla na baada ya tukio yanaonyesha wazi kuwa Ramadhani Ighondu ni mdau katika tukio hili.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba baadala ya serikali kutoa tamko kwamba sasa imepata uhakika kwamba afisa wake alikiuka kanuni za ajira yake na ingeaza rasmi kuwasaka washirika wa afisa hiyu jambo hilo halijatokea mpaka sasa huku gazeti hili lililosidia kubainisha ushahidi likifungiwa. Zaidi, tulitegemea serikali ingemkana afisa huyo kwamba siyo mwajiriwa wake katika idara hiyo, kama hivyo ndivyo ilivyo, au vinginevyo tungeitarajia serikali itangaze kwamba inachukua hatua za kisheria dhidi ya afisa huyo ambaye ametajwa kuhusika katika makosa ya jinai kinyume cha utaratibu wa mwajiri wake. Pia tungetemea Jeshi la polisi lingetumia fursa hii kumkamata mshukiwa huyu wa Usalama wa Taifa na kulisadia Jeshi la Polisi kuwapata wale waliotekeleza udhalimu huu dhidi ya Dr Steven Ulimboka. Kwa namna yoyote vitendo vya aina hiyo vinaiabisha serikali na haviwezi kuwa sehemu ya utawala bora ambao serikali yetu imekuwa ikitangaza kwamba inauzingatia.

Mpaka sasa kumekuwapo na matamko mbali mbali kutoka kwa wadau, viongozi wa kiroho, mabalozi na hata Baraza la Habari Tanzania (MCT) likiwa peke yake na hata kwa kushirikiana na wadau wengine wakilaani kufungiwa kwa gazeti hili lakini serikali imeendelea kuwa kaidi katika hili.

Tunachosisitiza

1. Kwa Serikali

Tunaendelea kuwasihi viongozi wa nchi waone sasa umuhimu wa kukutana na viongozi wa Hali Halisi na kujadili namna ya kulifungulia gazeti hili kwani tayari Dr Steven Ulimboka ameshaweka wazi kilichoandikwa na Mwanahalisi ni cha kweli kabisa. Serikali itambue kuwa suala hili sio dogo katika anga za kidemokrasia na haki za binadamu kwani ubabe wa baadhi ya viongozi serikalini leo unaweza iweka nchi pabaya siku za usoni.

2. Vyombo vya Habari

Vyombo vya habari pamoja na taasisi mbalimbali katika tasnia ya habari tuweke tofauti zetu pembeni na kuungana kwa pamoja katika hili na kuhakisha kuwa ukandamizaji wa uhuru wa habari kama huu wa wazi wazi haupati nafasi katika enzi hizi za uwazi na ukweli. Vyombo na taasisi mbalimbali za habari bado mna nafasi na uwezo mkubwa katika kuhakisha gazeti la Mwanahalisi halipotei katika tasnia ya habari hapa nchini.

3. Jumuiya ya Kimataifa

Kwa kuwa mmekuwa wadau wakubwa wa maendeleo na utekelezaji wa haki za binadamu hapa nchini, tukiwa tunaendelea kuuthamini mchango wenu, tunawasihi muendelee kuishawishi serikali kwa njia za kidiplomasia kuhusu suala la kuheshimu kazi za watetezi haki za binadamu na uhuru wa habari. Nafasi zenu za kidiplomasia na uhusiano mkubwa mlionao na nchi ya Tanzania inaweza pia kutumika kushawishi viongozi wa Tanzania walifungulie gazeti la Mwanahalisi.

Kutokana na hali ilivyo ya uvunjifu wa haki za watetezi wa haki za binadamu ikiwamo haki ya kutoa habari, MISA-Tan, mwanachama wa THRD-Coalition anaehusika na uhuru wa habari inaandaa mkutano wa siku moja utakaowakutanisha wadau mbalimbali katika tasnia ya habari ili kujadili hatma ya gazeti la Mwanahalisi na uhuru wa habari nchini.

Mwisho Tunawasihi wanaharakati, watanzania wote wasichoke wala wasirudi nyuma katika azma hii ya kutetea haki, uhuru na ulinzi kwa haki na watetezi wake. 

MATOKEO YA CHAGUZI ZA UDIWANI SEHEMU MBALI MBALI OCTOBA 2012

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Daraja Mbili-ARUSHA

Katika matokeo kamili ya uchaguzi wa Udiwani wa kata ya Daraja Mbili, CHADEMA wameweza kushinda kwa kupata kura 2193 , CCM kura 1324, CUF kura 162, TLP kura 42 na NCCR mageuzi kura 22.

Waliojiandikisha ni wananchi elfu kumi na sita mia mbili tisini na tano, waliopiga kura wapo 3,770, zilizo halali ni kura 3,743 na zilizoharibika ni 27.



KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbrod Slaa akijumuika kucheza ngoma ya kisukuma iliyokuwa ikitumbuizwa na katika Kijiji cha Lubili, Misungwi, Mwanza. Dkt. Slaa alifika kijijini hapo akiwa katika mizunguko ya mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Kata ya Lubili. Anayeonekana kushoto akishangilia kwa kupiga makofi ni Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere. 





BASTOLA NJE NJE UCHAGUZI ARUSHA, RISASI ZARINDIMA HEWANI

UCHAGUZI mdogo wa udiwani katika kata ya Darajambili Mkoani Arusha leo umeingia dosari baada ya risasi kurindima hewani mfulululizo asubuhi ya leo karibu na maeneo ya kupigia kura hali iliyozua taharuki kwa wakazi wa kata hiyo waliokuwa wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Risasi hizo zinadaiwa kupigwa na mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari pamoja na mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) wilayani Arusha,Godfrey Mwalusamba mara baada ya kuibuka tafrani baina ya wafuasi wa CCM na Chadema katika eneo la Shule ya sekondari ya Felix Mrema.

Katika vurugu hizo dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Haleluya Natai pamoja na wafuasi wa Chadema zaidi ya 15 walikamatwa na jeshi la polisi huku Nasari na aliyekua mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema wakitokomea kusikojulikana lakini kisha baadaye walionekana katika viunga vya kupigia kura.

Hatahivyo,katika hali isiyo ya kawaida naye mgombea wa Chadema katika kata hiyo,Prosper Msofe alionekana akirandaranda katika vituo vya kupigia kura huku akiwa na silaha yake aina ya bastola kiunoni hali ambayo ilizua mshangao kwa wapiga kura wa kata hiyo.

Katika vurugu hizo inadaiwa kuwa Nasari aliyekuwa akiongozana na lema wakiwa katika gari mojawapo walivamia ngome ya CCM iliyopo karibu na ofisi za chama hicho kata ya daraja mbili hali ambayo ilipelekea wafuasi wa CCM kuwavamia lakini Nasari alijiami na kisha kufyatua risasi tatu hewani.

Hatahivyo, kada wa CCM ,Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema wakati wa majibishano karibu na kituo cha kupigia kura.

Katika vurugu hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha Martin Munis naye aliporwa simu yake ya mkononi na fedha ambapo alitoa taarifa katika jeshi la polisi na kupewa AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Nasari na Lema.

Wakati huohuo,wafuasi wa Chadema waliokuwa mita chache karibu na kituo cha kupigia kura cha sekondari ya Felix Mrema baada ya zoezi la uchaguzi kwisha, wakati wakisubiri matokeo, walivamia ofisi za CCM zilizokuwa karibu na kituo hicho na kisha kujaribu kung”oa bendera ya chama hicho lakini jitihada hizo zilizimwa na wafuasi wa CCM baada ya kumshusha kabla hajaikaribia bendera hiyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya matukio hayo alisema kwamba ni mapema sana kuzizungumzia lakini alikiri kushikiliwa kwa baadhi ya wafuasi wa CCM na Chadema ambao walihusika na vurugu katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake,Nasari alipoulizwa juu ya hatua yake ya kurusha risasi hewani alipinga vikali lakini alipotafutwa Mwalusamba alikiri kurusha risasi hizo hewani huku akidai kwamba alifyatua kwa lengo la kujihami.
Aidha saa nne usiku matokeo yamekemilika na kutangazwa na Modest Lupogo kwa niaba ya kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole ambapo alisema kuwa idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura ni 16295 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 3770 tu.

Akutangaza mshindi (diwani mpya wa kata ya daraja mbili)Lupogo alisema kuwa Prosper Msofe aliibuka kidedea kwa kura 2193 kupitia Chadema, akifuatiwa na mpinzani wake Philip Mushi Philip kupitia CCM aliyepata kura 1324, huku CUF ikipata kura 162, TLP wakipata kura 42, na NSSR kuambulia kura 22

Wakati huo huo katika kata ya Bangata iliyoko wilayani Arumeru mkoani Arusha akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Halipha Idda alisema kuwa Olais Peter kupitia CCM ameibuka kidedea kwa kura 1177 na kuwaacha wapinzani wake Erick Samson Mollel kupitia Chadema kwa kura 881 huku Samweli Saimon Ndosi kupiti TLP akiambulia kura 3.

CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA


Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo)
Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibwaga CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zilizopatikana zimesema, katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
Chadema: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (CHADEMA) na Clement Michael (TADEA) .

Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanyika, zimasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi huo kwa kura.



Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo)

Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo )
CHADEMA YAITOA JASHO CCM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kukipa wakati mgumu Chama cha Mapinduzi (CCM) katika siasa, ambapo kwenye matokeo ya udiwani katika uchaguzi uliofanyika leo, chama hicho kimefanikiwa kutetea kata zake na kunyakua nyingine za CCM.

Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.

Hadi sasa matokeo ya kata 14 yanaonyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.

Matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuikaba CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.

CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.

Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.

CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.

Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.

Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.




Mfuasi wa CHADEMA akiwa na majeraha kichwani baada ya kushambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa vijana wa CCM katika kituo cha kupigia kura Jijini Arusha kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya daraja Mbili Manispaa ya Arusha. (picha: Raha za Pwani)

CCM KATA YA MLANGALI LUDEWA NO, CHADEMA YES

Katika kuonyesha kuwa chama cha mapinduzi (CCM) hakikubaliki katika kata ya Mlangali wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ni baada ya wapiga kura wa kata hiyo kumgalagaza vibaya mgombea wa Chama cha mapinduzi (CCM) Andrew Mhagama na kumchagua na kumchagua mgombea wa Chadema Faraja Mlelwa wa Chadema.
katika uchaguzi huo mgopmbea wa Chadema Bw Faraja ameshinda kwa tofauti ya kura 163 dhidi ya mgombea wa CCM mzee Mhagama na hoja kubwa ya kufanya wapiga kura kutomchagua Mhagama ni kuwa ni mzee ambaye itakuwa vigumu kufanyakazi na mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe (CCM) ambae ni kijana .


CCM YASHINDA UDIWANI SONGEA

Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kutetea kiti chake cha Udiwani katika kata ya MLETELE iliyopo katika manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA baada Mgombea wa kiti hicho MAURUS LUNGU kwa tiketi ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika leo.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo mdogo, msimamizi wa Uchaguzi huo ZAKARIA NACHOA amesema MAULUS LUNGU amepata kura 955 akiwapiga mweleka Mgombea wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA LEOCARDO MAPUNDA aliyepata kura 297, Mgombea SALUM CHALE wa Chama Cha Wananchi CUF aliyepata Kura 27.

Uchaguzi huo umefanyika kwa lengo la kuziba nafasi ya aliyekua diwani wa kata hiyo FLAVIAN LEGELE ambaye alifariki Dunia

Hata hivyo Uchaguzi Mdogo wa kata ya MLETELE uliingia doa siku moja kabla ya siku ya Uchaguzi baada ya wafuasi wa Vyama viwili vilivyokua na upinzani Mkubwa CHADEMA na CCM kushambuliana kwa mapanga ambapo watu sita wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa Mjini SONGEA kwa Matibabu

Miongoni mwa waliojeruhiwa na kulazwa Hospitali ni NYENJE ALLY MPONJI (32), MASHAKA MBAWALA (45) na THABIT SULEIMAN (29) waliojeruhiwa kichwani mikononi na miguuni.

Wengine ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Changarawe aliyeshambuliwa kwa kipigo na majeruhi wengine walitibiwa na kuondoka.

Chanzo cha vurugu hizo ni wafuasi wa vyama hivyo kukutana katika eneo la kanisani na kisha kuanza kushutumiana na ndipo mashambulizi yakaanza katika gari mojawapo lililokuwepo eneo la tukio na ndipo mapigano yalipoanza na haikujulikana silaha aina ya mapanga, fimbo, mawe na magongo yalikotoka na kuanza kutumika katika mapigano hayo.

Magazet Leo Jumatatu oct. 29

Tweeted this Like this, be the first of your Friends








October 24, 2012

PERSONAL DEVELOPMENT: HAPPY PERSON VS UNHAPPY PERSON

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Happy People vs. Unhappy People: 10 Differences - Happiness emfographics by Vadim Kotelnikov with Julia Vostrilova

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VYA AFYA NGAZI YA CHETI, DIPLOMA NA ADVANCED DIPLOMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Ministry of Health and Social Welfare
Majina ya Wanafunzi Wapya na Vituo Walivyopangiwamwaka 2012/13


MWANAJESHI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE WAKATI WA MAZOEZI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mmoja wa marubani wa jeshi amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya ndege waliokuwa wakiirusha kuanguka jijini Dar es Salaam.

Ndege hiyo mali ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWT) ilirushwa na marubani hao wawili na mmoja alifariki dunia wakati akijaribu kuruka baada ya ndege hiyo kupata hitilafu wakati ikiwa hewani.

Tukio hilo limetokea katika kambi ya Jeshi la Anga, Ukonga jijini Dar es Salaam. Mwili wa mwanajeshi aliyefariki umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.

Askari aliyejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ni Kapteni Feruz Kwibika ambaye alipasuka kichwa na kulazwa katika hospitali hiyo. Kwibika alijeruhiwa vibaya baada ya kuruka kutoka ndani ya ndege hiyo kwa lengo la kuokoa maisha yake baada ya kutokea hitilafu hiyo.

Chanzo: http://www.habarimasai.com/

October 23, 2012

ANGALIA PICHA NAMNA WEMA SEPETU ALIVYOFANYA KUFURU YA SHOPPING YA NGUO ZENYE THAMANI YA 4.3 MILION.!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Mrembo huyo alinaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo tu, zenye thamani ya Sh. milioni 4.3 katika duka la Amina Designer lililopo ndani ya Jengo la Quality Centre jijini Dar.

“Ni utamaduni wa kawaida kwangu kufanya shopping mara kwa mara. Sioni uchungu wa kutoa fedha, labda ni kwa sababu natumia kadi kulipia, ningekuwa natoa kwenye pochi na kuhesabu kumpa muuzaji, nisingeweza kufanya hivyo, fedha nyingi kama ile ukiishika mkononi na kulipa kununua nguo roho inauma,” alisema Wema

HIZI NDIZO SABABU ALIZOTOA AUNT EZEKIEL ZA KUANZA NA HARUSI KABLA YA KITCHEN PARTY NA SEND-OFF

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Wiki iliyopita picha za muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel akifunga ndoa zilisambaa kwa kasi kwenye mtandao na kuzua maswali mengi kama iwapo amefunga ndoa kweli ama ni usanii tu. Wengi waliamini kuwa amefunga ndoa na wengi pia walikuwa na mashaka.

Waliokuwa na mashaka walihisi si kweli kutokana na sababu zifuatazo.

1. Aunt Ezekiel alikuwa akiendelea kukusanya michango ya harusi iweje aamue kufunga ndoa wakati bado anachangisha?

2. Kwanini harusi yake isihudhuriwe na watu wake wa karibu hata kama ni ya kiislamu? (kutokana na picha hizo)

3. Aliwahi kuhojiwa na kudai kuwa angefunga ndoa mwezi November

Lakini ukweli kuwa picha hizo zilimaanisha kuwa tayari amefunga ndoa. Lakini kuna sababu za harusi yake kuwa hivyo.

“Ni mchumba wangu na hakika yeye ndiye mwenye maamuzi nikaamua nifanye hivyo,” ameiambia ‘Movie Leo’ ya Clouds FM.

“Naweza sema bado yaani siko sawa mpaka nihakikishe hivyo vitu vyote vimeenda vimepita salama manake unajua shughuli yoyote hata kama ndogo lakini lazima unajua yaani unakaa ni pressure yaani sijui itakuaje sijui itakuwa vipi

Kwahiyo naweza kusema kwasababu ni mwanzo kwahiyo bado kiukweli naona yaani huko mbele kutakuaje.”

Kutokana na kufanya mchakato wake ‘kiflashback’ yaani kuanza na hatua ya mwisho ya harusi na kurudi nyuma, muigizaji huyo pia ameelezea jinsi Kitchen Party za Send-off zitakavyokuwa,“nataka nifanye vitu vya tofauti na kila kitu nataka kiwe tofauti na vile watu ambavyo wamezoea kuviona au wamewahi kwenda , kwahiyo mwisho wa siku nikisema niseme itakuaje, itakuwa hivi itakuwa hivi naweza nikawa nimezusha ugomvi.”

And by the way sasa jina lake ni Rahma baada ya kubadilisha dini na kuwa muislamu.

BINTI AMETOWEKA NYUMBANI, YEYOTE ATAKAYE MWONA ATOE TAARIFA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

NEEMA MKINGA RUGARABAMU mwenye picha hapo juu ametoweka nyumbani kwao na hajulikani halipo. Yeyote atakae muona atoe taarifa kituo cha polisi RB KJN/RB/7279/2012 au apige simu namba 0754546164 au 0715546164 au 0759676654.

Zawadi itatolewa kwa atakayetoa taarifa ya upatikanaji wake!

Asante.

MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI UJERUMANI NA WAFADHILI ! JUMAPILI 28-10-2012 ,MJINI MAINASCHAFF

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)  Unapenda kuwakaribisha Watanzania wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr. 30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya Jumapili Tarehe 28.10.2012, Kuanzia saa 04:00  za Asubuhi.
 
 Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU). 
 
Katika Hafla hiyo Kuanzia saa  9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday'' itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji  ufadhili kupitia Umoja huu.  Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr. Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. 
 
Hafla hii inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.

Umoja wa Watanzania Ujerumani  UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee  Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya. 

Tunawaomba Watanzania Wote  na marafiki wa Tanzania  wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na 
kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu

HAYA NDIO MENO YA TEMBO KUTOKA TANZANIA YALIYOKAMATWA HONG KONG

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Hong Kong authorities confiscated $3.4 million ($26.7 million in Hong Kong currency) worth of ivory found in two shipping containers this week.

The illegal goods weighed more than 8,000 pounds, making it one of the biggest seizures of ivory in Hong Kong.

The containers arrived from Tanzania and Kenya, according to Hong Kong customs officials. The agency seized a total of 1,209 pieces of ivory tusks and three pounds of ivory ornaments from the two containers.

Hong Kong Customs was on alert after a tip-off from Guangdong officials in China. On October 16, Hong Kong officers inspected a container from Tanzania claiming to carry plastic scrap and found $1.7 million worth of ivory. A day later, a second container from Kenya was seized with ivory valued at $1.7 million, according to Hong Kong Customs.

Seven people, including one Hong Kong resident, have been arrested by Chinese authorities in connection to the cases, said a customs spokeswoman.

Hong Kong is viewed as a transit point for the illegal ivory trade, feeding into increasing demands in China, according to a Time article published this week.

Elephants are being killed in Africa at an alarming rate as international demand soars for ivory. Much of the demand comes from increasingly affluent Asian countries, particularly China and Thailand.

The last major bust in Hong Kong occurred in 2011, when officials seized a shipment of ivory and rhino horns valued at $2.2 million in Hong Kong dollars. Priest embroiled in ivory smuggling controversy. Will elephants still roam earth in 20 years? SOURCE: CNN-HONG KONG

MH, HAYA SASA FARID.....NDOO INAMHUSU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Kiongozi wa uamsho Zanzibar...

Magazeti Leo Jumanne oct. 23

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




















Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat